Pages

Ads 468x60px

Thursday, May 31, 2012

DIWANI WA KATA YA INYALA MWALINGO M.KISEMBA KUSHOTO NA MWENYEKITI WA ASASI ZA KIRAIA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI AGGREY KANDONGA AKIJIBU KERO ZA WANANCHI WA INYALA.

BAADHI YA WANANCHI WA MBEYA VIJIJINI WAKIBADILISHANA MAWAZO KATIKA MDAHALO ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA INYALA

Watanzania wenge wamekuwa na kasumba mbaya yakutokuona umuhimu wa mikutano ya vitongoji, vjiji na mitaa hivyo kupelekea kushindwa kuwakilisha karo na mataatizo yao na kuona viongozi waliowachagua kuwa ni watendaji wabovu na wasiowajibika kwao

Hayo yamesemwa na diwani wa kata ya Inyala MWALINGO M. KISEMBA katika mdahalo ulioandaliwa na mtandao wa asasi za kiraia mkoani mbeya (MBENGONET)  kwa malengo ya kuimalisha  mahusiano na kuongeza wigo wa majadiliano kati ya wabunge, madiwani na wananchi

“Jukumu la diwani ni kuchukua matatizo na kero za wananchi  na kuipelekea serikali, Pia kuhamasisha wananchi katika shughuri za maendeleo na kuwawakilisha wananchi katika baraza la madiwani katika halmashauri nakushiliki kupanga bajeti kwa niaba ya wananchi . Hivyo wengi hawapendi kutokeza katika mikutano ya kimaendeleo “ amesema mwalingo.

Kwa upande wa wananchi wameulalamikia uwongozi akiwemo mbunge wa wilaya ya mbeya vijijini LACSON MWANJALA kwakuwa mbali na wapiga kura wake kwani tangu achaguliwe octoba 30/2010 hajawahi watembelea wala kujua matatizo na kero walizonazo na kushindwa mtetezi wa shida zao

Mmoja wa wananchi JOSEPH CHAMBELA alisema wamekuwa na matatizo mengi ikiwa na pamoja na ukosefu wa huduma bora katika hospitali yao haswa ukitumia huduma ya bima ya afya na ukihudumiwa utaambiwa hakuna dawa hivi tunatibiwa bule? Alihoji CHEMBELA

Matatizo mengine ni pamoja na gari la wagonjwa na tunapotaka huduma kwa mama wajawazito na wakati mwingine kuambiwa halina mafuta pia kutopata pembejeo za kilimo mbolea kwa wakati na kwa bei kubwa wakati mazao yanapovunwa huuzwa kwa bei ya chini hivyo kupelekea mkulima kutonufaika na kilimo.

Mwisho wananchi walishauri wilaya ya mbeya vijijini igawe upya kwakuwa ni kubwa sana na kupelekea baadhi ya vijiji kushundwa kupata huduma muhimu kwakuwa zinapatikana mbali, Pia kumpunguzia kajukumu Afisa mtendaji wa kata hiyo anayetumikia vijiji viwili na anaishi mbali na kata anayofanya kazi.


Wednesday, May 30, 2012

MTEMBEA KWA MIGUU ANAYEKADILIWA KUWA NA UMLI KATI YA (25-28) ANAHOFIWA KUFA MALA BAADA YA KUGONGWA NA GARI LA MIZIGO IANA YA LORI LENYE NAMBA ZA USAJILI T425 BLP AMBALO LILIKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AMBAYE HAKUJULIKANA KUTOKANA NA KUKIMBIA MARA BAADA YA KUSABABISHA AJARI HIYO

AJALI HIYO IMETOKEA KIJIJI CHA MLOWO BARABARA YA MBEYA NA TUNDUMA
MMOJA WA MASHUHUDA WA AJALI HIYO AMBAYE HAKUTAKA JINA LAKE LITAJWE ALISEMA CHANZO CHAKE NI MTEMBEA KWA MIGUU HUYO KUINGIA BARABARANI GHAFRA NA KUKUTANA NA GARI HILO AMBALO LILIKUWA NA MWENDO KASI HIVYO DEREVA KUSHINDWA KULIZUI NA KISHA KUMGONGA.

NAYE DEREVA WA LORI HILO MARA BAADA YA KUONA KUWA AMEMGONGA ALIKIMBIA KUSIKO JULIKANA NA KULITELEKEZA LORI HILO AMBALO BAADAE MAOFISA WA POLISI WALIKWEMDA ENEO LA TUKIO KWA KULIONDOA NA KULIPELEKA KITUO CHA POLISI KILICHOPO VWAWA

MPAKA TUNAONDOKA ENEO LA TUKIO HAKUNA ALIYEMTAMBUA MTU HUYO ANAYESADIKIWAKUWA AMEKUFA KATIKA AJARI HIYO

MWILI WA MTU ANAYESADIKIWA AMEKUFA UKIWA UMELALA PEMBENIZONI MWA BARABARANI MARA BAADA YA AJARI KUTOKEA.

BAADHI YA WANANCHI WA MJI MDOGO WA MLOWO WAKISHUHUDIA MWILI WA ALIYEGONGWA NA LORI.

HILI NDILO LORI LILILOSABABISHA AJARI YA KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU.LIKIENDESHWA NA AFISA WA POLISI BARA BAADA YA DEREVA WAKE KUKIMBIA

MWAENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA ILEJE AKISOMA MOJA YA MADA KATIKA MDAHALO ULIOANDALIWA NA MTANDAO WA MASHIRIKA YA KIRAIA MKOANI MBEYA.

WANANCHI WALIOHUDHULIA MDAHALO HUO ILIOFANYIKA KATIKA KATA YA ITUMBA UKUMBI WA RADI WELO WILAYA YA ILEJE.

MMOJA WA WANANCHI WA ILEJE AKICHANGIA KERO YAKE KATIKA MDAHALO HUO

Tuesday, May 29, 2012


MADIWANI  WA YA ILEJE WAMEMKATAA MKURUGENZI WA WILAYA SILVIA SILIWA KWAMADAI KUWA AMEWAKUMBATIA MAOFISA WAKE WANAO TUHUMIWA NA UPOTEVU WA PESA ZAIDI YA MILIONI (80)

AKIONGEA MWANYEKITI WA HALMASHURI YA WILAYA MOHAMED MWALA KATIKA MDAHALO WA MASHIRIKA YA KIRAIA MKOANI MBEYA MBEGONET NA ILENGO NET ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA RADI WELO ITUMBA WILAYANI ILEJE

KATIKA HOTUBA YAKE MWALA ALIPONGEZA UWAJIBIKAJI WA MADIWANI HAO KWA KUONYESHA MFANO KWA KUWAWAJIBISHA BAADHI YA MAOFISA WA HALMASHAURU HIYO AKIWEMO MKURUGENZI NA AFISA MIPANGO MCHUZI LIMBANGA, CHISANGA ALIYEKUWA OFISI YA FEDHA NA WENGINE WENGI.

KWA UPANDE WAKE  SILIWA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA WILAYA HIYO AMEKUBARI KUWEPO NA UPOTEVU WA KIASI HICHO KIKUBWA CHA FEDHA HIZO AMBAZO NI FEDHA ZA WALIPA KODI WA TANZANIA AKIONGEA KATIKA KIKAO NA MADIWANI KUWA UPOTEVU HUO ULIJITOKEZA WAKATI WA UWONGOZI WA NKURUGENZI ILIYEPITA DYAMVUNYE.

“NIKWELI PESA HIZO ZIPOTEA NA NIMEWANIKISHINDWA KUZUNGUMZIA SWALA HILO NI KUTOKANA NA KUTOPEWA USHILIKIANO WA KUTOSHA NA MAOFISA WANGU KWANI TOKA NIMEFIKA SIJAKABIDHIWA OFISI HIVYO KUSHINDWA KUTOA USHILIKIANO WA KUTOSHA NANYI KWA SABABU HIZO NIMEKUWA NA UGUMU WAKUTOA TAARIFA SAHIHI” ALISEMA SILIWA

NAO WANANCHI WALIHUDHURIA MDAHALO HUO WALIKUWA NA MAMBO MENGI YA KUIHOJI SERIKALI JUU YA AHADI WANAZOZITOA KATIKA MAJUKWA WANAPOJINADI KUWA ENDAPO WATAPEWA FULSA YA KUWAONGOZA WATAWATENDEA

HASHIMU KIBONA ALIHOJI AHADI YA UJENZI WA BARABARA ITOKAYO MPEMBA HADI ILEJE AMBAYO ILITAKIWA KUJEGWA KWA KIWANGO CHA LAMI,PIA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA, AJIRA KWA VIJANA WALIOSOMA,MBOLEA NA PEMBEJEO ZA KILIMO.

AKIJIBU HOJA HIZO MWENYEKITI WA HALMASHAURI HIYO MOHAMEDI AMEWATAKA WANANCHI KUWA NA SUBULA KWAKUWA KILA AHADI WALIZOPEWA ZIPO KATIKA MCHAKATO WA KUZITEKELEZA MALA BAADA YA MZUNGUMZO NA WAHUSIKA KIKUBWA NA KWAMBA MPAKA SASA KIASI CHA BILIONI (8) HALMASHAURI IMEZIPATA KAMA LUZUKU TOKA SERIKALINI.




  






Monday, May 28, 2012


UMOJA WA WA MAMA WA WACHUNGAJI NA MAASIKOFU WA JIJI LA MBEYA WAMEWATAKA WATUMISHI HAO KUWA NA UMOJA KATIKA KUFANYA KAZI YA MUNGU, HAYO YAMESEMWA NA MWENYEKITI WA UMOJA HUO RHODA MWAKANANI KATIKA HAFRA ILIYO ANDALIWA LEO TAREHE 28/05/2012 KATIKA UKUMBI WA RAIS WA AWAMU YA TATU BENJAMINI MKAPA
KATIKA HOTUBA YAKE RHODA AMEWAOMBA WACHUNGAJI NA MAASIKOFU KUWA NA UMOJA SHAMBANI MWA BWANA KWANI WANAFANYA KAZI YA MUNGU KILA MMOJA KWA WAKATI WAKE HIVYO NI VEMA WAKAFANYA KWA USHRIKIANO NA UMOJA ILI KUUJENGA MWILI WA KRISTO
HAFRA HIYO  IMEANDALIWANA WAMAMA HAO  KWA MALENGO YA KUWAPONGEZA NA KUWAPUMZISHA WACHUNGAJI NA MAASIKOFU KWA KAZI NGUMU WANAYOIFANYA KILA SIKU KATIKA KUYATEKELEZA MAJUKUMU YAO YA KILA SIKU KWANI WAMEYATAMBUA KUWA NI MAGUMU BILA  MSAADA WA MUNGU HAWAWEZI. 
HAFRA HII IMEKUWA IKIFANYIKA KILA MWAKA KWA KUWAALIKA NA KUWAKUTANISHA PAMOJA  WATUMISHI MBALIMBALI  KWA KULA CHAKULA CHA PAMOJA NA KUWAJENGA KWA MANENO YENYE FARAJA NA TUMAINI ILI KUWATI MOYO NA KUFANYA KAZI ZAO KWA NGUVU MPYA.
VIONGOZI WA UMOJA HUO KATIKATI NI MWENYEKITI RHODA MWAKANANI KUSHOTO NI NDASALAMA MWANSASU KATIBU NA KULIA NI LENA MWAKAJE MJUMBE. (PICHA NA CHARLES MWAIPOPO)


 BAADHI YA MAASIKOFU, WACHUNGAJI NA WAGENI MBALIMBALI WALIOHUDHURIA KATIKA HAFRA HIYO (PICHA NA CHARLES MWAIPOPO)




Sunday, May 27, 2012

ZAWADI ZENYE THAMANI ZAIDI YA LAKIMBILI ZATOLEWA KWA WATOTO YATIMA
             KATIKA SIKUKU YA VIJANA WA KANISA LA MOLAVIANI MBEYA MJINI


KWAYA YA VIJANA USHIRIKA WA MBEYA MJINI MBEYA MORAVIANI TOWN CHOIR (CAMPUN) WAMEADHIMIASHA SIKUKU YAO YA KIKATIBAKATIKA KANISA HILO KWA KUTOA VITU MBALIMBALI VIKIWEMO VITAMBAA VYA KUSHONA NGUO KWA WATOTO YATIMA.

KATIBU WA KWAYA HIYO YOHANA KAJANGE AKIMKABIDHI MCHUNGAJI WA KANISA HILO STEPHANO MWAKIBIBI KWA NIABA YA VIJANA WOTE ILI AWAKABIDHIZAWADI HIYO  VIONGOZI WA NA MCHUNGAJI WA KANISA LA MORAVIANI USHIRIKA WA MSHEWE KWA KUSUDI LA KUWAPELEKEA WATOTO YATIMA  WAISHIO HUKO

"TUMEKUWA NA UTARATIBU WA MUDA MLEFU WA KUTOA ZAWADI KWA WATOTO  WAISHIO KATIKA MAZINGILA MAGUMU NA YATIMA KILA MWAKA KWA VITUO MBALIMBALI IKIWA NI PAMOJA NA KITUO KINACHO MILIKIWA NA KANISA LA MORAVIANI TANZANIA JIMBO LA KUSUINI CHA MBOZI MISSION, NSALAGA NA NURU OPHANS KILICHOPO UYOLE" ALISEMA KAJANGE.

NAYE MCHUNGAJI WA KANISA HILO  STEPHANO MWAKIBIBI AMEWASHUKURU SANA VIJANA HAO KWA MOYO WAO WA UPENDO WALIOUONYESHA KWA KUWAJARI WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGILA MAGUNA NA YATIMA KWANI HILI NDILO AGIZO ALILOTUOCHIA MUNGU UPENDO.

"MUNGU ALITUACHIA NENO KUU KUWA NI UPENDO WA KUWATUNZA WAHITAJI KAMA WAJANE, YATIMA NA WENYE  SHIDA MBALIMBALI KAMA MLIVYOFANYA NINYILEO MMELITIMIZA AGIZO HILO LEO KWA VITENDO MUNGU AWABARIKI ALISEMA MWAKIBIBI"

JUMAPILI HII YA TAREHE 27/05/2012 NI SIKU YA KUADHIMISHA SIKUKUU YA IDARA YA VIJANA (B) KATIKA KANISA LA MAORAVIANI TANZANIA JIMBO LA KUSINI MAGHARABI HIVYO VIJANA WOTE KIJIMBO YAMEADHIMISHA SIKU HII.

MKURUGENZI WA MBEYA MORAVIAN TOWN CHOIR KATIKATI AGGREY KANDONGA LITOA MAELEZO KABLA YA KUTOA ZADI KWA MCHUNGAJI ILI AWAKABIDHI WAWAKILISHI KWA WATOTO YATIMA KULIA NI MCHUNGAJI STEPHANO MWAKIBIBI NA KUSHOTO KWAKE NI MWANYELA MWENYEKITI WA KWAYA YA VIJA KANISA LA BAPTISITI MAJENGO KWAYA RASMI KATIKA SIKUKU HIYO.

MBEYA MORAVIANI TOWN CHOIR WAKIMPELEKEA MCHUNGAJI BAADHI YA ZAWADI ZA WATOTO YAIMA KWANIABA YAO KWA MCHUNGAJI MWAKIBIBI.
MBEYA MORAVIAN TOWN CHOIR (CAMPUN) WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA WALIYOPIGA WAKIWA KATIKA KANISA LA KKKT USHIRIKA WA RWANDA WALIPO HUDHURIA IBAADA YA HARABEE YA UCHANGIAJI WA UJENZI WANYUMBA YA MCHUNGAJI  MWAKALELI.

Thursday, May 24, 2012

VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NA SERIKALI WAMESHINDWA KUJITOKEZA KATIKA MDAHALO WA KUIMALISHA WIGO WA WANANCHI KATIKA KUJADILIANA NA VIONGOZI WAO MDAHALA HUO UMEANDALIWA NA MTANDAO WA MASHIRIKA YA KIRAIA JIJINI MBEYA KWA UFADHILI WA THE FOUNDATION OF CIVIL SOCIETY

VIONGOZI AMBAO WALTAKIWA KUWEPO KATIKA MDAHLO HUOKWA UPANDE WA SIASA NI PAMOJA NA MBUNGE WA JIMBO LA MBEYA JOSEPH MBILINYI, WABUNGE WATE WA VITI MAALU, MADIWANI, MSTAHIKI MEYA ATANASI KAPUNGA, NA MUWKILISHI SERIKALINI MKURUGEZI WA JIJI NA KWA UPANDE WA ULIZINA USALAMA NI OCD.

HATAHIVYO WANANCHI WALIOHUDULIA MDAHALO HUO WALITKA NA TAFSILI TOFAUTI KWA KITENDO CHA KUTO HUDHULIA VIONGOZI HAO NI KUWADHARAU WAPIGA KURA WAO. HATAHI BAADAE WALIJITOKEZA MADIWANI WAWILI TOKA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) BYD N. MWABULANGA KATA YA FOREST NA LUCAS MWAMPIKI KATA YA MWAKIBETE AMBAO WALISEMA HAWAKUWA NA TAARIFA YA MDAHALO HUO.

NAYE KATBU WA SHIRIKA HILO FILIMONI MWANSASU ALITHIBITISHA KUPELEKA TAARIFA YA MDAHALO HUO KWABARUA OFISINI KWA MKURUGEZI NA KUMTAKA MEYA WA JIJI NA MUWAKILISHI WA MADIWANI WAHUDHULIE KATIKA MDAHALO HUO INASHANGAZA KAMA HAKUNA HATA MMJA ALIYEFIKA HIVYO INAASHILIA VIONGOZI KUWA KIMBIA WAPIGA KURA WAO.

KWA UPANDE WA WANACHI WALITOA KRO ZAO JAPO VIONGIZI HAO HAWAPO
BAADHI YA KERO HIZO NI KUPANDA  KWA KODI ZA MAJENGO BILA KUWASHILIKISHA WADAU,MICHANGO YA SHULE IMEKUWA MINGI KIASI CHA KUWA KERO KWA WANACHI, PIABIMA NA PENSHENA KWA WAZEE WAKULIMA WAMESAHAILIKA ZAIDI IPO KWA WAFANYA KAZI NA WATUMISHI WA SERIKALI,AJIRA KWA VIJANA WALIOSOMA NA KIISHIA VIJIWANI KUNAPILEKEA VITENDO VYA UWOVU MITAANI

KERO NYINGINE NI UJENZI WA NYUMBA ZA MAGORAFA MAENEO YA SOKOMATOLA KITU AMBACHO KWA WAMILIKI WA NYUMBA HIZO HAWANA KIPATO CHA KUJENGA MAJENGO HASERIKALI IWATAFUTE WAWEKEZAJI WAINGIE UBIA NA WAMILIKI WA MAJENGO HAYO.

BAADHI YA WANANCHI WALIOHUDHILIA KATIKA MDAHARO HUO WAKICHANGIA MAONI.

MADIWANI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) KUCHOTO NI BOYD MWABULANGA DIWANI FORESTI NA ANAYEMFUATIA NI LUCAS MWAMPIKI WAKIJIBI MOJA YA HOJA ILIYOTOLEWA NA WANANCHI

   HAWA NI BAADHI YA WANANCHI WALIO HUDHURIA MDAHALO HUO AKIWEPO MWANDISHI WA HABARO TOKA SHIRIKA LA UTANGAZAJI (TBC) HESEA CHEYO


MSIMAMIZI WA MDAHARO HUO AGGREY KANDONGA AKIWAJIBIKA IPASAVYO KATKA JUKUMU LAKE ILI KUHAKIKISHA MAMBO YANA KWENDA VIZURI.


MWISHO KATBU WA MTANDAO HUO FILIMONI MWANSASU AKIHIMISHA KWA KUWASHUKURU WANANCHI KWA KUHUDHURIA MDAHALO

WANANCHI WAKITOKA UKUMBINI HAPO HUKU WAKIJADILIANA MAMBO MBALIMBALI

  

Saturday, May 19, 2012

WAFANYA BIASHRA NDOGONDOGO (MACHINGA) WAKIENDELEA NA BIASHARA ZAO MAENEO YA UHINDINI JIJINI MBEYA.

NAO WANUNUZI WANAENDELEA KUPATA HUDUMA HII YA WAMACHINGA KATIKA MAENEO YA UHINDINI JIJINI MBEYA.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

-JIJI LA KIRI  WAMACHINGA KUTOVAMIA MAENEO.
 
-WAPO KWA MUDA WAKATI SERIKALI IKIKAMILISHA MAENEO WALIYOTENGEWA.
-WAMACHINGA  WASEMA TUPO TAYARI KUHAMIA MAENEO MAPYA
 
HALMASHAURI  ya Jiji la Mbeya, imesema wafanyabiashara ndogondogo maharufu kwa jina la (Wamachinga) hawajavamia maeneo wanayofanyia biashara zao sasa  bali wapo kwa muda wakati serikali ikikamilisha miundombinu kwenye maeneo waliyoyapendekeza.
 
Wamachinga hao ni wale wanaoendeshea biashara zao kandokando ya barabara inayoingia kwenye soko kuu la Mwanjelwa pamoja na wale wa barabara inayoanzia eneo la Mafiat kuelekea Soko Matola.
 
Awali, halmashauri ya Jiji la Mbeya, iliwaondoa wa machinga bila ya kuwashirikisha  jambo lililopelekea wafanyabiashara  hao kufanya vurugu zilizoambatana na  kufunga barabara katika eneo la Mwanjelwa, wakipinga kuondolewa katika eneo wanalofanyia biashara zao ndogondogo bila kuoneshwa eneo jipya.
 
Akizungumza na Freedonia Leo kwa njia ya simu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Juma Iddy alikiri kuwepo kwa wamachinga kwenye maeneo yasiyoruhusiwa na kwamba wapo kwa muda wakati wakisubili kukamilishwa kwa eneo maalumu walilotengewa.
 
“Wamachinga hawajarudi, wapo kwa muda wakati serikali ikikamilisha baadhi ya miundombinu kwenye maeneo mapya na ifikapo Mei 30  mwaka huu maeneo hayo yatakuwa yamekamilika,” alisema
 
Aliyataja maeneo hayo kuwa ni eneo la barabara ya Bulongwa-iliyopo nyuma ya Soko jipya Mwanjelwa, eneo la Chuo cha wafanyakazi(OTTU) pamoja na eneo   Moondust-Soweto.
 
 Aidha, Iddy alifafanua kuwa ifikapo Juni 15, mwaka huu wamachinga hao watatakiwa kuhamia kwenye maeneo hayo na endapo watakaidi agizo hilo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
 
Wamachinga kwa upande wao walisema, wapo tayari kuondoka kwenye barabara hizo endapo serikali itawapeleka kwenye maeneo ambayo wameyapendekeza.
 
“Tupo tayari kuondoka kwenye eneo hili la barabara kama serikali itafuata mapendekezo yetu  kuhusu eneo tunalolihitaji,”alisema John Kadege
 
Alisema, moja ya eneo walilolipendekeza ni kandokando ya Benki ya Posta mbali na lile walilopatiwa wahanga wa moto wa soko kuu la Uhindini.
 
Freedonia Leo, lilifanikiwa kuzungumza na mmoja wa wanunuzi wa bidhaa hizo zilizotandazwa kandokando ya barabara Alex Sichale, alisema kitendo cha wafanyabiashara hao kuendesha biashara kandokando ya barabara ni ukiukwaji wa sheria pia ni usumbufu kwa wapita njia pamoja na waendesha magari.
 
 
Akizungumzia suala hilo Diwani wa Kata ya Forest Boyd Mwabulanga kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), alisema wamachinga wanatakiwa kutii na kutekeleza sheria mbalimbali ikiwemo ya uendeshaji wa biashara katika maeneo maalumu.
 
“Halmashauri ipo katika hatua za mwisho za  ukarabati wa miundombinu katika maeneo yaliyopendekezwa na wamachinga wenyewe hivyo watakapotakiwa kuondoka basi kusiwepo na siasa,”alisema
 
Freedonia Leo, lilifanikiwa kuzungumza na Diwani  wa Kata ya Itezi  Frank Mahemba kupitia chama cha mapinduzi(CCM) ambaye alisema mzungumzaji wa suala hilo ni Meya wa Jiji la Mbeya.
 
Jitihada za kumpata Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Athanas Kapunga zilishindikana baada ya kumkosa ofisini na alipotafutwa kwa njia ya simu hakupatikana.
 
Mwisho.