Pages

Ads 468x60px

Wednesday, February 27, 2013

PAPA BENEDICTOR AAGA RASMI ATOA HOYUDA YA MWISHO





Na  VATICAN City, Vatican 
 YAMETIMIA. Safari ya miaka saba ya Baba Mtakatifu Benedict XVI inakamilika leo pale atakapong’atuka rasmi katika uongozi wa Kanisa Katoliki, ifikapo saa 2:00 usiku kwa saa za Italia (saa 4:00 usiku kwa saa za Tanzania).
Kwa siku mbili, Papa amekuwa na shughuli nyingi katika makao yake, Gandolfo Castel, Vatican akijiandaa kimwili kuondoka, akiweka sawa nyaraka zake binafsi na zile za kanisa ambazo zitawekwa katika kumbukumbu.


Kwa upande mwingine Vatican, nchi ambayo ipo ndani ya Jiji la Rome iliyozungukwa na ukuta, ikiwa na ukubwa wa hekta 44 na wakazi 832 pekee, imekuwa katika hekaheka nyingi.
Jana, waumini zaidi ya 50,000 na wengine wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani wakiwamo makardinali, maaskofu, mapadri na walei walialikwa kwa shughuli rasmi ya kumuaga kiongozi huyo.

Tofauti na kanuni yake, leo Benedict hatavaa viatu vyekundu kama ilivyozoeleka na badala yake amechagua viatu rahisi vya ngozi vilivyobuniwa Mexico. Alipewa viatu hivyo ikiwa ni zawadi wakati wa ziara nchini humo 2012.

Tangu alipotangaza uamuzi wake wa kung’atuka Februari 11, mwaka huu, utata umegubika nafasi yake katika maisha mapya ndani ya Vatican, akiitwa Papa Mstaafu.

Waumini, wataalamu na hata viongozi mbalimbali wa Kikatoliki wameanza kuhoji ni jinsi gani viongozi wawili (Papa) wataishi, huku wote wakivaa mavazi meupe wakiitwa Papa, wakiishi umbali mdogo kati yao, wakiwa na wasaidizi wengi wanaowahudumia.

Vatican
Nje ya Gandolfo Castel, ulinzi umeimarishwa na vibali vya kuingia Vatican vimesitishwa.
Juzi, Vatican ilitangaza kwamba Papa Benedict XVI atajulikana kama ‘Emeritus Pope’, yaani Papa Mstaafu mwenye cheo cha heshima, akiendelea kuitwa, ‘mtakatifu’ na ambaye ataendelea kuvaa nguo nyeupe.

Mavazi na hata jina lake jipya ni masuala ambayo yamezua uvumi mwingi, huku suala la mrithi wake mpya pia likiwa gumzo, kwani tukio kama hilo lilitokea miaka 600 iliyopita.
Ni uamuzi uliolishtua kanisa hilo lenye waumini 1.2 bilioni duniani na wengi wanasema awali, haikushauriwa Papa kustaafu kwani kwa kufanya hivyo kunaacha mizozo na minong’ono ya kuwania madaraka.

Hata hivyo, uongozi wa Vatican umesisitiza kuwa uamuzi huo wa Papa Benedict XVI ni wa kipekee na hakuna mzozo ambao utatokea baina yake na mrithi wake ambaye mchakato wa kumpata unatarajiwa kuanza ndani ya wiki mbili zijazo.

“Kulingana na mabadiliko katika kanisa letu, kuna Papa mmoja. Ni dhahiri kwamba katika hali ya sasa hakutakuwa na tatizo,” anasema Mhariri wa Gazeti la L’Oservatore Romano linalomilikiwa na Vatican, Giovanni Maria Vian.

Hofu iliyopo
Hata hivyo, wakosoaji wa mambo hawakubaliani na hoja hiyo na baadhi ya makardinali walioko Vatican kwa usiri mwingi, wanazungumzia suala hilo wakieleza kwamba litazua tatizo kubwa kwa Papa ajaye, hasa ikiwa mtangulizi wake, Benedict akiwa bado hai.

Mtaalamu wa tauhidi (theolojia), raia wa Uswisi, Hans Kueng ambaye amekuwa mtu wa karibu wa Papa Benedict XVI, ingawa kwa sasa ni mkosoaji wake amesema:
“Kwa sasa, Benedict XVI akiwa bado hai, kuna hatari ya kuwa na Papa kivuli, mwenye mamlaka kamili ambaye kwa chinichini anaweza kumshinikiza mrithi wake kufikia uamuzi.”
Hans Kueng alisema hayo alipozungumza na Gazeti la Der Spiegel la Ujerumani.

Msemaji wa Vatican, Padri Federico Lombardi alisema Papa Benedict XVI kwa upande wake aliamua aitwe Papa Mstaafu au ‘kiongozi mstaafu wa Roma.’ Anasema haelewi ni kwa nini ameamua kuacha jina lake la sasa la Askofu wa Rome.

Kwa wiki mbili zilizopita, maofisa mbalimbali wa Vatican wamekuwa wakifikiri kwamba Papa angeanza kuvaa mavazi meusi na kutumia jina la Askofu Mstaafu wa Rome ili kuepuka mkanganyiko na mrithi wake.
Mwingine ambaye amekuwa akizusha mkanganyiko ni Katibu wa Papa, Askofu Mkuu, George Gaenswein ambaye ataendelea kuwatumikia Papa wote wawili, yaani Benedict XVI kwenye Monasteri ndani ya Vatican na kazi yake ya kawaida ya kuwa kiranja katika nyumba ya Papa mpya.

Kwa upande wake, Papa Benedict XVI anasema anastaafu na sasa ataishi maisha ya sala na tafakuri ya kina, mbali na majukumu mengine ya kidunia.
Hata hivyo, bado atakuwapo kwenye nchi ndogo ya Vatican, mahali ambako makazi yake yatakuwa jirani na mnara wa kurushia matangazo wa Kituo cha Redio cha Vatican, akiliangalia vizuri Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Kwa upande wake, Kueng anasema ni kosa kwa Askofu Gaenswein kuwatumikia Papa wawili kwa wakati mmoja na pia Benedict XVI kubakia jirani na mahali hapo.
“Hakuna padri ambaye anapenda mtangulizi wake kuishi karibu naye na kufuatilia anayoyafanya.

Hata kama Askofu wa Rome, haipendezi kutenda kazi huku mtangulizi wako akiona na kufuatilia.”
Mbali na mitazamo hiyo, wengine wamedhani kuwa uamuzi wa Papa Benedict XVI unalenga kudumisha utamaduni wa watangulizi wake.

“Ninashangazwa kuona Papa Benedict XVI akiendelea kuitwa mbarikiwa na kuvaa nguo nyeupe,” anasema Padri James Martin, Mtawa wa Jesuit pia mwandishi na mhariri, lakini baadaye anajirudi na kusema:
“Lakini sioni ajabu, mbona marais wastaafu wa Marekani, bado wanaitwa Rais? ni alama ya heshima kwake.”

Katika mkanganyiko huo, wapo wanaoamini kwamba yanayotokea yanatokana na nguvu ya roho mtakatifu, huku wengine wakipiga upatu kwamba ni zamu ya Afrika kutoa Papa na wanatajwa Makardinali Peter Turkson wa Ghana na Francis Arinze wa Nigeria.

WAANDISHI WA HABARI MKOANI MBEYA WAPATA SEMINA KUCHAMBUA SABABU ZINAZO SABABISHA WANAUME KUTOSHIRIKI HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI

MRATIBU WA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO MKOANI MBEYA PRISCA BUTUYUYU AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI

MWANAHABARI  GABRIEL MBWILE AKIWASILISHA MOJA YA MADA ZILIZOKUWA ZIKIENDELEA

WANAHABARI WAKIWA KATIKA CHUMA CHA SEMINA KATIKA HOSPITALI YA MKOA JIJINI MBEYA

Tuesday, February 26, 2013

SAFARI YA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MTWARA


WAAMNDISHI WA HABARI KUTOKA MIKOA MBALIMBALI NCHINI TANZANIA WAKIWA KATIKA OFISI ZA MAKAO MAKUU YA NIHF JIJINI DAR ES SALAM WAKISUBIRI USAFIRI WA KUELEKEA MKOANI MTWARA





WAANDISHI WA HABARI WAKIWA KATIKA BASI TAYARI KWA SAFARI YA KUELEKEA MJINI MTWARA

SAFARI ILIPOFIKA MKOA WA PWANI ILIINGIA KASORO KIDOGO MARA BAADA BASI HILO KUPASUA MPIRA WA UPEPO WA BREK LILIPOSHUGHULIKIWA SAFARI IKAENDELEA




HALI YA SAFARI ILIENDELEA KUANDAMWA NA BALAA LA KUPASUA HUO MPIRA ILIPOFIKA MJI WA KIBITI HALI HIYO ILIJITOKEZA TANA FUNDI AKIEENDELEA KUPAMBANA ILI KUFANIKISHA SAFARI HIYO



WAANDISHI WAKIWA KATIKA MAKUNDI WAKIBADILISHANA MWAZO WAKISUBIBIRIA KUTENGENEZWA KWA GARI KISHA KUENDELEA NA SAFARI

KWA BAHATI NZURI WAANDISHI WALIKUTANA NA KINYOZI TANGU MWAKA 1975 MWANDISHI WA BLOG HII ALIPATA NAFASI YA KUNYOA NYWELE ZAKE
UNAPOFANYA SAFARI YA KUELEKEA MTWARA USIPOZUNGUMZIA DARAJA LA MKAPA UTAKUA HAUJAFIKA SAFARI YA KUELEKEA HUKO



PAMOJA NA ADHA ZOTE ZA SAFARI HATIMAYE WAANDISHI WANAWASILI KATIKA OFISI ZA NIHF MTWARA


 WAGENI MBALIMBALI WAKIWA KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA CHUO CHA UALIMU MTWARA WAKISUBIRI KUAANZA KONGAMANO
MKURUGENZI WA NIHF AKIWAKARIBISHA WAGENI WAALIKWA KATIKA KONGAMANO HILO
 MWENYEKITI WA WAKUU WA MIKOA NCHINI ABASS KANDORO AKISHUKURU KWA MWALIKO HUO KWA NIABA YA WAALIKWA WOTE

MKUU WA MKOA WA MTWARA AKIMKARIBISHA MGENI RASMI KUFUNGUA KONGAMANO LA NANE LA NIHF

MGENI RASMI NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA AFYA AKIFUNGU KONGAMANO





WAANDISHI NA WADAU MBLIMBLI WAKITOA NA KUCHANGIA TAFITI ZILIZOFANYWA NA NIHF






             BAADHI YA WAANDISHI WAKIENDELEA KUSIKILIZA TAFITI MBALIMBALI
MWANDHISHI WA BLOG HII CHARLES ABRAHAM KULIA AKIWA NA MASUD KIPANYA MARA BAAYA YA MAPUMZIKO

MWANYEKITI WA WAKUU WA MIKOA NCHINI ABASI KANDRO MKUU WA MKOA WA MBEYA AKIFUNGA KONGAMANO LA NANE AL NIHF MKOANI MTWARA

WAANDISHI WAPATA HABARI MBAYA KUWEPO KWA TETESI KUTEKWA NA WENYEJI WA MTWARA HIVYO WAAMUA KUONDOKA KWA KUTOROKA NA BABASI MADOGO ILIWASTMBULIWE KWA KUTUMIA YALE WALIYOKUJA NAYO






WAANDISHI WAPOKELEWA NA JESHI LA POLIS MAENEO YA MKOANI LINDI ILI KULINDA USALAMA WAO WAKIENDELEA KUSUBIRIA UASFIRI WAO WA MABASI MAKUBWA AMBAYO YALIKUJA TUPU NA KUWACHUKUA NA KURUDI JIJINI DAR ES SLAM