Pages

Ads 468x60px

Sunday, April 28, 2013

ALIYEZIKWA AKIWA HAI AFUKULIWA NA KUKUTWA AMEKUFA CHUNYA MBEYA


VIJANA WAKICHIMBUA KABURI ALIMOZIKWA ALIYEKUWA HAI 
KWANZA KABISA WANAANZA TOA JENEZA LA ALIEKUFA KWA UGONJWA NA KUZANIWA AMEROGWA NA ALIYEZIKWA AKIWA HAI MAANA KATIKA KABURI HILO WALIZIWA WATU WAWILI KATIKA KABURI MOJA  ALIE HAI NA MFU
JENEZA LA ALIEKUFA KWA UGONJWA TAYARI LIMETOLEWA HILO PEMBENI SASA ANAFUKULIWAALIEZIKWA HAI
MWILI WA ALIEZIKWA AKIWA HAI SASA UNATOLEWA KABURINI
HII MITI NDIYO ILIYOTENGANISHA JENEZA NA ALIEZIKWA AKIWA HAI KWANZA ALIANZA ALIE HAI KUZIKWA IKAFUATIA MITI HIYO NDIYO LIKAFUATA JENEZA LA ALIEKUFA KWA UGONJWA
MWILI WA ALIEZIKWA AKIWA HAI BAADA YA KUTOLEWA KABURINI
MDOGO WA MAREHEMU ALIEZIKWA AKIWA HAI
MWILI WA ALIEKUFA KWA UGONJWA ULIZIKWA TENA NA WANAUSALAMA KUONDOKA NA MWILI ALIEZIKWA AKIWA HAI
WANANCHI HAO HAIKUTOSHA BAADA YA KUMZIKA MWENZAO AKIWA HAI WALIKWENDA KUCHOMA NYUMBA YAKE
NA KUHARIBU MAZAO YAKE SHAMBANI





KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida wananchi wa kijiji na kata ya Mkwajuni Wilaya ya Chunya Mkoani hapa wamemzika Mwanakijiji mwenzao akiwa hai wakimtuhumu kusababisha kifo cha Mkazi mmoja kijijini hapo.
  
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Apri 26 mwaka huu  majira ya Saa Nane Mchana katika Kitongoji cha Maweni Makaburini baada ya Mhanga aliyefahamika kwa jina la Victory Mwachirui(68) kuhudhuria mazishi ya Pita Barton(28)aliyefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, Thobias Ismail amesema marehemu alipatwa na umauti akiwa anapatiwa matibabu kwa mganga wa jadi ambaye jina lake halikuweza kujulikana maramoja.
Amesema wakati taratibu za mazishi zikiendelea Ndugu wa marehemu walidai kuwa kifo cha Marehemu kilisababishwa na Mwachirui ambaye ni Katekista mstaafu kwa imani za kishirikina.
Ameongeza kuwa wakati kaburi likichimbwa kwa ajili ya kumzika  marehemu ndipo vijana waliokuwa wakichimba waliagiza Wazee wa Mila wafike makaburini kwa ajili ya kuangalia utaratibu wa mazishi na kukagua ukubwa wa Kaburi ambalo lilikuwa limekwisha chimbwa.
  
Kutokana na mwito huo walifika wazee wanne akiwemo Mzee Mwachirui ambaye walimsisitiza kusogea jirani na kaburi ambapo baada ya kusogea alipigwa na Sururu kichwani na kuangukia kaburini huku akisindikizwa na marungu.
  
Baada ya Mzee huyo  kupoteza fahamu Vijana hao walianza kutandika fito ndani ya kaburi kisha kufukia kwa udongo kiasi kwa lengo la kutenganisha na Mwili wa Marehemu Pita uliokuwa kwenye jeneza baada ya kuwazika kwenye kaburi moja.
  
Baada ya kukamilika kwa zoezi la mazishi kundi la vijana lilielekea hadi nyumbani kwa Mzee aliyezikwa akiwa hai na kuiteketeza nyumba yake huku wakiapa kutotoa siri wakidai Siri ya Jeshi.
  
Hata hivyo baadhi ya wananchi walitoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho aliyefahamika kwa jina la Credo Kayanza ambaye pia alitoa taarifa kwa Diwani wa Kata hiyo Chesco Ngairo ambao kwa pamoja walitoa taarifa Jeshi la Polisi ambao baada ya taarifa hiyo walifika eneo la tukio huku wakidhani lililotokea ni kuchomwa kwa nyumba pekee.
  
Jeshi la Polisi baada ya kufanya upelelezi na kubaini kitendo hicho waliwaamuru baadhi ya Vijana kufukua kaburi hilo zoezi ambalo lilifanyika baada ya Vijana hao kulipwa.
  
Baada ya kufukuliwa kwa kaburi hilo Mwili wa Marehemu Mzee Mwachirui ulichukuliwa na kupelekwa katika Hospitali ya Misheni ya Mkwajuni kwa ajili ya Uchunguzi huku Mwili wa Pita ukizikwa upya palepale.
  
Baada ya kukamilika kwa uchunguzi mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi ambapo Marehemu alizikwa katika eneo tofauti na alipokuwa amefukiwa awali.
  
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo pia ametoa wito na kuwaasa  wananchi na jamii kuacha tabia  ya kuamini mambo ya ushirikina na uchawi kwa madai kuwa hauna faida kwao bali huchochea migogoro katika jamii zao.
Aidha ameongeza kuwa wakumbuke kitendo cha kujichukulia sheria mkononi ni kosa kisheria ambapo pia  amewaomba wenye taarifa za walipo waliohusika na mauaji hayo kuzifikisha polisi haraka ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao ingawa hakuna aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo.

Picha na E. Kamanga wa Mbeya yetu

MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI


 Marais wa jumuiya ya Afrika Mashariki wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka laiyekuwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Uganda Marehemu Eriya Kategaya wakati wa ufunguzi wa kikao cha kumi na moja cha Jumuiya hiyo jijini Arusha leo mchan. Katika Hoteli ya Ngurdoto.Kutoka kushoto Rais Wa Burundu Pierre Nkurunzinza,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya wakati wa ufunguzi wa kikao cha juu cha kumi na moja cha Wakuu wa nchi wa jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofaniyka jijini Arusha.
 Marais  Wa jumuiya ya Afrika Mashariki waliohudhuria Mkutano wa Wakuu wa jumuiya hiyo katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo.Kutoka kushoto ni Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi,Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda,Mwenyeji wa mkutano Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Mpya wa Kenya,Uhuru Kenyatta(picha na Freddy Maro)
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Mkewe Margareth Kenyatta wakifurahia ngoma za utamaduni muda mfupi bbada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika jijijini Arusha(picha na Freddy Maro)

Rais .Jakaya Kikwete akimkaribisha Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alipowasili juzi jioni kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuia ya Afrika ya Mashariki unaofanyika jijini Arusha. (PICHA NA FREDDY MARO)

Wednesday, April 24, 2013

Uelewa mdogo wa wananchi nchini Tanzania kuhusu afya ya uzazi na mtoto umepelekea kuendelea kuzorota kwa idadi ya wanaume wanaohudhuria huduma ya kliniki kutokana ushirikiano hafifu uliopo katika jamii.

mmutta@fhi360.org -->

Hayo yamebainishwa na ofisi ya mganga mkuu mkoa wa mbeya kitengo cha huduma za afya ya uzazi na mtoto kwa kushirikiana na shirika la UJERUMANI (GIZ).

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake mratibu wa huduma hiyo PRISCA BUTUYUYU amesema kumekua na upungufu mkubwa kwa baadhi ya wanaume kutoshiriki katika huduma za afya ya uzazi.

“Katika tafiti zilizofanywa kwa wilaya nane za mkoa wa mbeya tangu mwaka 2009 hadi 2011  zimeonyesha idadi za wanawake wanaokwenda klinic wakiwa na wenzi wao imendelea kuporomoka kila wakati hivyo ofisi yetu imeliona hilo na umuhimu wake hivyo kuchukua jukumu la kuhamasisha wanaume kushiriki katika hupata huduma za afya wakiwa na wenzi wao” BUTUYUYU amesema.

Kunafaida kubwa kwa wenzi kushiriki pamoja katika huduma za afya  ya uzazi kama vile kupima pamoja, hususani maambukizi ya VVU kwani kwa kufanya hivyo mnaweza kujitambua na kuishi maisha ya kumlinda mtoto pamoja na mwenzi wake endapo mmoja wao atagundulika ana maambukizi, BUTUYUYU amesea

Ameongeza kua mbali na kupima magonjwa pia kunaelimu mbalimbali ikiwemo kujifunza namana ya kupanga uzazi, jinsi ya kulea mimba kujiandaa  kupokea mtoto atakapozaliwa  pamoja na jinsi ya kumlea.

Kwakuona umuhimu wa swala hilo kwa wananchi wa TANZANIA,   ENGENDER HEALTH kwa kushirikiana na shirika la FHI 360 limetoa mradi wa champion  wa kuhamasisha vyombo mbalimbali vya habari kushiriki katika kampeni hii ili kuandika habari pamoja na vipindi vyenye kutoa ujumbe wenye kuhamasisha wenza kushiriki katika huduma za afya ya uzazi,

Akiongea katika semina ya waandishi wa habari iliyofanyika katika ukumbi wa IFISI COMMUNITY CENTER afisa mratibu mwandamizi wa mradi wa champion MUGANYIZI MUTTA amewataka waandishi kushiriki katika kampeni hizi.

“Mradi huu upo katika mikoa kumi yenye maambukizi ya juu ya VVu, kwa hiyo tumelenga katika kuhamasisha wanaume kupunguza kuwa na mahusiano ya wanawake wengi, kupambana na mila na desturi katika jamii, Kuweka sera mahari pa kazi kuhusu swala la wanaume na maambukizi ya VVU” amesema MUGANYIZI.

Ameongeza kuwa habari zilenge kuhamasisha mambo hayo muhimu na  mwandishi  atakaye andika habari na ikatumika katika chombo chake itakuwa imeinga katika shindano la Champion ambalo zaidi ya Tshs milioni mbili kushindaniwa.
   

Tuesday, April 23, 2013

WANAUME WATAKIWA KUONGOZANA NA WENZI WAO KATIKA KUPATA HUDUMA ZA AFYA

mmutta@fhi360.org
NILITEMBELE KITO CHA AFYA CHA RUANDA KILICHOPO MWANJELWA JIJI MBEYA KUJIONEA HUDUMA ZINAVYOENDLEA HUSUSANU HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI NA MTOTO


SELINA KOMBANI MRAIBU WA HUDUA ZA AFYA YA UZAZO NA MTOTO ALIE UPANDE WA KULIA AKIONGEA NA MASHAKA BONIFAS PAMOJA NA MKEWE SEKELA MWASONYA WALIPOHUDHURIA KLINIKI PAMOJA



BAADA YA MAHOJIANO SELINA ANAMPATIA HUDUMA HARAKA KWAKUA AMEONGOZANA NA MWENZI WAKAKE


BAADA YA KUWAHUDUMIA WALE WALIONGOZANA NA WENZI WAO KATIKA KUPATA HUDUMA NDIPO SERINI HUAANZA KUTOA ELIMU KWA WALE AMBAO HAWAKUONGOZANA NA WENZI



                   BAADA YA MAFUNZO NDIPO SHUGHURI ZA UPIMAJI ZINAENDELEA

BAADHI YAO WAKISUBILIA HUDUMA ZA DAKRALI WAKIWA KATIKA FORENI TOFAUTI NA WALE WALIKWENDA NA WENZI WAO HUPEWA KIPAU MBELE




JESTINA LUHANGA AKICHEKA JAPO KWA MAUMIVU MAKALI KUTOKANA NA MAUMIVU YA KUJIFUNGUA KWA UPASUAJI BAADA YA KUFARIJIWA NA MWENZI WAKE KWA KULETEA ZAWADI YA KITOTO CHA KIKE

BAADHI YA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WAKIWA KATIKA WAD YA MAMA WAJA WAZITO WAKIMTAKIA HARI BI, JESTINA

Baraza la mawaziri kigugumizi


Huenda Rais Uhuru Kenyatta akalitangaza Baraza la Baraza la mawaziri wiki hii.

Nairobi.Baraza la mawaziri nchini Kenya linangojewa kwa hamu na wananchi ambapo wangi wanatarajia liwe la mseto kama ilivyo Katiba ya Kenya.

Taarifa kutoka Kenya ambazo ni za kuaminika zimesema kwamba kuna uwezekano mkubwa kutangazwa kwa Baraza hilo kati kati ya wiki hii.

Pia Taarifa zilifichua kwamba washirika kwenye muungano wa Jubilee bado wanajadiliana kuhusu ni upande upi utatoa nafasi kwa baadhi ya vyama vidogo vilivyotia sahihi mkataba wa maelewano baada ya uchaguzi mkuu kwa lengo la kuimarisha utawala wa Jubielee.

Kutokana na hali hiyo raia wa  Kenya wamekuwa wakisubiri kwa hamu kusikia baraza jipya la mawaziri likitangazwa .

Taarifa ziliendeela kudodosa kwamba  mahojiano na washirika wa karibu wa viongozi yalionyesha kuwa viongozi hao wameamua kubadilisha kabisa muundo wa utawala.

Kwa sasa anachokifanya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akiwa na timu yake ,anaandaa majina ya baraza lake la Mawaziri na pia makatibu,wakuu wa mashirika pamoja na nyadhifa zingine za juu wakiwemo wakurugenzi wa Wizara na Idara.

Hiyo ina maana kuwa Wakenya watajionea baraza jipya kabisa la mawaziri, makatibu wapya, mabalozi, maofisa wakuu wa mashirika ya serikali na wakurugenzi wa wizara na idara mbalimbali.

Hata hivyo awali Rais Kenyatta alishatoa ahadi ya  kulitangaza baraza lake la  mawaziri wapya huku akizingatia taaluma, utendaji wa kazi, uwakilishi wa kimaeneo na jinsia.
Kutokana na hali hii, baadhi ya mabalozi walioagizwa warejee nyumbani huenda wasirudi katika nafasi zao za awali.

Thursday, April 18, 2013

WASIFU WA MAREHEMU FATUMA BINTI BARAKA 'BI KIDUDE'


Marehemu Bi Kidude alikuwa ni gwiji wa muziki katika Bara la Afrika. Jina lake halisi ni Fatuma binti Baraka. Bi Kidude ni msanii mkongwe na mahiri sana katika fani ya muziki wa mwambao ambao hujulikana kwa jina la Taarabu.


Muziki huu ambao ni mchanganyiko wa muziki toka nchi za Kiarabu na vionjo vya muziki wa Kiafrikaumekita sana katika mwambao wa Afrika Mashariki yaani Zanzibar, Mombasa, Lamu na kwingineko.


Leo hii ni Marehemu! Nguli na Mtunukiwa wa Nishani ya Uhuru wa Tanganyika/Tanzania 2012, Fatuma binti Baraka au Bi Kidude, alizaliwa katika kijiji cha Mfagimarigo Zanzibar katika familia ya watoto saba (7). Baba yake Mzee Baraka alikuwa ni mfanyabiashara wa nazi, zao ambalo ni la kutumainiwa sana Zanzibar.


Bi Kidude aliwahi kusimulia kuwa hafahamu tarehe halisi aliyozaliwa, isipokuwa anachojua ni kwamba alizaliwa wakati rupia ikitumika kama fedha, na vilevile ana hakika ni kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Ulaya. Wataalamu wa mahesabu baada ya kupata taarifa hizo wakampigia mahesabu na kumkabidhi miaka yake kwamba ni zaidi ya miaka 90.


Bi Kidude aliendelea kusema uimbaji aliuanza tangu alipokuwa na umri wa miaka kumi na alijifunza kutoka kwa msanii mkongwe na aliyetamba sana enzi hizo Sitti binti Saad. Anasema wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali walikuwa wakifika Zanzibar kuja kumwona Sitti, na kwa vile Bi Kidude na Sitti walikuwa wako karibu basi yeye alikuwa akiwapeleka wageni wale nyumbani kwa Bi Sitti, wakifika huko wageni walikuwa wakiingia ndani na yeye kubakia nje, kule ndani Bi Sitti alikuwa akiwaimbia wale wageni, na yeye huku nje alikuwa akimsikiliza kwa makini na kumfuatiza jinsi alivyokuwa akiimba. Aliendelea hivyo hadi akawa mahiri sana katika uimbaji.


Alipokuwa na miaka 13, kwa mara ya kwanza alitoroka nyumbani kwao Zanzibar na kukimbilia Tanzania Bara, baada ya kulazimishwa kuolewa. Lakini alipokuwa kigoli wa kutosha kuolewa aliolewa ingawa ndoa hiyo nayo haikudumu kutokana na manyanyaso aliyokuwa akiyapata, hivyo aliamua kukimbilia kaskazini mwa Misri ikiwa ni katika miaka ya 1930, huko aling'ara sana katika fani yake ya uimbaji na uchezaji ngoma. Lakini ilipofika miaka ya 1940 aliamua kurudi nyumbani Zanzibar ambako aliendelea na shughuli zake uimbaji.


Bi Kidude hategemei kazi moja tu ya kuimba, kwani pia ni mfanyabiashara ya 'wanja' na 'hina' ambavyo anavitengeneza yeye mwenyewe, pia ni mtaalamu wa matibabu kwa dawa za mitishamba na zaidi ya hayo ni mwalimu mzuri sana wa 'Unyago' na ameanzisha chuo chake mwenyewe na anasema katika wanafunzi wake wote hakuna aliyepata talaka kutoka kwa mumewe.


Watu wanasema 'Utu uzima dawa' Bi Kidude ana upeo mkubwa sana wa akili kwani pamoja na kukulia katika mazingira yaliyogubikwa na tamaduni za kiarabu ambapo mwanamke anatakiwa wakati wote akiwa hadharani ajifunike, Bi Kidude aliliona hili katika upeo mwingine kwamba ni sheria tu ya kitamaduni toka Uarabuni, hivyo aliamua kuvunja sheria hiyo na kuondoa hijabu mwilini mwake, na sasa hivi anavaa kama Mtanzania na si kama Mwarabu. Lakini hakubakia hapo alivunja na miiko mingine zaidi ya kutokunywa na kuvuta, kwani Bi Kidude anakunywa pombe na kuvuta sigara jambo ambalo si kawaida kwa wanawake Zanzibar.


Bi Kidude amekwisha tembelea nchi nyingi sana ikiwa ni pamoja na Oman, Ufaransa, Hispania, Ufini, Ujerumani na Uingereza.


Amekwisha pata tuzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ile ya Tamasha la Filamu la Nchi za Jahazi (ZIFF) mwaka 1999 tuzo ni ya maisha. Pia mwaka jana tuzo ya WOMAX ilienda kwake.


Nyimbo alizowahi kuimba ni pamoja na Muhogo wa Jang'ombe, na anaimba kwa Kiswahili na Kiarabu. Hakuwahi kupata elimu nyingine zaidi ya Kurani.


Bi Kidude pia amekuwa akishirikishwa na wasanii wengi wakongwe na chipukizi katika nyimbo zao. Miongoni mwa nyimbo zinazotamba sana siku hizi ambazo Bi Kifude ameimba na vijana wa kisasa ni za Msanii Ali Toll maarufu AT.


Mbali na AT lakini pia Bi Kidude amewika na kung'ara zaidi katika wimbo mwingine wa vijana wa Ahmada Umelewa wa Msanii Offside Trick ambao umepigwa marufuku kupigwa kwa sasa visiwani Zanzibar.


R.I.P FATUMA BARAKA “BI KIDUDE”..