Pages

Ads 468x60px

Tuesday, July 30, 2013

Majambazi wavamia na kuua kwa kumpiga lisasi mfanya biashara wa kisimani Tunduma na kutokamea na zaidi ya shilingi milioni ishirini


Ni wale wanao badilisha fedha katika mpaka wa Tanzania na Zambia


mfanya biashara JULIUS VISENT maarufu kwa jina la DELE akiwahishwa katika hospitali ya Rufaa mbeya kujalibu kuokoa maisha yake
 

Sunday, July 28, 2013

WAIGIZAJI WA MBEYA CITY MOVIE WAKIWA KATIKA MAZOEZI YA KUKAMLISHA FILAM YA BINADAM KIGEU GEU WANAYOTEGEMEA KUANZA KUPIGA PICHA HIVI KARIBUNI






WAIGIZAJI WAKIWA KATIKA MIKAO MBALIMBALI YA MAZOEZI YANAYOENDELEA KATKA UKUMBI WA CCM MKOA

MAMRUKI WA TIM YA WATUMA SALAM WAIFUNGA KWA MBINDE BARAKA FC


Nikatika mechi ya kugombania mbuzi kati ya timu ya watangazaji na watuma salamu wa Baraka fm Radio

Timu ya watuma salam yaibuka washindi kwa mabao matatu kwa mbili thidi ta watangazaji





KIKOSI KILICHOWAKILISHA KWA UPANDE WA TIMU YA BARAKA FC


KIKOSI KILICHOWAKILISHA TIMU YA WATUMA SALAMU
 PROGRAM MENEJA LINA MWAMBUNGU AKIONGEA NA WATUMA SALAMU KABLA YA KUWAKABITHI ZAWADI
 MWASIBU WA BARAKA FM RADIO FANUEL MWANDEKO AKIWAPONGEZA WATUMA SALAMU KWA USHINDI HUO
EMILI RAZALO AKIIPATIA GOLI LA KWANZA TIMU YA WATANGAZAJI WA BARAKA RADIO
FANUEL NA LINA VIONGOZI WA BARAKA WAKIKABIDHI ZAWADI YA MBUZI KWA VIONGOZI WA WATUMA SALAMU
          OBI MWAKASAGULE AKIPOKEA ZAWADI YA MBUZI

"SASA NIMEOKOKA.....UJINGA SITAKI TENA"...LULU MICHAEL



MUIGIZAJI machachari wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema baada ya kupata misukosuko ya kimaisha, sasa maisha yake ameyaelekeza katika sala kumuomba Mungu amsamehe makosa yake. 


Lulu alisema hayo juzi, katika kipindi cha Friday Night Live (FNL), kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha EATV cha Jijini Dar es Salaam.

“Sasa hivi nasali sana, namuamini Mungu katika maisha yangu na mbali ya kwenda kanisani, pia nasali mwenyewe katika sala zangu.

“Ningependa maisha ya sasa ninayoishi ningeishi siku za nyuma, lakini yote ya Mungu labda maisha yale nisingeyaishi siku za nyuma, ningekuja kuyaishi baadaye,” alisema Lulu.

Katika hatua nyingine, alisema anavutiwa na kazi ya msanii wa bongo fleva, Bernard Paul ’Ben Pol’ ambaye tungo za nyimbo zake zinamkosha kuzisikiliza.

MKIMBIAJI WA KIKE MKENYA, IRENE CHEBET CHEPTAI, AANGUKA NA KUZIMIA WAKATI AKIMALIZIA MBIO ZA MITA 3,000 JIJINI LONDON......


Collapsed: Irine Chebet Cheptai was rushed to hospital after collapsing following the 3,000m
Jopo la Madaktari wakihaha kumpatia huduma ya kwanza, mkimbiaji mwanadada wa nchini Kenya, Irine Cheptai, aliyeanguka na kuzimia wakati akimalizia mbio za mita 3,000 kwenye Uwanja wa Olimpiki.
treatment: Chebet Cheptai left the track unconscious but, according to reports, later regained consciousness in hospital
Cheptai akiwa amewekeaa mtungi wa hewa ya oksijeni, baada ya kuanguka na kuzimia kutokana na shambulio la moyo. Hata hivyo aliweza kupata fahamu na kuzinduka baada ya kufikishwa hospitali.
The Kenyan finished 11th in the race
Cheptai (wa pili kulia) akikimbia mbio za mita 3,000 kwenye Uwanja wa Olimpiki jijini London.
*********************************
LONDON, England

Cheptai, binti wa miaka 21, alimaliza mbio akiwa nafasi ya 11, katika muda bora zaidi katika rekodi yake binafsi, alipotumia dakika 8:56.20, lakini akaanguka ghafla na kupoteza fahamu baada tu ya kuvuka mstari wa kumalizia

MKIMBIAJI wa mbio ndefu wa kimataifa wa Kenya, Irine Chebet Cheptai jana alikimbizwa hospitali kwa matibabu baada ya kupatwa na mshituko wa moyo kwenye Uwanja wa Olimpiki baada ya kumaliza mbio za mita 3,000.

Cheptai, binti wa miaka 21, alimaliza mbio akiwa nafasi ya 11, katika muda bora zaidi katika rekodi yake binafsi, alipotumia dakika 8:56.20, lakini akaanguka ghafla na kupoteza fahamu baada tu ya kuvuka mstari wa kumalizia.

Madaktari waliokuwa uwanjani hapo wakaharakisha kumtundikia mtungi wa Oksijeni, ambapo kwa mujibu wa taarifa kuhusiana na tukio hilo zilipasha kuwa alikuja kurejewa na fahamu akiwa hospitalini.

Tukio lake limeshtua wengi kutokana na kukimbia katika mbio fupi kulinganisha na zile alizozoea za mita 5,000, ambazo ameshiriki Diamond League mara mbili msimu huu, na anakumbukwa kwa rekodi yake ya dakika 14:50.99 jijini Shanghai, Mei mwaka huu.
Daily Ma

Thursday, July 25, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUTURU NA WANANCHI MKOANI ARUSHA

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: 

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tano kutoka kushoto) akishiriki swala ya Magharibi na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wa Mkoani Arusha, wakati wa hafla ya Futari ya pamoja aliyoiandaa na kufuturu na wananchi hao katika Hoteli ya Naura Mkoani Arusha jana Julai, 23, 2013. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwaongoza baadhi ya wananchi wa mkoani Arusha kuchukua futari, wakati wa hafla ya Futari ya pamoja aliyoiandaa na kufuturu na wananchi hao katika Hoteli ya Naura Mkoani Arusha jana Julai, 23, 2013. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wageni wake baada ya kushiriki nao futari ya pamoja aliyoiandaa na kufuturu na wananchi hao katika Hoteli ya Naura Mkoani Arusha jana Julai, 23, 2013. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakiagana na wageni wao baada ya kushiriki nao futari ya pamoja aliyoiandaa na kufuturu na wananchi hao katika Hoteli ya Naura Mkoani Arusha jana Julai, 23, 2013. Picha na OMR

Sunday, July 21, 2013

Lowassa amfagilia Rais Kikwete


Na Swahili TV

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa  Edward Lowassa (pichani), amemsifia Rais Jakaya Kikwete kuwa ameweza kuifanya Tanzania kupata heshima katika ulingo wa kimataifa, aliyasema hayo wakati akihojiwa na Swahili TV jijini Washington DC.
 
Alisema kitendo cha Rais wa Marekani  Bwana Barack Obama kuja nchini na viongozi mbalimbali wa mataifa makubwa  kumeonyesha Rais Kikwete  anakubalika.

“Ni hivi karibuni  tu  Rais Xi Jinping wa China, Rais Obama na Rais mstaafu wa Marekani  George W.Bush  walikuwa nchini Tanzania, hii inaonyesha kuwa Tanzania iko juu katika medani za kimataifa” alisema Mheshimiwa Lowassa.
 
Mheshimiwa Lowassa ambaye yuko nchini Marekani kwa ziara ya kikazi, aliongeza kwa kusema, Rais  Kikwete anastahili pongezi sana kwa hilo kwani sio rahisi kwa viongozi wa mataifa makubwa kutembelea nchi zingine  labda kama mko juu sana katika medani za kimataifa.
 
Pia alisema  Rais Kikwete amekuwa akihusishwa  na utatuzi au ushauri wa kutatua matatizo mbalimbali ya nchi zingine na pia ameanza kuishirikisha Tanzania katika usimamizi wa amani katika nchi mbalimbali.

Tanzania iliweka historia hivi karibuni kwa maraisi wawili wa Marekani kukutana  katika nchi moja kwa wakati mmoja,  Rais Barack Obama na George W.Bush walikutana jijini Dar es Salaam mwezi huu.
Kwa habari zaidi tembelea Swahili TV Blog 

MIILI YA MASHUJAA 7 WA JWTZ WALIUAWA SUDAN YAWASILI DAR


 Moja ya majeneza yenye miili ya Askari 7  waliuawa na waasi wakilinda amani Darfur, Sudan, likishushwa kutoka kwenye ndege ya Umoja wa Mataifa (UN), baada ya kuwasili leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


                           Baadhi ya wanafamilia wakiwa na huzuni wakati wa mapokezi hayo



Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia), akiwa na  baadhi ya viongozi waliofika kupokea miili hiyo.



Saturday, July 20, 2013

RAIS KIKWETE AKUTANA NA PROFESA LIPUMBA KWA MAZUNGUMZO IKULU DAR



  
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana alikutana na Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba na kufanya naye mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam.
 
 Mazungumzo hayo yalihusu masuala mbalimbali ya siasa na uchumi nchini.Pichani Rais Kikwete akiwa na Professa Lipumba katika mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam jana. 
 
Rais Kikwete, akiagana na Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba baada ya mazungumzo yao jana. Picha na Fredy Mar

TAARIFA MAALUM YA TFDA KWA UMMA KUHUSU UTHABITII WA DAWA AINA YA 'DICLOFENAC' ILIYODAIWA KUWA NA MDHARA MWILINI..!


1.Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ina jukumu la kulinda na kudumisha afya ya jamii kwa kuhakiki ubora, usalama na ufanisi wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.

2. Hivi karibuni, TFDA imepokea taarifa ya kuwepo kwa hofu juu ya usalama wa dawa aina ya Diclofenac kupitia mitandao ya simu na vyombo vya habari. Kufuatia taarifa hiyo, TFDA inapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:
a. Diclofenac ni dawa iliyoko kwenye kundi la dawa zinazojulikana kitaalam kama “Non – Steroidal Anti-inflammatory Drugs”(NSAIDs). Dawa hizi hutumika kutuliza maumivu na kuondoa uvimbe unaosababishwa na



magonjwa mbalimbali. Magonjwa hayo ni pamoja na magonjwa ya viungo, mifupa, uvimbe wa fizi na maumivu ya kichwa.

b. Mamlaka imesajili dawa ya Diclofenac kutoka makampuni mbalimbali ndani na nje ya nchi baada ya kutathmini ubora, usalama na ufanisi wake. Hata hivyo Diclofenac, kama ilivyo kwa dawa nyingine, ina madhara yanayofahamika. Kwa baadhi ya wagonjwa Diclofenac inaweza kusababisha vidonda vya tumbo, kuumwa kichwa, kuharisha, kutapika na kuwashwa mwili.



c. Pamoja na madhara yaliyoainishwa hapo juu, hivi karibuni imetolewa taarifa na Mamlaka ya udhibiti wa dawa ya nchi za Umoja wa Ulaya (European Medicines Agency) kwamba watu wenye matatizo ya moyo na shinikizo la damu, kisukari, waliowahi kupata kiharusi, wenye lehemu (cholesterol) nyingi kwenye damu, mshituko wa moyo na wanaovuta sigara wanaweza kupata matatizo kwenye moyo na mfumo wa damu ikiwa watatumia Diclofenac kwa kiwango kikubwa na kwa muda mrefu.



3. Kufuatia taarifa hiyo, TFDA inaendelea kufuatilia madhara yatokanayo na dawa hii kwa kushirikiana na taasisi nyingine za kitaalam ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO). Aidha, tunawakumbusha watoa huduma za afya kutoa taarifa za madhara yatokanayo na matumizi ya dawa kwa kujaza fomu maalum zinazopatikana katika vituo vyote vya afya nchini.

4. Mamlaka inasha+uri watoa huduma za afya nchini na wagonjwa kuchukua tahadhari za madhara haya hasa kwa watu wenye magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, kisukari, wenye lehemu nyingi kwenye damu na wanaovuta sigara ikiwa ni pamoja na kutumia dawa mbadala.

5. Vilevile wananchi wanashauriwa kuepuka matumizi holela ya dawa bila kupata ushauri wa kitaalam ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) – Makao Makuu
S. L. P 77150
Dar-es-Salaam
Tanzania
Simu: +255 22 2450751
+255 22 2450512
Barua pepe: info@tfda.or.t

MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU AUAWA KIKATILI



Mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Kizega wilayani Iramba Bi. Mariamu Alphonce mwenye umri wa miaka kumi ameuwawa kikatili kwa kukatwa shingo na kucharangwa kwa panga sehemu mbalimbali za mwili wake na kaka yake bwana Elibariki  Alphonce.


Akieleza kwa uchungu baba wa mtoto huyo bwana Alphonce Msengi amesema alipofika nyumbani kwake majira ya saa kumi na moja jioni alikuta damu nyingi na alipo angali vizuri alimuona mtoto wake Mariamu Alphonce akiwa amekatwakatwa kwa mapanga na tayari alikuwa ameshafariki.



Bwana Msengi baada ya kuona hivyo alipiga yowe na walikuja majirani na watoto na wakamwambia tumemuona mtoto wako Elibariki akiwa na mapanga mawili akikimbia huku akiwa hana nguo. 

Wakieleza mwenyekiti wa kitongoji Bi Vailet Mbigu na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kizega bwana Elisante Gyuzi wamesema pamoja na shule kuandaa taratibu zote za mashishi , kijana aliyefanya unyana huo huwa anavuta bangi na mara nyingi alikuwa akisikika kumtishia kumuuwa baba yake kwa kumkata kwa panga.




Kwa upande wake  kaimu mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Iramba daktari Timoth Sumbe amesema wamempokea Mariamu Alphonce akiwa ameshafariki huku mwili wake ukiwa na majeraha ya kukatwakatwa sehemu ya shingoni,kichwani.



Akiongea kwa simu kamanda wa jeshi lapolisi mkoani Singida bwana Godfrey Kamwela amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na jeshi lake lina endelea kumsaka mtuhumiwa bwana Elibariki Alphonce ambaye alitoweka baada ya mauaji ili aweze kufikishwa mahakamani.

Wednesday, July 17, 2013

PICHA: WANAJESHI WA TANZANIA WALIO UAWA DARFUL WAAGWA


 Capt. John Kivunge, a Tanzanian Staff Officer with JOC, reads a program of the brief ceremony.
Prayers from a chaplain.
Prayers from an Imam for the fallen peacekeepers.

Military salute as the 'Last Post'  rings out by Nigbatt in honour of the fallen heroes.