Pages

Ads 468x60px

Saturday, June 30, 2012

INASEMEKANA KUMEKUWA NA BAADHI YA WATENDAJI WA MABENKI KUTOKUWA WAAMIFU KUINGIZA PESA BANDIA KATIKA ATM ZAO KINYEMELA NA KUWAFANYA WANANCHI KUPATA PESA HIZO LAKINI PIA UNAPOCHUKUA ZAIDI YA MILIONI MOJA DILISHANI BASI UTAWEKEWA PESA HIZO BANDIA KUWA MAKINI EWE MTANZANIA
                                                                IJUE PESA BANDIA

Friday, June 29, 2012


SAKATA LA KUGOMA KWA MADAKTARI LIME CHUKUA SURA MPYA MKOANI MBEYA MARA BAADA YA BODI YA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KUWAFUKUZA NA KUWARUDISHA KWA MWAAJIRI WAO KATIBU MKUU WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII KWA HATUA ZA KINIDHAMU NA WALE WAISHIO HOSTELI KUONDOKA MARA MOJA IFIKAPO SAA KUMI NA MOJA NA KUVIACHA VYUMBA KUWA WAZI.
JANA WALIONEKANA MADAKTARI HAO WAKIHAHA KUTAFUTA HIFADHI YAO NA MALI ZAO ILI KUTII AMRI ILIYOTOLEWA NA HOSPITALI YA RUFAA ILIYOWATAKA KUONDOKA MARA MOJA, HALI HIYO IMEJITOKEZA KUTOKANA NA MSUGUANO KATI YA SERIKALI NA MADAKTARI HAO NCHI NZIMA WAKIDAI BAADHI YA HAKI ZAO.
MADAKTARI WAMEKUWA WAKIENDESHA MIGOMO ILI KUSHUNIKIZA SERIKALI KUWATIMIZIA MATAKWA YAO HAYO,NA  HII NI MARA YA PILI KUFANYA MGOMO WA AINA HIYO KWANI MNAMO MWEZI MARCH KULIENDESHWA  MGOMO KWA MADAKTARI NAKU SABABISHA VIFO NA  ADHA KUBWA KWA WANACHI WA TANZANIA.
MNAMO JUNE 23 MWAKA HUU KAMATI YA MADAKTARI ILIBADIKA TANGAZO LAKUANZA MGOMO USIO NA KIKOMO KITU AMBACHO KILITEKELEZWA KWAKUTOKUINGIA KAZINI .
HATAHIVYO MNAMO JUNE 28 MWAKA HUU BODI YA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA ILITOA MAAMUZI YA MAHAKAMA KUU YA KAZI JUU YA MGOGORO WAO HUO KWA KUYABANDIKA IKIWATAKA WASISHIRIKI MAANDAMANO WALA MGOMO  WOWOTE NAKISHA KUTOA WARAKA WAKUWAFUKUZA MADAKTARI HAO.

 Hili ni Tangazo liliwataka madaktari kuanza mgomo Hospitari ya Rufaa Mbeya,
 
PRESS RELEASE
MADAKTARI WA HOSPITAL YA RUFAA MBEYA KUTOTEKELEZA WAJIBU WAO WA KUHUDUMIA WAGONJWA.
Tarehe 22/6/2012 mahakama kuu ya kazi Tanzania (The high cout of Tanzania labour division of the high court at Dar es salam) ilitoa hukumu na. 73 ya 2012(miss Appl no.73 of 2012  kwenye kesi kati ya mwanasheria mkuu wa serikali (Attomey general na chama cha madaktari Tanzania (Medical Association of Tanzania (Mat) hukumu hiyo iliamuliwa wanachama wa MAT nchi nzima  wasifanye wala kushiriki kwenye mgomo. Ninanukuu (I therefore, based on the afore stated reasons do hereby grant the application order temporary injunction the following effect;
That the respondent and its members country, are restrained from colling or participating the strike pending the determination of the application into parties it is so orderd S.C Moshi
                 Judge
              22/6/2012
Hukumu hiyo ilijulishwa kwa wafanya kazi wote hata hivyo,Kuanzia june23mwaka huu Siku ya jumamaosi asubuhi yalibandikwa matangazo sehemu mbalimbali za Hospitali ya Rufaa ambayo yaliwaasa wafanyakazi wagome hayakuwa yameonyesha kuwa yametolewa na nani ila tu ilionyesha imetolewa na KAMATI
Siku hiyo yajune 23mwaka huu Wafanyakazi 15 waliokuwa zamu(Intern Doctor 12 na Registrars 3) hawakufika kazini Tarehe 24/6/2012 wafanya kazi 19 Intern Doctors 15 Registrars 4) hawakufika kazini na kuanzia tarehe 25/6/2012 hadi leo Imethibitika kuwa Intern Doctors 54 Registrars 18 hawakufika hadi leo Tarehe 28/6/2012.
Tarehe 25/6/2012 Bodi ya hospital ilifanya kikao cha dharura hali ya utendaji kazi na utaoji wa huduma hospitalini. Bodi iliamua yafuatayo
1.    Mwenyekiti wa bodi akutane na madaktari ambao hawakufika kazini ili awasikilize sababu za kutofika na kujadili namna ya kumaliza matatizo hayo.
2.    Madaktari wote ambao hawafiki kazini waandikiwe barua za kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kuvunja mkataba walioingia na Hospitali na pia kukiuka kanuni za kudumu za utumishi wa umma Toleo la 2009, kifungu na. f 16-f 17 na f 27
3.    Iwapo madaktari ambao hawafiki kazini hawataripoti au kueleza sababu za kulidhisha ifikapo Tarehe 28/6/2012 kwakuzingatia kanuni za utumishi wa umma toleo la 2009 kifungi na. 16-17 na f 27 madaktari hao watakuwa wamesimamishwa kazi na kurudishwa kwa mwaajiri wao ambaye ni Katibu mkuu wa wizara ya Afya ustawi wa jamii kwa hatua zaidi za kinidhamu zinazostahili
4.    Bodi iliwasiliana na Taasisi mbalimbali hapa Mbeya na nje ya mkoa ili kupata wafanyakazi wa kusaidia kupunguza makali ya katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.

Matokeo ya maamuzi hayo ni kama ifuatavyo:-
 
(i)                Madaktari wote walioalikwa kukutana na mwenyekiti wa Bodi ya hospitali Rufaa Mbeya hawakuhudhuria
(ii)             Barua walizo andikiwa ili kujieleza kwa nini wasichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kutofika kazini hazikujibiwa.
(iii)           Tumepata ushirikiano toka kwa mkurugenzi wajiji kwa kupatiwa madaktari watano kusaidi hospitali ya Rufaa

Leo Tarehe 28/6/2012 madaktari Intern 54 wanapewa barua zao za kuwaeleza kuwa Bodi ya hospitali ya Rufaa Imesitisha Internship yao hapo hospitalini na kuwarudisha kwa Katibu Mkuu wa wizara ya Afya na ustawi wa jamii kwa hatua zaidi zinazosthili. Hivyo kwa wale wanao kaa Hostel waondoke kabla ya saa kumi na moja jioni leo.

Madaktari waajiliwa wanakabidhiwa Barua zao za kusimamishwa ajira yao katika hospitali ya Rufaa Mbeya  na kurudishwa kwa Katibu mkuu wa wizara ya Afya na ustawi wa jamii kwa hatua zaidi za kinidhamu.

Aidha wote wanapaswa kukubidhi mali zote za Hospitali.
Madaktari wakijiandaa kuondoka katika Hostel ya Hospitali ya Rufaa Mbeya. Wakitii Amli ya kuwataka kufanya hivyo.
MADKTARI WA HOSPITAL YA RUFAA MBEYA WAKIONDOKA ENEO LA HOSTEL MARA BAADA YA KUONDOLEWA NA BODI YA HOSPITALI HIYO
 

Wednesday, June 27, 2012

DR STEPHEN ULIMBOKA AKIZUNGUMZA KITU KATIKA MKUTANO WA MADAKTALI.
DR STEPHEN ULIMBOKA BAADA YA KULA KICHAPO NA WATU WASIOJULIKANA

Waandishi wa Habari wa Baraka fm Radio wapata mafunzo ya wiki tatu ili kujengewa uwezo wa kuandaa vipindi vyao. Sana katika mradi wanaotarajia kuanza wa kuandaa vipindi vya kilimo cha mikunde, ili kurutubisha udongo na kuvirusha katika Radio hiyo.
Mafunzo hayo yanafadhiliwa na shirika la Faida Mari, Farm Radio International walioko Arusha na Wizara ya kilimo.
Mradi huu umeanzishwa kwa malengo ya kujibu matatizo ya wakulima katika kurutubisha udongo na kuondokana na matumizi ya Mboleo za kisasa, Kubuni na kuandaa vipindi vitakavyo waelimisha wakulima iliwaweze kujifunza mbinu za kurutubisha udongo, kusambaza taaifa za kurutubisha udongo pi taarifa ya pembejeo kwa wakulima mbalimbali.
Muwezeshaji Felix Kaombwe toka Radio Maria Akielezea kitu kwa waandishi wa habari katika semina inayo endelea katika ukubi wa chuo cha ufundi Moraviani.
Muwezeshaji Ester Mwangabula tika Farm Radio akisikiliza kwa makini wakati wa kujieleza mmaja wa wanansemina.
Waandishi wakiendelea na semina Aliyesimama na Charlee Mwaipopo akichangia moja ya mada



Tuesday, June 26, 2012

    MASIKINI KAUMBA NYOTA CHANGA YENYE NDOTO KUBWA IMEZIMA GAFRA



Vitendo vya ukatili kwa baadhi wanawake na utoaji mimba vimendelea kushamili katika nchi yetu ya Tanzania hivi karibuni kumekuwepo kulipotiwa na vyombo vya habari mbalimbali vikilaani vitendo hivyo
Kwamujibu wa Blogg ya Morogoro Yetu Imebaini kuwa vitendo hivyo vimekilithili sana kwa wanafunzi walioko vyuoni kwani hivi karibuni wameokota mimba ya kitoto kichanga chenye jinsia ya kiume kikiwa kimetupwa katika shimo la maji machafu na baada ya kufuatilia ikagundulika kuwa aliye kifanya kitendo hicho ni mwanfunzi wa chuo cha sua mjini Morogoro.
Hata hivyo vitendo hivi vimekuwa vikisikika kwa wingi hata hapa jijini Mbeya.
Wiki mbili hazijapita Amekutwa ametupwa mtoto wa jinsia ya kiume katika ghuba la kutupa takataka katika shule ya msingi mwenge maeneo ya Soweto, Hazijapita siku nyingi katupwa tena motto mwingine. Maeneo hayohayo.
MALAFYALELEO Blogg Inaweza kubaliana kuwa vitendo hivi vimeongezeka jijini Mbeya Labda ni kutokana na kuongezeka kwa vyuo ukweli wa mambo haya utaugundua kuwa limekuwa ni jambo la kawaida kuokotwa vitoto vichanga vikiwa vimetupwa katia mashimo ya vyoo na malanyingine katika baghuba ya takataka.
Hivi ukatili huu utakuwa na majibu gani kwa mwenyezi mungu, Sitaki kuamini kwamba mtu hushika mimba kwa bahati mbaya kama Rugha za wengi hupenda kujitetea, sikubari kushawishiwa na maneno hayo yananitia kichefuchefu We msomi mzima unapanda mbegu usiyo taka kuota na kuivuna inaingia akilini hiyo? Hata hivyo ni kwanini Mnaogopa mimba kulika UKIMWI?
Pumbavu, mjinga wewe Unawezaje kufanya tendo la ndoa bila kutumia kinga? Kwanini mnafanya vitu kama vipofu? Kwanini mnazikosesha haki ya kuishi Roho zisizo na hatia?Kwanini lakini nyie watu mnawaza niniiii jamani mimi ningelikuwa mungu sijui ingekweje?
                           Hasira Imenizidi Tukutane wiki ijayo. 
Mtoto alekutwa ametupwa katika ghuba la Takataka shule ya msingi Mwenge soweto
 

Zaidi ya watuhumiwa (88) wametiwa mbaloni na jeshi la polisi kwa makosa mbalimbali ikiwemo wizi wa kuvunja na kubomoa lakini pia wizi wa mafuta ya magari yanayofanya shughuri za ujenzi wa barabara ya Tunduma na sumbawanga.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda Athumani Diwani amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika msako unaoendelea mkoani mbeya tangu tarehe 08/06/2012 mpaka hivi leo vitu mbalimbali vimekatwa.
Diwani amesema vitu vilivyo kamatwa ni pamoja na pikipiki tatu (3) Zenye usajiri no T489 BQU aina ya Sanya T584 BPU aina ya STAR T301 BRU aina ya saug Vitu vingine ni simu za mkononi,computer laptop, Bunduki mbili aina ya shotgun na Risasi kumi na mbili Vitu vingine ni Tiv, Radio, nk
Kamanda Diwani ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Mbeya kutoa ushirikiano wa kutosha kwa jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za uharifu ili kuliweka mji wetu katika hali ya usalama zaidi, Lakini pia kwa upande wa wa halifu  A mewataka kuacha mara moja kwakua Biashara hiyo haitalipa tena katika mkoa huu.
Kisha akawataka wananchi kufika polisi kituo cha kati kwa ajili ya kuweza kuvitambua vitu vyao iwapo mtu alipotelewa ama kuibiwa kitu.
  Kamanda Athuman Diwani akiongea na Waandishi wa Habari Nje ya ofisi yake mkoani.
 Kamanda Diwani Akionyesha Bunduki mbili zinazozaniwa kuhusika na vitendo vya uharifu zilizo tengenezwa kienyeji na kutumia risasi za kawaida lakini zinauwa.
     Hivi ni Baadhi ya vitu vilivyokamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani mbeya