Pages

Ads 468x60px

Wednesday, April 25, 2012

UEFA CHAMPIONS LEAGUE 2011/2012: LEO NI REAL MADRID DHIDI YA BAYERN MUNICH SANTIAGO BERNABEU


LEO NI MPAMBANO WA KUKATA NA SHOKA, BAADA YA CHELSEA KUIVUA UBINGWA BARCELONA HAPO JANA USIKU WA 3;45 KWA HAPA AFRIKA MASHARIKI LEO HII TUNASHUHUDIA MTANANGE DHIDI YA REAL MADRID NA BAYERN MUNICH.



SOMALIA NA CHANGAMOTO YA KUTEGUA MABOMU

Serikali ya Somalia imesema kuwa changamoto kuu iliyoko mbele yake sasa ni kutegua mabomu yaliyotegwa kwenye mitaa ya Mogadishu mji mkuu wa nchi hiyo na kwamba kutokea milipuko mingi kumewazuia wakazi wa mji huo kurejea majumbani mwao.
Serikali ya Somalia imetangaza kuwa licha ya juhudi zinazofanywa na nchi hiyo kwa ajili ya kuyaangamiza mabomu yaliyotegwa katika maeneo mbalimbali ya Mogadishu, lakini maeneo mengi ya mji mkuu huo yanakabiliwa na hatari ya kutokea milipuko. Serikali ya Somalia imesema kuwa si kwamba inapuuza suala la kutegua mabomu yaliyotegwa katika maeneo mbalimbali nchini humo ukilinganisha na kupambana moja kwa moja na wanamgambo wa al Shabab, bali imesema kuwa baada ya kundi hilo kushindwa katika vita na jeshi la Somalia, wanamgambo wake walianza kutega mabomu kwenye mitaa mbalimbali kama mbinu yao mpya.

CHANZO: IRNA