Pages

Ads 468x60px

Monday, July 23, 2012

 Rais Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na madiwani 
 Rais Dr. Jakaya Kikwete akiwa anashuka kwenye ndege

Hivi ndivyo uwanja wa Kimataifa wa Songwe unavyo onekana kwa sasa
 Rais Dr Jakaya Kikwete akiwa anapita kati kati ya watoto skaut
RAIS JAKAYA KIKWETE NA KULIA KWAKE NI  KAMISHNA WA UMOJA WA ULAYA KITENGO CHA MAENDELEO ADRIS PIEBALGS  PAMOJA NA BAROZI WA UJERUMANI WAKIKATA UTEPE KWA PAMOJA KUZINDUA MRADI WA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA JIJINI MBEYA

RAIS KIKWETE AKIHUTUBIA WANANCHI WA MBEYA KATIKA UZINDUZI WA MRADI WA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA          

Thursday, July 19, 2012

BOTI YA KMKM IKIWA KATIKA ZOEZI LA KUOKO MAJERUHI WA MELI ILIYOZAMA
BAADHI YA ABILIA WAKIWA KATIKA CHOMBA CHA KUOKOLEA WAKISUBIRI KUOKOLEWA
                MMOJA WA WAOKOAJI AKIWA NA MOJA YA MAITI YA AJARI HIYO
                        ASKALI WA UOKOAJI WAKITOKA MAITI WA AJARI HIYO
        MADAKTARI WAKITOA HUDUMA YA KWANZA KWA MAJERUHI WA AJARI


HAWA NI BAADI YA MAJERUHI WALIOKWISHA PATIWA HUDUMA YA KWANZA

Wednesday, July 18, 2012

SAKATA LA NDOA YA PADRI DR. SLAA NA WASEMAVYO UWAZI



Dk. Willibroad Slaa na mchumba wake, Josephine Mshumbushi.
Josephine na Mahimbo siku ya ndoa yao.

Hati ya talaka kati ya  Josephine Mshumbushi na Aminieli Mahimbo.

Na Makongoro Oging’

SAKATA la ndoa ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibroad Slaa na mchumba wake, Josephine Mshumbushi limefichua siri mpya kuhusu maisha yao ya kimapenzi.

Siri hiyo, inahusu historia ya mateso aliyowahi kuyapata Dk. Slaa kutoka kwa mwanamke ambaye jina lake linahifadhiwa, kabla ya kuamua kuinua mikono na kudondokea kwa Josephine.

Imebainika kuwa wakati Slaa analo lake la kuteswa na mwanamke wake, Josephine naye ana siri inayomuumiza kutokana na yale aliyotendewa na mwanaume wake (jina tunalo), aliyekuwa naye kabla ya kutua kwa mwanasiasa huyo.

Josephine, amekiri wazi kwamba mwanaume wake aliyepita, alimtesa na kumdhalilisha kiasi cha kumfanya kuchangia mapenzi na wasaidizi wa kazi za nyumbani (ma-house girl).

Dk. Slaa, alipozungumza na mwandishi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwake, Tegeta, Dar es Salaam, alikiri kuteswa na mwanamke aliyewahi kuwa naye kabla ya Josephine kisha akaelekeza kila kitu kuhusu maisha yao na uhusiano wao, kizungumzwe na mchumba wake huyo.

Akieleza mambo kwa mtindo wa kuchambua, Josephine alisema, haoni sababu ya kutoolewa na Dk. Slaa, kwani anampenda kupita kiasi na kwamba kiongozi huyo alikutatanaye Dodoma akiwa amekondeana kwa mawazo kutokana na mateso ya mwanamke huyo (jina bado tunalihifadhi).

“Mimi na Dk. Slaa tulikutana bungeni. Mimi nilikuwa pale kama mtumishi wa bunge, yeye alikuwa pale kama mbunge wa Jimbo la Karatu. Uhusiano wetu ulianza kule. Sasa nimemtunza na amenenepeana watu wanaanza kumtamani. Huyu ni wangu.

“Watu wamuone Dk. Slaa hivi sasa, hapo kabla alikuwa anateseka. Hakuwa na mwili huu ambao watu wanamuona nao. Mwanamke wake wa zamani alikuwa anamnyanyasa, kila siku baba wa watu anashinda na kukesha kwa mawazo, sasa hivi katulia. Nampa huduma nzuri, nampikia mapochopocho ndiyo maana ananawiri,” alisema Josephine.

Aliendelea kusema, kama kuna watu wanaamini yeye hatafunga ndoa na Dk. Slaa, wanajidanganya, kwani wanazo haki za kimsingi za kutimiza azma yao.

“Mimi najua Slaa ana watoto aliozaa na mwanamke mwingine, hata mimi nimeishi na Slaa miaka minne na tumezaa mtoto mmoja. Nimeishi na Slaa bila ndoa kwa muda mrefu na sasa tumeamua tufunge ndoa Julai 21, mwaka huu,” alisema Josephine.

Aliendelea kusema: “Nitafurahi sana nikishatimiza hii azma ya kuolewa na Slaa. Ni mume mzuri hasa, namuomba Mungu akamilishe malengo yetu. Unajua huko nyuma niliwahi kuteswa na mwanaume, niliishi na mwanaume asiyejua thamani ya mke.

“Huyo mwanaume alikuwa anasababisha nichangie mapenzi na ma-house girl, kwani kila house girl niliyemuajiri, alitembea naye. Sasa hivi yote hayo yamekwisha. Dk. Slaa anajiheshimu, sina tena vurugu za mwanaume wangu kutembea na house girl.”

Kuhusu matarajio ya kimaisha, Josephine alisema kuwa anaamini panapo majaliwa baada ya kufunga ndoa na Dk. Slaa, wataishi raha mustarehe kwa sababu wanaelewana vizuri.

“Raha ya maisha ya ndoa ni kuelewana, ndiyo maana nasema sioni sababu ya mimi na Dk. Slaa kutofunga ndoa. Tunapendana na kuelewana sana. Dk. Slaa akiondoka kwangu, hatapata mwanamke atakayeelewana naye kama mimi. Hata mimi siwezi kumpata mwanaume wa kuelewana naye kama ilivyo kwangu na Slaa.

“Jambo pekee ninaloweza kuwaomba Watanzania ni kutuombea tufunge ndoa yetu salama, atukinge na maradhi ili tuendelee kuishi raha mustarehe na tuendelee kutetea masilahi yao,” alisema.

Aliongeza kuwa maandalizi ya ndoa yao yamekamilika na kilichobaki kwa sasa ni siku ifike ili watawazwe rasmi kuwa mke na mume.

KILICHOPO JUU YA DAWATI
Wakati Josephine na Slaa, wakieleza mipango yao ya ndoa, kwa upande mwingine, Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Mkoa wa Manyara, Rose Kamili, amewasilisha pingamizi mahakama kuu, akidai kuwa, Dk. Slaa ni mume wake halali.

Rose ambaye ni mzazi mwenza wa Dk. Slaa, aliwasilisha hati ya pingamizi Mahakama Kuu, akitaka pia alipwe fidia ya shilingi milioni 550.

Alitaka Dk. Slaa amlipe shilingi milioni 50 kwa kitendo chake cha kumtelekeza na watoto, akaomba pia Josephine amlipe shilingi milioni 500 kwa kitendo cha kumsababishia maumivu makali baada ya kumchukulia mume wake.

Mbunge huyo alidai kuwa yeye na Dk. Slaa walifunga ndoa ya kimila tangu miaka ya 1980, baada ya katibu huyo wa Chadema kuachana na ukasisi wa Kanisa Katoliki (Upadri), hivyo yeye ni mke halali mwenye stahili zote.

UNAKUMBUKA SAKATA LA MAHIMBO?
Awali, ilionekana kwamba pingamizi la ndoa ya Dk. Slaa na Josephine lingetoka kwa mwanaume anayeitwa Aminieli Mahimbo.

Mahimbo, alikuwa mume wa ndoa wa Josephine na ndoa yao ilifungwa mwaka 2002.

Hata hivyo, Uwazi limenasa talaka inayowatenganisha rasmi Josephine na Mahimbo, iliyotolewa na Mahakama ya Mwanzo, Manzese, Dar es Salaam, Aprili 16, mwaka huu, hivyo kuthibitisha kwamba hakuna kizuizi tena upande huo.
0 comments

Katika hali isiokuwa yakawaida mwanamke mmoja mkazi wa Isanga jijini Mbeya amejitosa kwenye kazi iliyozoweleka na wanaume yakuendesha bajaji ili kujikwamua kimaisha.
Mwanamke huyo mkazi wa Isanga Jiji Mbeya Jasmini konga amesema hayo wakati akiwa katika shughuli zake akizungumza na blog ya malafyale na kuwataka wanawake kuondokana na matazamo potofu kuwa kuna kazi zinazo fanywa na wanaume tu.
Jasmini amesema kilichomvutia kufanya kazi ya kuendesha bajaji ni kutaka kuona kwamba hata wanawake wanaweza na pia ameipenda kwakua inamsaidia kupata kipato sha kujikimu kimaisha akisaidiana na mume wake kuendesha maisha ya kila siku nakuongeza kuwa muda mlefu alikuwa akiitamani  kazi hiyo hivyo anafurahia kutimiza ndoto yake.
Amesema licha ya changamoto nyingi anazokutana nazo akiwa barabarani bado hakati taamaa ikiwemo kuwahi kupaki mapema bajaji yake kutokana na majukumu mengine ya kutunza familia kwani ana mume na mtoto hivyo kusababisha wakati mwingine kutofikisha malengo ya tajiri yake.
 Mwanamke huyo amesema malengo yake ya baadae ni kuona anamiliki Bajaji yake mwenyewe ili kuwa huru zaidi kwa kijiajiri na kupata kipato chake.
Naye Abdalla Muhamed mmoja wa madereva hao ameitaka jamii kuheshimu kazi za madereva hao kwani inawapatia kipato chao cha kila siku hivyo kuizarau ni kuwakatisha tamaa vijana .
Dereva wa Bajiji Jasmini Konga akiwajibika katika Bajaji yake akiwa na Mtoto wake wa kiume
 Jasmini akiwa katika mkao wa kuondoka maeeneo ya kuegesha Bajaji karibu na jengo la Kasisi Mwanjelwa.

Wednesday, July 18, 2012

BREAKING NYUUUUZZZ
KWA HABARI ZILIZOIFIKIA HIVI KARIBUNI NI KWAMBA MELI YA ABIRIA ILIYOKUWA IKITOKEA JIJINI DAR-ES-SALAM KUELEKEA ZANZIBAR INAYOTAMBULIKA KWA JINA LA SKAGET IMEPINDUKA NA INAZAMA NA ILIKUWA NA ABIRIA ZAIDI YA 200 KATIKA KISIWA CHA CHUMBI MPAKANIA MWA DAR-ES-SALAM NA ZANZIBAR  NA VIKOSI VYA UOKOAJI VINAELEKEA HUKO KWA HABARI ZAIDI ENDELEA KUTEMBELEA MTANDAO HUU WA KIJAMII

KANISA LA MORAVIANI TANZANIA KUWATENGA WAUMINI WAKE WATAKAO OA AMA KUOLEWA NA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU.
WALIOPATA KIPAIMARA WATATENGWA WENYEWE WASIOPATA KIPAIMARA KUTENGWA WAZAZI WAO.
Hayo yamesemwa na mchungaji ALIYIZA SILUMBWE wa Kanisa la Moraviani Tanzania Jimbo la kusini Magharibi ushirika wa Chindi Wilyani Momba, Akiongea wakati wa kuendesha ibaada ya sikuku ya umoja wa akina mama iliyo fanyika kimtaa katika kanisa la Moravia ushilika wa Msangano Silumbwwe aliwataka wazazi kutowakubalia watoto wao kuoa ama kuolewa na waumini wa dini ya Kiislamu.
“Ndugu zangu wenzetu waislamu wamepanga mikakati ya kuumaliza ukristo kwa kuwashauri vijana wao kuoa mabinti zetu kwa gharama kubwa na kwa mabiti wao waolewe na vijana wetu kwa ahadi za kuwapa mali na mitaji ya kuanzia maisha katika ndoa zao ila wauache ukristo sasa basi kama kanisa limegundua hilo na kutoa tamko kuwa kila muumini asikubali mototo wake kuolewa na mtomto wa kiislamu”amesema Silumbwe.
 Maandamano ya wachungaji na akina mama katika sikuuu ya umoja wa akina mama mtaa wa Msangano Wilayani Momba.
 Mchungaji Aliyiza Silumbwe Akisisitiza jambo wakato wa ibaada hiyo
 Mwalimu wa shule ya jumapili mwanye ulemavu wa macho ushirika wa Msangano Mwenyekipaji cha aina yake kwa kusoma vifungu vyote vya Biblia. 
 Huu ni mnara wa kumbukumbu ya mwinjilisti wa kwanza AMBILISHISHE MWACHANIKA kupeleka Injili katika Bonde la Unyamwanga mwaka 1907-1911 Mnara huu umejengwa nje ya kanisa la Moraviani ushirika wa Msangano.


KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA

TAMKO  LA DODOMA


MSIMAMO WA KANISA LA KIINJILI LA KILUTHERI TANZANIA KUHUSU NDOA ZA JINSIA MOJA.

1.   Utangulizi
  1.1 Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT), Linamshukuru mungu kwamba katika hekima yake isiyopimika, na kwa njia ya mwana wake Yesu Kristo ametuunganisha waumini wake wote ulimwenguni kuwa mwili mmoja na hivyo kutufanya tuhusiane. Kwa kwa njia hiyo tunaweza kutembea pamoja na kufanikishwa katika mambo mengi.
1.2 katiak uhusiano wetu kama mwili mmoja tumeshilikiana katika mambo magumu na mepesi kilichotuwezesha kudumu pamoja hadi sasa, kwa msaada wa mungu, ni kutambua na kukumbuka kwamba kila siku ya ibaada, tunakili kuwa kanisa la mungu ni moja, takatifu  ulimwengu pote na la kimitume. Hivyo, tukio lolote katika kanisa mojawapo, lisilo la kawaida katika misimamo na mafundisho yaliyozoeleka kwa karne nyingi katika kanisa la mungu,ni lazima litaamsha mshtuko na itikio la aina moja au nyingine kutoka makanisa mengine duniani pote.

1.3 Kwa wakati uliopo. Mojawapo ya matukio yasiyo ya kawaida, kwa mtazamo na uelewa  wa KKKT, ni hilo la baadhi ya makanisa - hasa kule  ulaya  na Marekani – kuamua kuhalalisha ndo za watu wa jinsia moja katika kufanya hivyo,sababu mbalimbali zinatolewa na makanisa husika uwamuzi wao huo. Hapa tutaje tu, kwa muhtasari baadhi ya sababu zinazo tolewa na makanisa hayo.

1.3.1 Kwamba eti mafundisho ya kanisa kwa ndoa, kulingana na maandiko matakatifu,  ni kati ya mwanaume na mwanamke si kama inavyo fafanuliwa. kwa msingi wa hoja kama hii, hao wanao tetea ndoa za watu wa jinsia moja wameanza kusama kila linalo wezekana  kubomoa kifungu kimoja  baada ya kingine  kinachoonyesha kwamba ndoa halali, kibablia, ni kati ya mwanaume na mwanamke. Wanafanya hivyo kwa kuleta tafsiri zao “ mpya na yamkini potofu” – tofauti na msimamo wa kanisa uliodumu kwa miaka mingi  kuhusu maana ya ndoa kulingana na mafundisho ya neno la mungu. Baadhi ya vifungu vya Biblia vinavyo pigwa vita  na kupewa tafsili nyingine  na wapenda ndoa za watu wa jinsia moja ni hivi vifuatavyo: Mwanzo 1:26-28; 2: 24;
Mt. 19: 5-6a; Rum. 1:26-27a na Gal. 3:28

1.3.2 Kwamba eti kilicho muhimu, kwa habari za mahusiano kati ya wawili wahusika katika mahusiano ya kindoa au namna nyingine za mahusiano ni upendo. Mradi watu wanapendana, mahusiano kamahayo ni sahihi na halali ndivyo wanavyodai watetezi wa ndoa kati ya watu wa jinsia moja.

1.3.3 Kwamba eti mazingira na tamaduni zao za wakati huu ni tofauti na zawakati uliopita kuhusu maana na mtazamo juu ya nini halali na nini si halali  kwa mahusiano ya kindoa na kimapenzi. Wanaongeza kudai kuwa swala la maadili kuhusu nini ni dhambi na nini si dhambi, hubadilika kulingana na wakati na mazingila ya mahali mtu alipo. Kwa macho yao, mtazamo wa jamii juu ya maadili, hasa kuusiana na swala la mahusiano ya kindoa au kimapenzi kati ya watu wa jinsia moja au jinsia tofauti umebadilika, na wanalitaka kanisa nalo liende na wakati katika mtazamo ama msimamo wake kuhusu mambo haya . kadhalika wateteaji wa mambo wanadai kwamba, “tabia za kukemea na kukunjia uso mambo ya ndoa za watu wa jinsia moja zimepitwa na wakati,”  Hivyo , wanatutaka sisi wengine wote katika kanisa la mungu na jamii ya ulimwengu kwa ujumla tukubali kubadilika na kwenda na wakati, kama wao, katika mazingila haya mapya!

1.3.4 Kwamba eti kwa kuwa sheria za nchi hizo yaliko makanisa yanayo tetea na kuhalalisha ndoa za watu wa jinsia moja zimebadilika na kuwa upande wa ndoa za aina hiyo, makanisa katika nchi hizo yangejikuta pagumu sana katika kazi na maisha yao kama yangeng’ang’nia msimamo wao wa miaka yote iliyopita kuhusu ndoa kati ya watu wa jinsia moja, na maswala mengine ya mahusiano kati ya watu wa jinsia hiyo moja. Maana yake, kwa tafsiri yetu, makanisa hayo yameamua kukabiliana na hatua zilizochukuliwa na mamlaka ya nchi zao kama njia ya majadiliano ili hayo makanisa yasije yaka poteza maslahi yao fulan katika swala zima la ndoa endapo yangeendelea kushikilia msimamo wao wa miaka yote iliyopita – yaan, kupinga na kukataa uhalali wa ndoa za watu wa jinsia moja.
1.3.5 Kwamba eti suala la mahusiano – kindoa au kujamiiana ki-namna nyingine – kati ya watu wa jinsia moja, ni uamuzi wa kati ya watu wawili wanaohusika; wana uhuru kuamua kufanya wapendavyo katika hili. Kwahiyo dai la msingi ni kwamba siyo sawa kwa yoyote kuwaingilia katika mambo yao hayo, bali kuwaacha huru wafanye wapendavyo. Na makanisa yaliyo halalisha ndoa za watu wa jinsia moja.

2. HOJA MBADALA
2.1kuhusu hoja zitolewazo na watetezi wa ndoa za watu wa jinsia moja, Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania lina mtazamo na msimamo tofauti. Halikubaliani na sababu zozote zinazotolewa watetezi wa ndoa za aina hiyo na uhalalishwaji wake.

2.2 Kanisa hili, (KKKT), Linasimama juu ya msingi wa neno la mungu kwamba maana ya ndoa ni kama inavyo fundishwa katika vifungu vya Biblia vilivyo tajwa sehemu ya 1.3.1 hapo juu. Vifungu ambavyo vimeanza kupewa maana na tafsiri  tusiyoweza kuikubali.  Sisi na wengine wote  duniani pote wlio na msimamo kama wetu katika swala hili la kupinga ndoa za watu wa jinsia moja, tunaamini kuwa Biblia haitafsiriwi ka wapendavyo watu Fulani au mamlaka Fulani ama utamaduni Fulani bali hujitafsiri yenyewe  kwa rugha mbalimbali kwa usahihi wake usio badilika

2.3 Kanisa hili linaamini kwamba upendo ni kiini cha mapenzi na uhusiano wa kweli Kati ya watu wawili wanaoishi, au wanotaka kuishi pamoja, katika ndoa. Lakini, kwa habari ya kuolewa na kuoa, upendo huu ni kati ya watu wawili wa jinsia tofauti. Aidha KKKT inaelewa somo juu ya upendo ni pana sana, na kwamba kuna maadili maalumu kuhusu matumizi sahihi ya karama hii ya upendo ua kupendana. Kanuni maadili kuhusu maana sahihi ya upendo na matumizi yake zinapokiukwa ua kuanza kupindishwapindishwa kwa sababu yoyote ile, basi upo uwezekano mkubwa wa binadam kujikuta katika hali ambayo neno upendo upo kati ya watu wawili wahusika, basi ndoa ya aina yoyote inakubalika . Hoja hii ikikubalika kanisa na jamii kwa ujumla tunaweza kujikuta mahali ambapo tunaanza kurudia na kutetea ndoa hata kati ya wana na ndugu, wazazi na watoto napengine hata kati ya binadam na wanyama – si mladi kinachowaunganisha hao viumbe wawili kinaitwa upendo! Haidhuru ni tafsiri gani imetolewa? Tunacho taka kusisitiza hapa ni kwamba, tuwe waangalifu sana tunapo zungumzia neno upendo ha kudiliki kufanya kuwa kigezo muhimu na pekee kuliko vyote katika swala la ndoa.

2.4 Jibu liliotangulia, hapo juu, linahusu pia uhalalishwaji na ushabikiaji wa ndoa za watu wa jinsia moja kwa hoja kwamba katika tamaduni na jamii za watu wa nchi zile ambako ndoa za jinsia moja zimehalalishwa, pamekuwepo na mabadiliko makubwa katika fikra za watu. Watu hawaonitena kwamba ni vibaya wala kutokuwa halali kwa watu wa jinsia moja kuoana. Utamaduni wao wa sasa una mwelekeo unaoungua mkono ndoa za jinsia hiyo. Mtazamo wa kimaadili wa sasa ni tofauti na wakati uliopita. KKKT inakubali kuwa nikweli misimamo Fulani ya kimaadili inaweza kubadilika kulingana na watu wako wapi na niwakati gani. Lakini waumini wa KKKT wanajua na kuamini kuwa kuna mambo yasiyo badilika kama pua kutobadilika kuwa mdomo au masikio kuwa macho.

2.5 Ni kweli kuwa maadili yaliyo angaliwa na jamii kwa mwelekeo hasi miaka iliyo, sasa yaangaliwa kwa mwelekeo wa chanya au kulidhia. Ni dhahili kuwa wakani wa sasa na tofauti, na jamiiimebadilika katika mwelekeo na mtazamo wake katika mambo mengi. Lakini ni kweli, vilevile, kwamba maadili na msimamo wa kanisa na wa jamii kwa ujumla, haviwezi kuwa na misingi ya kimaadili inayo yumbayumba wakati wote. Ni lazaima na jamii viwe na kanuni za kimaadali zinazoweza kihimili mabadiliko ya kijamii, kisayansi, kisiasa, kiuchumi, nk.kanisa hili linaamini kuwa, kwa msingi wa mafundisho ua neno la Mungu, yako maadili yasiyopaswa kubadilishwa na kupindishwa pindishwa na misukumo ya mabadiliko ya wakati, hali na mali.Mojawapo katika hayo, yahusu suala la ndoa na maana yake.Aidha kukubali ndoa za watu wa jinsia moja ni kuhujumu msingi wa agizo la Mungu kuhusu uumbaji unaoendelea.

2.6 Aidha, mabadiliko ya kimaadili katika jamii moja, mahali Fulani, tuseme Ulaya na Marekani, yasichukuliwe kama ndio mwongozo kwa mabadiliko mahali pengine pote ulimwenguni. Wala mabadiliko yao ya kitamaduni, kijamii, nk, katika nchi za Ulaya na Marekani yasilazimishwe juu ya watu wa nchi nyingine au makanisa katika nchi hizo. Kwa sababu hao watu wa sehemu nyingine, nje ya Ulaya na Marekani, pia wanamisingi yao kijamii inayolinda maadili yao. Sisi kama watanzania/Waafrika, tuna maadili yetu yaliyojengwa juu ya misingi ya tamaduni zetu bayana ambazo zinatambua mahusiano, ki – ndoa, kati ya watu wa jinsia tofauti. Kwa hiyo, kama watu wengine watasema kwamba wanahalalisha ndoa za watu wa jinsia moja kwa kuwa mazingira mapya ya mahali na wakati walipo yanaruhusu hayo, basi ieleweke kuwa mazingira ya wakati na tamaduni zetu hayaruhusiwi mambo hayo

2.7 Hoja ya kwamba ndoa au mahusiano kati ya watu wa jinsia moja ni jambo la watu wawili , ni hoja ya upande mmoja. Kwetu sisi waumini wa KKKT kwa upande wa pili tunabainisha kuwa hilo siyo tukio kati ya watu wawili tu bali inaeleweka daima kuwa wao ni sehemu ya familia na jamii pana zaidi. Hao wawili hawawezi kuruhusiwa kujifanya mambo hata yasiyokubalika na jamii, kwa kinga ya: “Tuache peke yetu,msituingilie katika mambo yetu; haya ni mambo yetu wenyewe, na ni uamuzi wetu wenyewe, kufanya tulivyoamua kufanya,” nk. Hapana! Katika Kanisa na jamii kwa ujumla, kwa kadri tunavyohusika katika mazingira na utamaduni wetu, kuna mambo ambayo binadamu yeyote, haidhuru yuko wapi, sharti atambue kuwa yeye si peke yake na wala hapaswi kuishi kwa nafsi yake tu katika mambo yote na wakati wote. Ndio ilivyo katika suala hili la ndoa za watu wa jinsia moja.

3. HITIMISHO
3.1 Kwa hiyo basi, kwa msingi wa ufahamu wa kanisa moja, na kwa kuona ulazima wa kuongoza kanisa Kichungaji, kwa kufuata ufahamu wa Neno la Mungu na maungamo yake. Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania linapenda kuonyesha bayana  msimamo wake wa sauti ya kinabii, kuhusiana na suala  la ndoa za watu wa jinsia moja, kwamba ni msongo mwitu na mwiba mkali katika mwili wa Bwana Yesu Kristo (1 kor. 12: 12- 27) unaosababisha jeraha lenye maumivu makali kwa wana KKKT na wengina wengi wa mahali pengine ulimwenguni pote wenye msimamo kama wetu katika suala hili, katika ngazi mbalimbali za uhusiano na mfumo wa uongozi.

3.2  Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania linaona kuwa maamuzi yoyote ya upande mmoja yasiyoendana na uelewa na mtazamo wa pamoja katika suala la ndoa  kati ya watu wa jinsia moja yanadhoofisha umoja wa kanisa lote kama mwili wa kristo.

3.3 Kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania bado linakataa utumiaji usio sahihi na tafsiri potofu za maandiko Matakatifu ili kuhalalisha ndoa za watu wa jinsia moja.

3.4 Tunaamini kwamba hakuna sehemu yoyote ya kanisa la Mungu inayoweza kufaulu kutatua mambo yake yote peke yake, bila nguvu ya pamoja ya mwili mzima wa Kristo. Kama isemwavyo:  Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. Jambo hili la maamuzi kuhusu kuhalalishwa kwa ndoa za watu wa jinsia moja, limeonyesha dhahiri kwamba nguvu ya umoja wetu imedhoofishwa.

3.5 Bila shaka haitoshi wala haisaidii tukiishia katika kulaumiana na kuhukumiana kutokana na tofauti zetu juu ya suala hili. Busara na hekima ya Roho Mtakatifu, itusukume kuzama katika maombi, toba, kuendelea kushauriana, kuonyana na kusaidiana katika roho ya upendo wenye misingi ya Neno la Mungu (Kol. 3:5 – 17)
3.6 Tunapenda kuwatia moyo na kuwaunga mkono kwa dhati wale wote, katika makanisa yote ulimwenguni- wawe wengi au wachache wanaopinga, uamuzi wa kuhalalisha ndoa za watu wa jinsia moja. Tunatoa wito kuwa, sisi sote kwa pamaja tuendelee kuwa chumvi na nuru katika uhusiano wetu. Tukierekeza nguvu zetu katika kudumisha umoja na ushilikiano kati yetu. Umoja utatuwezesha kutoruhusu tena hali itayoleta majeraha zai kwenye mwili wa kristo, yaani kanisa.
3.7 Tunaona kwamaba hizi ni nyakati za uovu unao tafuta kulididimiza kanisa la mungu. Kwa hiyo tunatoa wito kwa waumini wote wa KKKT na makanisa mengine yenye msimamo kama wetu kuomba kwa thati na kutunza ushuhuda wa mtu binafsi na wa kanisa la mungu.
3.8 tunatoa tahadhari kwa kila muumini wa KKKT kuwa makini sana katika kupambanua na kuyakata mafundisho mageni ambayo yanaweza kupotosha kwa urahisi waumini katika ulimwengu huu wa utandawazi.
3.9 Katika hali halisi ya ushilikiano kati yetu na makanisa mengine ya Ulaya na Marekani, Nahali pengine, msimamo wa kanisa hili umewekwa bayana katika majibu ya hojaji iliyoandaliwa na fungamano la makanisa yo kilutheri duniani (FMKD)kuhusu ubadilishanaji wa watumishi. Kwakuwa lengo la hojaji hiyo na maamuzi yatakayo fanywa hatimaye na FMKD kutokana na majibu yaliyotolewa na makanisa mengine wanachama yanayotuhusu sisi pia;
3.9.1 Sisi KKKT kama wanachama tunasema kwamaba kanisa letu halitakuwa tayali kufanya mabadilishano ya watu wanayojumuisha wale walio katika ndoa za jinsia moja au wale wanao shabikia ndoa za jinsia hiyo na uhalalishwaji wake. kwa maneno ya wazi zaidi, ni kwamba walio katika ndoa za jinsia moja, na wanaoshabikia ndoa za jinsia hiyo na uhalalishwaji wake, hawakalibishwi katika kufanya kazi katika KKKT. KKKT haitakuwa tayari kuhusu suala hili hata kwa ushawishi na ua shinikizo la nguvu ya fedha.
3.9.2 Hata katika ushilikiano wake na wengine kwa njia ya vyombo vya ushilikiano kama vile LWF, WCC, LMC na/au mashirika mengine (ya kidini na yasiyo yakidini) n.k., KKKT haitaunga mkono mbinu zozote za kujaribu kupiga debe na kuwapenyeza katika mashirika hayo watu walio katika ndoa za jinsia moja au washabiki wa nda za jinsia moja, na aina zote za vitendo vya ushoga.
3.10 KKKT haiwezi kuwalazimisha watu wa Ulaya au Marekani, waone na kufanya kama sisi katika swala hili la ndoa za jinsia moja, lakini inaweza kuwaeleza msimamo wake kinaganaga kuhusu swala lenyewe. Inaamini kuwa upande mwingine pia utajali na kuheshimu msimamo wake kama unavyo elezwa katika tamko hili. Aidha KKKT inategemea kuwa marafiki zake, popote pale walipo, ambao, lakini, inatofautiana nao sana sasa katika suala hili la ndoa za watu wa jinsia moja, hawajaribu- na ingeomba wasijaribu- kwa namna yoyote ile, wakati wowote ule, mahali popote pale, kuujaribu msimamo wake dhidi ya ndoa za watu wa jinsia moja,ikiwa ni pamoja na vitendo vya namna zote za kishoga.
Maaskofu wa KKKT
1.    Askofu Dk. Alex malasusa Mkuu, KKKT
2.    Askofu Michael Adam, KKKT Dayosisi Mkoani Mara
3.    Askofu Paulo 1. Akyoo, KKKT Dayosisi ya Meru
4.    Askofu Dk. Benson K. Bagonza KKKT Dayosisi ya Karagwe
5.    Askofu Elisa Buberwa, KKKT Dayosisi ya kaskazini Magharibi
6.    Askofu Zebedayo Daudi, KKKT Dayosisi ya Mbulu
7.    Asikofu Andrew P. Gulle, KKKT Dayosisi Mashariki Ziwa Victoria
8.    Askofu Thomas Laiser, KKKT Dayosisi ya kaskazini kati
9.    Askofu Cleopa A. Lukilo, KKKT Dayosisi ya kusini
10.Askofu Jobu A. Mbwilo, KKKT Dayosisi ya Kusini Magharibi
11.Askofu Dk. Owdenburg M. Mdegella, KKKT Dayosisi ya Iringa
12.Askofu Renard K. Mtenji, KKKT Dayosisi ya Ulanga Kilombero
13.Askofu Dk Stephen I. Munga KKKT Dayosisi kaskazini mashariki
14.Askofu Dk Hance Mwakabana Dayosisi ya kusini kati
15.Askofu Dk Israel-Peter Mwakyolile, KKKT Dayosisi ya Konde
16.Askofu Festo Ngowa, KKKT Dayosisi ya Dodoma
17.Askofu Jacob mameo Ole Paulo, KKKT Dayosisi ya Morogoro
18.Askofu Dk Martin F. Shayo, KKKT Dayosisi ya Kaskazini
19.Askofu Eliuphoo Y. Sima, KKKT Dayosisi ya Kati
20.Msaidizi wa Asikofu Mch. Eliraha M. Mmwari KKKT Dayosisi ya pare
DODOMA
7 Januari 2010