Pages

Ads 468x60px

Friday, March 29, 2013

WASIFU 360: IJUMAA KUU

INAPOFIKA saa tisa alasiri, siku kama ya leo, maarufu kama Ijumaa Kuu, katika nyumba za ibada za Kikristo, kimya hutanda, mishumaa huzimwa na kuashiria kuwa ni siku ya majonzi.

 http://www.topnews.in/usa/files/jesus-crucifixion-full.jpg
Ijumaa Kuu ni siku ambayo Wakristo duniani kote hukumbuka mateso aliyoyapata Yesu baada ya kusulubishwa msalabani yapata zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita. Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimeipa thamani siku hii kwa kuitangaza kuwa ya mapunziko.
Siku hii huadhimishwa kwa ibada inayoambatana na kusoma mistari ya Biblia inayoelezea undani wa matukio yaliyosababisha kusulubiwa kwa Yesu Kristo.
Hii ni siku ambayo inatajwa kuwa na maana kubwa katika imani ya Kikristo. Waumini wanaamini kwamba, kusulubiwa na kufa kwa Yesu, kumeleta ukombozi duniani kote. Ijumaa Kuu haithibitishwi tu na vitabu vya dini, bali hata machapisho ya kihistoria, yanathibitisha juu ya kusulubiwa na kufa kwa Yesu.
Huadhimishwa kwa ibada huku zikitawaliwa na mistari na nyimbo za maombolezo ya kufa kwa Yesu. Rangi za vitambaa vipambwavyo kanisani, huwa ni zile zinazoashiria maombolezo. Hufanyika tangu asubuhi na inapofika saa tisa, muda unaosadikiwa kuwa ndipo Yesu alikata roho, makanisa hutawaliwa na kimya kiambatanacho na kuzima mishumaa ndani ya kanisa. Katika muda huo wengi hutafakari namna walivyokombolewa kwa damu ya Yesu.
Makanisa mengi, vikundi mbalimbali kama vile watoto, vijana na wanawake, hutumia siku hiyo kuonesha maigizo ya kusulubiwa na kufa kwake. Majina yanayotumika katika mataifa mbalimbali, yote hushabihiana kwa kuonesha nafasi ya siku hii. Ingawa majina hayo huweza kutofautiana kulingana na lugha itumikayo katika eneo fulani, lakini yote hulenga kuzungumzia nafasi na umuhimu wa Ijumaa Kuu.
Katika lugha ya Kijerumani, siku hii hujulikana kwa jina la Karfreitag linalomaanisha kuwa ni Ijumaa ya Maombolezo. Waisrael wanaiita Big Friday wakimaanisha ni siku kubwa na maalumu. Nchi za Amerika ya Kilatini, Spain, France, Italia, Ufilipino na Ureno wanaiita Ijumaa Takatifu. ‘Sexta-Feira Santa’ ni neno la Kireno lenye kumaanisha Ijumaa Takatifu.
Katika nchi zenye Wakristo wengi, kama vile Ujerumani, Uingereza Canada na New Zealand, hii ni siku ya mapumziko. Nchi nyingi zinazozungumza Kingereza, maduka mengi mitaani hufungwa kwa ajili ya kuadhimisha siku hii. Nchini Canada, benki, ofisi za serikali na shughuli zote za watu binafsi hufungwa siku hiyo.
Katika Jamhuri ya Ireland, ambayo ni nchi ya Kikatoliki, pombe huzuiwa kuuzwa wakati wa Ijumaa Kuu. Karibu sehemu za starehe na migahawa mingi nchini humo hufungwa kwa siku nzima ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku hiyo kuu. Nchini Ujerumani, ni makosa kufanya maonesho na shughuli mbalimbali za starehe kama vile kucheza muziki siku ya Ijumaa Kuu.
Hatua hiyo ambayo huwagusa hata wasio Wakristo, katika mwongo uliopita, iliwahi kuzua upinzani. Nchini Afrika Kusini, Sheria inatamka kufunga ofisi zote za serikali, shule wakati wa Ijumaa Kuu. Baadhi ya maduka hufungwa pia. Kuuza au kununua pombe pia kunakatazwa. Hapa nchini pia siku hii imo katika orodha ya siku zinazotambulika kuwa ni za mapumziko.
Mafundisho yanasema kwamba sambamba na waumini kuhudhuria ibada, Ijumaa Kuu ni siku kuu ambayo haina budi kutumiwa na Wakristo kutubu dhambi. Ni siku inayowakumbusha upendo wa dhati aliouonesha Kristo. Haipaswi kuchukuliwa kuwa siku ya mapumziko marefu pekee bali na wao pia kutafakari namna wanavyoonesha upendo kwa wengine na kuzidisha kufanya mambo yanayompendeza Mungu.
Ziko tamaduni mbalimbali walizojiwekea Wakristo wengi wakati wa Siku ya Ijumaa Kuu. Miongoni mwake, ni ulaji au kutokula aina fulani ya vyakula na kufunga kula. Hata hivyo, Wakristo wengi hawasubiri kufunga wakati wa Kwaresma au Ijumaa Kuu pekee, bali hufanya hivyo siku zote.
Viongozi wa dini wanafundisha kwamba kujinyima ni jambo la msingi na hivyo inatakiwa iwe ni kujinyima kitu fulani lakini wakati huo huo hicho ulichojinyima kitumike kumsaidia mwenye shida. Licha ya baadhi ya watu kufunga siku ya Ijumaa Kuu wapo ambao wamejiwekea utaratibu wa kufunga kila Ijumaa wakati wengine hufunga siku 40 kabla ya Pasaka.
Suala la kufunga linaloambatana na kutenda yaliyo mema, halina muda wala kikomo. Ulaji wa mkate mdogo aina ya keki hususan kwa jamii za Waingereza, pia ni utamaduni mwingine uambatanao na maadhimisho ya Ijumaa Kuu. Vile vile nyama, ni chakula ambacho waumini wengi wa Kikristo huiepuka.
Wakati awali ilizoeleka kwamba waumini wa madhehebu ya Katoliki ndio wenye utamaduni huo, lakini uchunguzi unonesha kwamba wapo waumini katika madhehebu mengine wanaozingatia pia utamaduni huo. Baadhi ya Walutheri katika nchi za Sweden, Scandinavia, Ujerumani na hata hapa nchini pia wanazingatia utamaduni wa kutokula nyama wakati wa Ijumaa Kuu.
Baadhi ya viongozi wa dini husema kwamba suala la kutokula nyama Ijumaa Kuu siyo imani, bali ni utamaduni. Yaani huchukuliwa kama jukumu binafsi lisilomlazimisha mtu. Viongozi wa dini wamekuwa wakifundisha kwamba maadhimisho ya Pasaka yanapaswa kuambatana na tafakuri kuhusu njia bora za kuendeleza amani kwa mtu binafsi na hata nchi kwa ujumla.
Katika kipindi hiki ambacho nchi za Afrika zinakabiliwa na changamoto ya kuimarisha amani na upendo, kwa mfano, Pasaka inaweza kutumika katika kurejesha hali ya kuvumiliana ili kuepuka migogoro ya kisiasa na kijamii.

Tuesday, March 26, 2013

Cheti alichotumia Mulugo, cha Mhadhiri wa Mkwawa


  Mwananchi
  Imebainika kuwa mmoja wa watu ambao Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo (pichani)anadaiwa kutumia jina lake kutafuta kazi ya ualimu katika Shule ya Sekondari ya Southern mkoani Mbeya ni
Mhadhiri katika Chuo Kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa (Muce), kilichopo mkoani Iringa.Mhadhiri huyo ni Dick Aron Mulungu ambaye alisoma na Mulugo katika Shule ya Sekondari ya Songea Wavulana kati ya 1994 na 1996 na alijiunga na shule hiyo baada ya kuhitimu kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kafule, ambayo iko mkoani Mbeya.

Taarifa zinaonyesha kuwa Mulungu alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kupata Shahada ya kwanza katika Elimu (BA Education) 2001 na baadaye alisoma na kupata Shahada ya Uzamili (MA Development studies ) 2007.

Alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi, mahojiano yalikuwa hivi:
Mwandishi: Hallow…(mwandishi akajitambulisha)
Mulungu: Sawa, unasemaje?
Mwanishi: Nazungumza na Dick Mulungu?

Mulungu: Ndiyo mimi.
Mwandishi: Hivi unamfahamu mtu anayeitwa Hamimu Agustino?
Mulungu: Aah… hivi ulisema unaitwa nani?
Mwandishi: Si nimeshajitambulisha jina na ofisi ninayotoka?
Mulungu: Nipigie kesho naona hapa kuna kelele.

Mwandishi: Mbona nakusikia vizuri tu?
Mulungu: Nipigie baada ya nusu saa basi.
Baada ya nusu saa…….
Mwandishi: Haloo… naona nusu saa imekwisha, uko tayari kuzungumza?
Mulungu: Huyo simfahamu.
Mwandishi: Kwani wewe si ulisoma Songea Boys?

Mulungu: Ndiyo
Mwandishi: Kwa hiyo humkumbuki mtu aliyekuwa akitumia jina hilo?
Mulungu: Huyo mtu namkumbuka ndiyo.
Mwandishi: Kwa sasa yuko wapi?
Mulungu: Siwezi kujua, si unajua tumesoma siku nyingi sasa huwezi kujua mtu amekwenda wapi… ni siku nyingi mno.
Mwandishi: Ahsante.Chuo Kikuu na siasa
Taarifa zinaonyesha kuwa Waziri Mulugo alijiunga na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania 2002 akitumia majina ya Philipo Hamimu Augustino na alisomea Shahada ya Sanaa katika Elimu (BA. Ed). Namba yake ya usajili chuoni hapo ni 08652/T.02.
Alipokuwa akiendelea na kazi ya ualimu Mulugo alianza harakati za kisiasa na ndipo alipoamua kwenda kugombea ubunge katika majimbo ya wilaya ya Chunya.

Kada wa chama cha NCCR Mageuzi wilayani Chunya, Nyawili Kalenda aliyejitambulisha kama mlezi wa siasa wa Waziri huyo alisema walifahamiana naye 2004 wakati Mulugo na rafiki yake walipokwenda kumtaka ushauri wa kugombea ubunge katika jimbo la Songwe.
Katika nakala za wasifu wake zinaonyesha kuwa 2008 alishika nafasi ndani ya CCM ambazo ni pamoja na mjumbe wa baraza la jumuiya ya wazazi wilaya ya Chunya, Katibu wa Elimu, Uchumi, Malezi na mazingira wa jumuiya ya wilaya hiyo na mjumbe wa baraza la wazazi mkoa wa Mbeya.Kauli yake
Mulugo anasema madai hayo yamekuwa yakitolewa mara kwa mara na amekuwa akiyajibu kwa kuwaonyesha vyeti vyake halali vya shule. “Hayo madai ni ya muda mrefu, wewe sijui utakuwa mtu wa 20 kuuliza swali kama hilo. Mimi vyeti ninavyo na hata ukitaka ushahidi nitakuonyesha,” alisema Waziri Mulugo.

Licha ya kukiri kurudia darasa la saba, Waziri Mulugo alisema jina la Hamimu amekuwa akilitumia katika elimu tangu awali na kwamba hakuvunja sheria kufanya hivyo.

“Jina la Hamim ni la nyumbani Philipo ni jina langu la ubatizo, nadhani haya ni mambo ya kawaida na kweli nilipokuwa shule watu walikuwa wananifahamu kama Hamimu pia Philipo ni jina langu la ubatizo na kumbuka tukifika chuo huwa tunatumia jina la baba.

“Na pia ni kweli nilirudia shule kwa sababu wakati ule wa Mwalimu Nyerere na Mwinyi (Ali Hassan), sheria ilikuwa inaruhusu maana wanafunzi walikuwa wachache mno, fikiria katika darasa letu la saba tulimaliza watu saba tu. Baadaye sheria hiyo ilibadilishwa,” aliongeza.Kuhusu jina la Dick Mulungu, alikiri kumfahamu mtu huyo na kwamba walisoma wote shule ya Sekondari ya Songea Boys. Hata hivyo, alipinga kutumia vyeti vyake.

JAMBAZI SUGU LAUWAWA KWA KUPIGWA RISASI KWENYE HARAKATI ZA KUTEKA MAGARI MLIMA NYOKA JIJINI MBEYA


Mwili wa Jambazi sugu  Emanuel Blasius Mdendemi ukiwa umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Mbeya
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya  Diwani akiangalia mwili jambazi lililouwawa na kikosi cha polisi Mbeya
Baadhi ya polisi na waandishi wa habari wakiwa nje yajengo la kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa Mbeya
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika Mkutano alioufanya na waandishi wa Habari Ofisini kwake ambapo alisema tukio hilo lilitokea  jana majira ya Saa 10(kumi) Alfajiri usiku wa kuamkia Machi 26, Mwaka huu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani akionyesha baadhi ya siraha alizokutwanazo jamabazi huyo aliyeuwawa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani akionyesaha hirizi iliyofungwa katika bunduki aliyokuwa anatumia jambazi huyo kama kinga katika matukio yake 
Hii ndiyo hirizi iliyofungwa katika bunduki aliyokuwa anatumia jamabazi huyo jamani waganga wakienyeji acheni hizo kuwadanganya watu matokeo yake ni kuongeza uhalifu nchini hakika nao tutawashughulikia kwani wamekuwa chanzo cha uhalifu nchini hayo yamesemwa na kamanda Diwani

Kamanda Diwani akiongea na waandishi wa habari


MTU mmoja ambaye anasadikiwa kuwa ni jambazi ameuawa kwa kupigwa risasi na Askari wa Jeshi la Polisi akiwa kwenye harakati za kuteka magari katika Eneo la Mlima Nyoka Jijini Mbeya baada ya kutokea kwa majibizano ya kurushiana risasi.
  
Jambazi huyo ni miongoni mwa watu waliokuwa wakitafutwa na Jeshi la Polisi Mkoani hapa akituhumiwa kuhusika na mauaji ya Askari Polisi mwenye namba G 68 PC Jafari yaliyotokea  Februari 6, Mwaka huu  katika eneo la Matundasi Wilayani Chunya.
  
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika Mkutano alioufanya na waandishi wa Habari Ofisini kwake ambapo alisema tukio hilo lilitokea  jana majira ya Saa 10(kumi) Alfajiri usiku wa kuamkia Machi 26, Mwaka huu.
  
Kamanda Diwani alisema kabla ya tukio majambazi wapatao wanne  tayari walikuwa wameweka mawe barabarani kwa nia ya kuteka magari ili wafanye uporaji katika eneo hilo la Mlima Nyoka ambalo limekuwa na matukio kadhaa ya watu kuporwa mali zao.
  
Alisema Jeshi la polisi baada ya kupata habari za kutegwa mawe, askari walifika kwa wakati kwa kuwa polisi walikuwa jirani na eneo hilo na kuweka mtego kwa kuwa majambazi hawakuwa wameonekana kwa wakati ule.
  
Aliongeza kuwa baada ya muda majambazi walipoona taa za gari walijitokeza tayari kushambulia lakini kabla ya hapo polisi walitoa amri ya kujisalimisha kinyume chake wakaanza kupiga risasi ovyo ndipo mashambulizi ya polisi yakafanywa.
  
Diwani alisema katika mapambano hayo alijeruhiwa jambazi mmoja kwa risasi kiunoni na ubavuni kulia na wengine watatu walifanikiwa kutoroka ambapo Marehemu alipowahishwa hospitali kwa matibabu daktari alibaini kuwa amekwisha fariki.
  
Alisema  jambazi huyo alikutwa na silaha moja SMG yenye namba  AB huku namba  nyingine zikiwa zimefutwa na magazine yake ikiwa na risasi ishirini na mbili (22) pamoja na mapanga mawili([2).
  
Aliongeza kuwa baada ya  Marehemu kufanyiwa upekuzi maungoni mwake jambazi huyo alikutwa na kitambulisho cha mkazi chenye namba B.0010453 chenye jina la Emanuel Blasius Mdendemi aliyezaliwa mwaka 1984 eneo la Matamba wilayani Makete Mkoa wa Iringa makazi yake ni Uwemba Mkoani Njombe.
  
“Jambazi huyu amebainika kuwa ni miongoni mwa majambazi waliokuwa kwenye mtandao wa majambazi uliokamatwa hivi karibuni kuhusiana na matukio waliyofanya Mikoa mbalimbali ikiwemo Mbeya,Njombe na Iringa.aidha amebainika kushiriki katika tukio la mauaji ya askari polisi PC Jafari wa kituo cha Mkwajuni – Chunya tarehe 06.02.2013.” Alisema Kamanda Diwani.
  
Aliongeza kuwa  ufuatiliaji wa majambazi waliotoroka unaendelea kufanywa ambapo pia  anatoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za wahalifu hao azitoe bila kuchelewa kwa jeshi la polisi ili zifanyiwe kazi.

Pia  amewatahadhalisha majambazi na wahalifu wa makosa yeyote kuachana na uhalifu kwa kuwa ni biashara isiyo na faida badala yake wafanye shughuli halali kupata maendeleo ambazo fursa zake ni nyingi.

Picha na Mbeya yetu 

Saturday, March 23, 2013

LWAKATARE AFIKISHWA MAHAKAMANI CHINI YA ULINZI MKALI WA POLISI



 Mkurugenzi wa Usalama na Ulinzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare akionesha ishara ya vidole ambayo ni salamu kwa wafuasi wa chama chake wakati akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Habari Mseto Blog)
 Askari wa mbwa wakiimarisha ulinzi wakati wa kesi hiyo.

Askari wa mbwa wakiimarisha ulinzi wakati wa kesi hiyo.
  Mkurugenzi wa Usalama na Ulinzi wa Chadema, Wilfred Lwakatare akiwa na mtuhumiwa mwenzake, Ludovick Joseph wakiingia mahakamani leo.
 Mkurugenzi wa Usalama na Ulinzi wa Chadema, Wilfred Lwakatare akiwa na mtuhumiwa mwenzake, Ludovick Joseph wakiingia mahakamani leo.

 Polisi wakisindikiza msafara wa gari lililompakia Mkurugenzi wa Usalama na Ulinzi wa Chadema, Wilfred Lwakatare kuelekea mahabusu hadi April 3 mwaka huu.
 Mkurugenzi wa Usalama na Ulinzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare akionesha ishara ya vidole ambayo ni salamu kwa wafuasi wa chama chake wakati akiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiteta jambo na mke wa Mkurugenzi wa Usalama na Ulinzi wa Chama hicho, Wilfred Lwakatare.
Jengo la Mahakama ya Kisutu.
Wafuasi wa Chadema wakiwa  wamekusanyika nje ya mahakama hiyo

Wednesday, March 20, 2013

Picha ya Marehemu enzi za uhai wake.

GLOBAL NEWS: PAPA FRANCIS ATAWAZWA



Baba Mtakatifu Francis, leo ametawazwa rasmi kuliongoza Kanisa Katoliki duniani katika Ibada ya Misa inayofanyika kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. 
 http://static.guim.co.uk/sys-images/Guardian/Pix/pictures/2013/3/19/1363679536671/Pope-Francis-drives-throu-010.jpg
Katika Ibada hiyo, Baba Mtakatifu Francis amevalishwa pete ikiashiria sasa amekuwa Baba Mtakatifu wa 266. Ibada hiyo inahudhuriwa na waumini wengi, tangu Mei, mwaka 2011 ambapo zaidi ya watu milioni 1.5 walifika Vatican kuhudhuria sherehe za kutangazwa mwenye heri, Papa Yohana Paulo wa Pili . Viongozi 130 kutoka duniani kote, wanahudhuria Ibada hiyo, akiwemo Makamu wa Rais wa Marekani, Joe Biden na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe.

WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI FOREST MBEYA WAANDAMANA KUTOKUWA NA IMANI NA MKUU WAO WA SHULE


Wanausalama wakifika katika shule ya sekondari Forest kutuliza maandamano yao
Wanafunzi sasa wametulia kumsikiliza Afisaelimu mkoa wa Mbeya aliyefika shuleni hapo kusikiliza kero zao
Ofisa Elimu wa Mkoa wa Mbeya Juma Kaponda akiwasisitizia wanafunzi hao kuwa waache tabia ya kuandamana wajuwe kuwa wamekuja kusoma siyo kuandamana
Moja ya wanafunzi akimweleza kero yao afisa elimu mkoa Mbeya
Mkuu wa Shule  Cesilia Kakera akiwa amejishika kichwa baada ya wanafunzi kutokuwa naimaninae kwa kushirikiana na walimu wanaotuhumiwa kupokea rushwa shuleni hapo
Ofisa Elimu wa Mkoa wa Mbeya Juma Kaponda amesema suala la walimu hao kukamatwa na kufikishwa Takukuru ni suala la ngazi nyingine hivyo hawatakiwi kulizungumzia. 




Hii ndiyo ofisi inayotumika kuwatesa wanafunzi ofisi hii huitwa guantanamo bay camp

IKIWA zimepita siku chache tangu Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mbeya kuwakamata Walimu wawili wa Shule ya Sekondari ya Forest wakituhumiwa kupokea rushwa sakata hilo limechukua sura mpya baada ya wanafunzi wa shule hiyo kuandamana.
Maandamano ya wanafunzi hao yametokana na Walimu hao kuwa nje ya dhamana na kuendelea kufundisha katika shule hiyo jambo ambalo wanafunzi hao wamelipinga na kusababisha maandamano yaliyozuiliwa na jeshi la polisi walipokuwa wakitaka kuelekea kwenye Ofisi za Ofisa Elimu wa Mkoa.
Kutokana na hali hiyo Ofisa Elimu wa Mkoa wa Mbeya Juma Kaponda amelazimika kufika Shuleni hapo kisha kuzungumza na wanafunzi ambao walimtajia sababu zaidi ya kumi zilizosababisha kufanya maandamano hayo.
  
Wamezitaja sababu hizo kuwa ni pamoja na sakata la walimu waliokamatwa kwa rushwa kuachiwa na kuendelea kufundisha, Walimu kutofundisha, Vitisho vya walimu kwa wanafunzi, Wazazi kutukanwa na walimu, Kutokuwa na imani na Mkuu wa Shule pamoja na ujirani wa walimu watuhumiwa na mkuu wa Shule.
Wamezitaja sababu zingine kuwa ni Mkuu wa shule kutumia matofali ya shule kujengea madarasa badala ya wigo,kutokuwa na vifaa vya michezo pamoja na kutotolewa kwa vibali vya kwenda kucheza na shule jirani.
Wameongeza kuwa Shule haifanyi mikutano ya wanafunzi( baraza la shule la wanafunzi), kutokuwa na vitambulisho vya wanafunzi, michango ya wigo, michango ya wigo wa shule na michango ya masomo ya jioni.
  
Akijibu tuhuma hizo Ofisa Elimu wa Mkoa wa Mbeya Juma Kaponda amesema suala la walimu hao kukamatwa na kufikishwa Takukuru ni suala la ngazi nyingine hivyo hawatakiwi kulizungumzia.
  
Kuhusu madai ya walimu kutofundisha Kaponda amesema si sababu ya kweli kutokana na wanafunzi hao kuwa kwenye mitihani ya kufungia mhura hivyo walimu hawawezi kuingia madarasani kufundisha.
  
Pia amewaagiza walimu hao kuwa na ushirikiano na wanafunzi na kutotoa lugha za vitisho kwa wanafunzi ambapo pia aliwaagiza wanafunzi kuwa watulivu na kuwasikiliza walimu wao.
  
Aidha amewaagiza walimu haokutoitisha mikutano ya wazazi pasipo kuwepo kwa bodi ya shule ambapo ameagiza kuwa kila mkutano wa wazazi utaklapofanyika ni vema mwenyekitiwa bodi ( ya shule akaongoza mikutano hiyo.
  
Kuhusu suala la vibali vya michezo, mikutano ya baraza la wanafunzi na vitambulisho Ofisa huyo aliagiza Mkuu wa Shule  hiyo Cesilia Kakera kulishughulikia mara moja na kumpelekea taarifa ofisini kwake mara moja.
Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Mbeya Daniel Mtuka alipoulizwa suala la walimu hao kuendelea na kazi ili hali walikuwa wamekamatwa kwa tuhuma za rushwa Kamanda huyo alisema wameachiwa kwa dhamana.
  
Mtuka amesema baada ya watuhumiwa hao ambao walikamatwa Machi 4, Mwaka huu bado wanashikiliwa na kikosi chake ingawa wako nje kwa dhamana na kuongeza kuwa uchunguzi wa kesi hiyo bado haujakamilika hivyo hawawezi kuwazuia kuendelea na kazi.
  
Amesema baada ya kukamilika uchunguzi ndipo itakapojulikana ni hatua ipi itakayofaa kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa kama watakuwa wamebainika kuhusika na sakata hilo.
Walimu hao walikamatwa kwa tuhuma za kushawishi na kupokea rushwa ya kati ya shilingi 500 na 1,000 kutoka kwa wanafunzi wanaochelewa kufika shuleni asubuhi kila siku.
  
Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Mbeya Daniel Mtuka, alisema walimu hao walikamatwa baada ya kupokea taarifa kutoka kwa baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo baada ya kuchoshwa na tabia hiyo.
  
Mtuka amewataja walimu hao kuwa ni Solomoni Mwasote na Faustin Robert ambao walikamatwa shuleni hapo wakiwa wanaendelea na zoezi hilo la kuwalipisha wanafunzi fedha.
HABARI NA J. MWAISANGO

Tuesday, March 19, 2013

Trafiki wa kike aliyejulikana kwa jina moja la Elikiza aliyekuwa akiongoza magari eneo la Bamaga, Mwenge jijini Dar, akifunikwa na wasamaria wema baada ya kugongwa na gari na inadhaniwa kuwa amekufa papo hapo.

Trafiki Elikiza baada ya kugongwa na gari eneo la Bamaga muda huu.

Baadhi ya wananchi waliofika eneo la tukio.

Hali ilivyokuwa eneo la tukio baada ya ajali hiyo.

Trafiki mmoja ambaye amefahamika kwa jina moja la Elikiza, muda huu amegongwa na gari aina ya VX ambayo haikujulikana namba na inadhaniwa kuwa amekufa papo hapo wakati akiongoza magari eneo la mataa ya Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam. Taarifa zilizopatikana eneo la tukio zinadai kuwa Trafiki huyo alikuwa akiongoza msafara na baada ya msafara huo, aliruhusu magari mengine yaendelee na safari ndipo ghafla gari lilipotoka upande wa pili na kumgonga.

(Picha na Shauri Kati / GPL)

Thursday, March 14, 2013

MITUME WALIOPO NCHINI KWA MASLAHI YAO BINAFSI HAO HAWAJATUMWA NA MUNGU, NI MATAPELI NA HULIPELEKA TAIFA KUPOTEZA AMANI







MKURUGENZI WA JEM MINISTRY JEREMIA MWAKANYILENGE AKIONGE NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE
WAANDISHI WA HABARI WAKIWA OFISI YA JEM MINISTRY WAKIONGEA NA MKURUGENZI JEREMIA MWAKANYILENGE

-->
KWAKUA MITUME WA KWELI YEYE NI MUHUDUMU WA JAMII NA MUNGU HUYAFANYA MAMBO MAGUMU KUWA MEPESI

Hayo yasememwa na mtume JEREMIA MWAKANYILENGE wa huduma ya Jem ministry ya jijini mbeya alipokuwa akiitambulisha huduma hiyo kwa waandishi wa habari ofisini kwake.

Mwakanyilenge amewataka waumini kuwa makini sana na huduma hizi zilizoshamili kuibuka kila siku kutokana na kuwepo na baadhi ya watumishi matapeli wanaotumia jina la kristo kujinufaisha wenyewe binafsi

“Ukiona mtume huduma yake inaleta uchochezi katika taifa hili ujue huyo si wa mungu atakuwa amejituma mwenyewe na ni tapeli, kwani aliyetumwa na mungu kweli huyafanya yaliyo magumu kwa watu kuwa mepesi” amesema mwakanyilenge.

Katika kikao hicho pia alipata nafasi ya kuitambulisha rasmi hudu yake ya JEM MINISTRY kua si kanisa jipya bali ni tasisi ya kuihudumia jamii kwa kuwapatia ajira katika idara zake za biashara kama vile JP PRODUCTION studio inayofanya kazi za kurekodi audio cd pamoja na video, lakini pia imeanzisha mfuko wa kustaafu wachungaji.

JP PRODUCTION imetoa ajira kwa wachungaji na vijana mbalimbali wenye kipaji cha uimbaji kwa kujikimu na maisha yao kama wengine, Lakini pia imekuwa ikisambaza kazi za waimbaji kwa kuwapa faida kubwa kuliko wasamabazaji wengine.

Kwa hivi sasa JEM MINISTY pamoja na JP PRODUCTION imeto kazi mpya ambayo ipo sokoni yenye nyimbo nane zilizoimbwa live na mtumishi wa mungu JEREMIA MWAKANYILENGE kwa kushirikiana na mwaimbaji wa kimataifa EFRAIM SEKELETI toka nchini zambia.