Pages

Ads 468x60px

Saturday, August 31, 2013

Safari yangu ya South Afrika ni njema sana


NILISOMA DARASANI DARAJA LEFU LA MTO ZAMBEZI NCHINI ZIMBABWE LEO NIPO HAPO
                                             NIKIWA HARALE NIMELALA HOTEL HII

JAMANI ILIKUA NI NGUMU KUACHA ASILI YA VYAKULA KUTOKANA NA MAZOEA KWANI NCHI ZA WENZETU KUNAVYAKULA VYA KUSHANGAZA IKANILAZIM KURUDI NYUMBANI YANI CHIPSI SAMAKI
                                      KAMA TZ TU MIFUGO KWA KWENDA MBELE
KILICHONISHANGAZA SANA WENZETU HUKU KUPIKA NI MAJANGA KWANI VYAKULA WANATEGEMEA KUNUNUA SUPER MERKET VILIVYOPIKWA TAYALI NAMI SIKUA NYUMA NASUBILA KUHUDUMIWA CHAKULA CHA MCHANA
 HAPANA SIKUELEKEA BORDER NILIKWANDA KUPUMZIKA HOTELI TAYARI KWA KUVUKA BEITBRIDGE ASUBUHI YEKE KUELEKEA AFRIKA YA KUSINI


HOTEL NILIYOTUMIA KUPUMZIKA NCHINI ZIMBABWE KABLE YA KUVUKA KWANDA KWA MZEE MADIBA
                ASUBUHI NILIENDELEA NA TARATIBU ZA KUVUKA BORDER YA ZIMBABWE


NAMSHUKURU MUNGU NIMEFIKA SALAMA NA HII MOJA YA MITAA  YA JOHNAZBAG NCHINI AFRIKA KUSINI TUOMEANE KWANI BAADA YA MAFUNZO YA WIKI TATU NTAKUA NIKIANZA SAFARI YA KURUDI NCHI YENYE ASALI NAYO MAZIWA KISIMA CHA AMANI TZ

Thursday, August 29, 2013

BREAKING NEWS......ASKOFU MOSES KULOLA AFARIKI DUNIA

moses_b8f0d.jpg
TAARIFA zilizotufikia hivi punde zimesema kuwa Askofu Moses Kulola amefariki dunia.

Chanzo chetu cha kuaminika ambazo kimesema, Askofu Kulola amefariki katika hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.
Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu.

Katika uhai wake, amepata watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dr Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi.
KATIKA PICHA
ALIPOKUWA MGONJWA
KATIKA MKUTANO WA INJILI
ALIPOKUWA NCHINI  ISRAEL

Wednesday, August 21, 2013

RWANDA NA UGANDA WAJITOA BANDARI YA DAR ES SALAAM



Chama cha Wasafirishaji wa Mafuta Tanzania (Tatoa), kimesema Rwanda na Uganda zitajitoa kutumia Bandari ya Dar es Salaam kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu.

Katibu Mtendaji wa Tatoa, Zacharia Hanspope aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya kukutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuwa nchi hizo zinajitoa kutokana na matatizo mbalimbali ambayo kwa muda mrefu zimekuwa zikiyalalamikia lakini Serikali haikuchukua hatua.

Hanspope alisema ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ni baadhi ya vikwazo ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa kwa muda mrefu na wafanyabiashara mbalimbali wa nchi hizo.

“Serikali ipunguze gharama za ushuru wa barabara na ushuru wa forodha ili kuwa na ushindani sawa na bandari nyingine na hivyo kuzivutia kutumia Bandari ya Dar es Salaam,” alisema Hanspope.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo alikataa kuzungumzia lolote kuhusu suala hilo akisema halina mantiki yoyote kwake.... “Hivi hilo jambo unaloniuliza lina sense (mantiki) yoyote? Mie siwezi kujibu lolote nenda ukamuulize mwenyewe (Hanspope) maana wakati akisema mimi sikuwepo.”

Alisema kujitoa kwa Rwanda na Uganda kuitumia Bandari ya Dar es Salaam hakutakiathiri chama hicho tu, bali uchumi wa taifa kwa ujumla.

Hayo yanatokea wakati Rwanda ikiendeleza vita yake ya maneno na Tanzania na mfululizo wa matukio ya kuitenga Tanzania kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Viongozi wa Kenya, Rwanda na Uganda walikutana Juni 25, mwaka huu mjini Entebbe, Uganda na kukubaliana kuongeza uhusiano wa kibiashara baina yao.

"MWAKYEMBE ALINDWE" BARAZA LA VIONGOZI WA DINI



 Mwenyekiti wa baraza la viongozi wa dini la kupambana na dawa za kulevya nchini Shekhe wa mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum

BARAZA la Viongozi wa Dini la Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, limetaka Jeshi la Polisi kumpa ulinzi Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, kutokana wa ujasiri alioonesha kupambana na dawa za kulevya.


Kutokana na ujasiri huo, Baraza hilo ambalo Mwenyekiti wake ni Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, limempongeza Dk Mwakyembe na kusisitiza umuhimu wa ulinzi huo kwake, kwa kuwa vita aliyoanza, inaweza kuhatarisha usalama wake.
Shekhe Salum alisema hayo jana alipozungumza na vyombo vya habari Dar es Salaam, akiongeza kuwa kitendo alichofanya waziri huyo kimeonesha uzalendo, ujasiri na upendo alionao kwa Taifa, alilosema linalochungulia kaburi kutokana na dawa hizo.
 

Maombi maalumu
Kutokana na ujasiri huo na hatari inayomkabili Dk Mwakyembe, pamoja na kutaka ulinzi wa Polisi, Shekhe Salum pia aliomba viongozi wa dini wa imani zote, kumwombea kwa uthubutu huo. Alisema watampa ushirikiano kwa kuunga mkono juhudi anazoonesha ambazo kwa kiasi kikubwa anaamini zitarejesha heshima ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA).


“Kwa dhati kabisa Baraza linataka mawaziri na viongozi nchini kuiga mfano wake, ili kuliondoa Taifa letu katika sifa mbaya ya dawa za kulevya,” alisema Shekhe Salum.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo, viongozi wana uwezo mkubwa wa kujitolea kupambana na dawa hizo, isipokuwa hakuna aliye tayari kuonesha uthubutu wake, suala alilosema kwa kiasi kikubwa limechangia mapambano dhidi ya dawa hizo kutofanikiwa.


Alisema kutokana na hali hiyo, Taifa limeendelea kupoteza nguvu kazi ya vijana wanaoathirika kila kukicha, kutokana na matumizi ya dawa hizo, jambo alilotaka viongozi wenzake wa dini kujipanga kuhakikisha wanawasaidia kupata nafuu wale ambao tayari wameshaathirika. Baraza hilo pia liliipongeza Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kwa ukaribu na mikakati inayowezesha ukamataji na udhibiti wa utumiaji wa dawa hizo nchini.
 

Waathirika
Shekhe Salum alisema kwa hali ilivyo sasa, familia moja kati ya mbili imeathirika na dawa hizo. Kutokana na hali hiyo, alisema Taifa limeendelea kupoteza nguvukazi ya vijana kila kukicha kutokana na matumizi ya dawa hizo, akataka viongozi wenzake wa dini kujipanga kuhakikisha wanawasaidia kupata nafuu ambao tayari wameathirika.
Tembelea http://jambotz8.blogspot.com/ kila siku.


Mwishoni mwa wiki iliyopita, Waziri Mwakyembe alitaja maofisa usalama wanne wa uwanja huo na watendaji wengine, wanaotuhumiwa kupitisha kilo 180 za dawa za kulevya zenye thamani ya Sh bilioni 6.8. Dawa hizo zilikamatwa Julai 5 Afrika Kusini zikitoka Tanzania, kupitia JNIA.

Mbali na kutaja maofisa hao, pia aliagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), maofisa hao wafukuzwe kazi, wakamatwe na kufunguliwa mashitaka mahakamani. Watuhumiwa Maofisa usalama hao watakaofukuzwa kazi na kufunguliwa mashitaka ya jinai chini ya Sheria ya Kuzuia Dawa za Kulevya ni Yusufu Issa, Jackson Manyonyi, Juliana Thadei na Mohamed Kalungwana.

Mbali na maofisa hao, pia aliagiza Jeshi la Polisi kumwondoa mara moja katika uwanja huo, askari Polisi, Ernest na kumchukulia hatua za kinidhamu kwa kushiriki kwenye njama za kupitisha mabegi sita ya dawa za kulevya, yaliyokamatwa Afrika Kusini. Pia alisema Polisi inapaswa kumsaka Nassoro Mangunga, aliyekwepa vyombo vya Dola Afrika Kusini na kutoroka na mabegi matatu ya dawa hizo. Tembelea http://jambotz8.blogspot.com/ kila siku.

Dk Mwakyembe alisema mbeba mizigo katika uwanja huo, Zahoro Seleman, anapaswa kufukuzwa kazi, kukamatwa na kufunguliwa mashitaka, ili aunganishwe na wenzake kujibu mashitaka ya jinai. Dk Mwakyembe pia aliiagiza Idara ya Usalama wa Taifa kuendesha uchunguzi wa kina kwa maofisa waliokuwa zamu siku ya tukio, kwa kuchelewa kuwafikisha mbwa wakati mwafaka kukagua mabegi hayo na kulisababishia Taifa fedheha kubwa.

Tuesday, August 20, 2013

Majambazi waliokamatwa na Jeshi la polisi juzi barabara ya mandela jijini dar es salam baada ya kuiba pesa kituo cha mafuta buguruni malapa wafariki dunia wakati wakipatiwa matibabu hospitalini



TASWIRA YA VURUGU MAANDAMANO YA CHADEMA JIJINI MWANZA.











MAANDAMANO ya amani yaliyokuwa yameandaliwa na chama cha demokrasia na maendeleo(chadema) yamegeuka shubiri kwa wakazi wa jiji la Mwanza baada ya kuibuka mapambano makali baina ya waandamanaji hao na jeshi la polisi mkoani Mwanza na kusababisha polisi kutumia nguvu kuwatawanya wafuasi wa chama hicho.

Maandamano hayo ya amani ambayo yalianzia katika eneo la Buzuruga nje kidogo ya jiji la Mwanza yalikuw ayakiongozwa na wabunge Highness Kiwia wa Ilemela  pamoja na Ezekiel Wenje kuelekea katika viwanja vya Furahisha yalilenga kumshinikiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ernest Ndikilo kutoa barua zinazodaiwa kuandikwa na ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi kuwarejesha madiwani watatu waliotimuliwa katika Manispaa ya Ilemela kutokana na kushindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo.

Polisi wenye silaha pamoja na askari kanzu walianza kutanda katika eneo hilo la Furahisha wakiongozwa na Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Mwanza RCO Konyo ambaye alikuwa akitumia gari lenye namba za usajili DK 068EXV aina ya Toyota Land Cruiser

Maandamano hayo ambayo awali yalionekana kana kwamba yangelimalizika salama yaliwasili katika viwanja vya Furahisha majira ya saa 5.38 huku yakiongozwa na gari la polisi lenye namba za usajili za nchi ya Uganda  779 UAG likiwa nimesheheni polisi wenye silaha nzito ikiwa ni pamoja na mabomu ya machozi na bunduki pamoja na askari kadhaa ambao walikuwa katikati ya maandamano hayo.

Baada ya maandamano hayo kuwasili katika viwanja vya Furahisha kwa amani,waandamani hao ambao walikuwa na mabango mbalimbali yaliyosomeka kuwa ‘Matata hatutaki uendelee kuwa Meya wa Ilemela rudia kazi yako ya awali, na jingine Jaji Sumari tumechoka kuahirisha mara kw amara kesi dhidi ya Matata na jingine  lililosomeka kuwa RD Ndikilo tunahitaji barua za kurejeshwa kwa madiwani wetu.

Hata hivyo tofauti na ilivyokuwa imetangazwa kuwa maandamano hayo ya amani yangelipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ernest Ndikilo,hakukuwa na kiongozi yoyote wa Serikali ambaye alikuwepo uwanjani hapo kupokea maandamano hayo.

Kufuatia kutoonekana kwa kiongozi yoyote wa Serikali,viongozi wa chadema pamoja na wabunge wao walikutana kwa faragha kwa dakika kadhaa kwa ajili ya kujua hatima ya maandamano hayo ambapo Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje alipanda jukwaani saa 6.45 na kuwaeleza maelfu ya waandamanaji kuwa wameamua kumtuma Mbunge wa Ilemela Highnes Kiwia kwenda ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuchukua majibu kwa ajili ya kuwaletea wananchi walioandamana juu ya hatima ya madiwani hao.

Hata hivyo saa moja baadae Mbunge huyo alisimama jukwani na wakuwaeleza waandamani hao kuwa simu ya Mbunge Kiwia ilikuwa haipatikani hivyo kuwataka kuandamana kwenda kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza kujua kulikoni na hapo ndipo hali ya hewa ilipochafuka.

Jeshi la polisi baada ya kuona wandamanaji hao wameanza kuelekea katika ofisi za Mkuu wa mkoa liliwataka kutawanyika ambapo waandamanaji hao walikaidi ndipo jeshi la polisi lilipoamua kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi hao.

Vurugu hizo ambazo zilianza majira ya saa 7.30 zilisababisha kufungwa kwa baadhi ya barabara kutokana na waandamanji hao kuweka vizuizi vya mawe na kuchoma matairi,ambapo pia maduka na ofisi mbalimbali zililazimika kufungwa kwa muda kupisha vurugu hizo.

Baadhi ya wananchi ambao walikuwa wakitumia usafiri wa umma walionekana wakishuka kupitia katika madirisha ya magari hayo na kukimbia kwa hofu ya kujeruhiwa na mabomu pamoja na mawe ambayo yalikuwa yakirushwa na waandamanji hao kwa jeshi la polisi.

MKUU WA MKOA WA MWANZA ALONGA.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza akizungumza na Mbunge Kiwia pamoja na viongozi wa chadema ofisini kwake alisema kuwa ameshangazwa na uvumi huo kuwa ofisi yake imekalia barua a kurejeshwa kwa madiwani Abubakar Kapera(Nyamanoro),Dan Kahungu(Kirumba) pamoja na Marietha Chenyenge(Ilemela).

RC Ndikilo alisema kuwa Serikali imekuwa ikifanya kazi zake kwa maandishi na sio kwa kufuata maneno ya mtaani na kueleza kuwa hana barua yoyote toka ofisi ya Waziri Mkuu inayomualifu kuhusu kuwarejesha madiwani hao baada ya kukata rufaa.

“Hata Mbunge kuna siku ulinipigia simu ukiniuliza juu ya kuwepo kwa barua hizo name nilikujibu kuwa kwa kuwa uko hapo Bungeni Dodoma ambapo pia kuna ofisi ya Waziri Mkuu nilikujibu kuwa ni muhimu ukawaona viongozi wakuu wa Tamisemi ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu,pia nilikushauri kuwa wakupe japo nakala ya barua hiyo”,alisema RC Ndikilo.

“Lakini cha kushangaza nimekuwa nikisikia maneno ya ajabu kuwa nimeficha barua za madiwani hao,ikumbukwe kuwa madiwnai hao hawakukata rufaa kwangu bali walikata rufaa ngazi ya juu kabisa,ili kukata mzizi wa fitina naomba kati ya tarehe 26 hadi 27 wewe Mbunge pamoja na mimi twende TAMISEMI kukutana na viongozi ili kukata mzizi wa fitina na tuje tuwaeleze wananchi ukweli uliopo”,alisema RC Ndikilo.

Kuhusu suala la Meya Henry Matata kutoondolewa madarakani RC Ndikilo alisema kuwa hawezi kulizungumzia suala hilo kw akuheshimu mamlaka ya mahakama na kuwataka chadema kuvuta subira hadi pale mahakama itakapotoa maamuzi yake.

KAULI YA MBUNGE KIWIA.

Akizungumza katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Kiwia alisema kuwa waliamua kuitisha maandamano hayo kutokana na kuelezwa na Waziri Hawa Ghasia kuwa tayari barua hizo zimeishatumwa mkoani Mwanza.

“Mheshimiwa Mkuu wa mkoa hawa madiwani waliosimamishw ani wawakilishi wa wananchi,wamekaa nje kwa miezi saba sasa na uchaguzi wa Meya haukuwa halali ndio maana tuliamua kuitisha maandamano kwa ajili ya kuhakikisha madiwani hawa wanarejeshwa.

RPC MANGU.

Akizungumza kwa simu juu ya kutokea kwa vurugu zilizosababisha kupigw akwa mabomu ya machozi,Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu alisema kuwa polisi walifanikiwa kudhibiti vurugu hizo na hadi sasa hawezi kusema ni wananchi wangapi ambao walikamatwa kuhusu vurugu hizo.

WANANCHI WAWALAUMU VIONGOZI NA WANASIASA NA KUWAPONGEZA POLISI.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na Mtanzania juu ya vurugu zilizotokea waliwaonyoshea kidole wanasiasa pamoja na viongozi wa mkoa wa Mwanza kutokana na kushindwa kusema ukweli juu ya tukio hilo.

Baadhi walisikika wakisema kuwa kama barua zipo kweli madiwani hao wanapaswa kupewa na kama azipo basi walioeneza maneno hayo wachukuliwe hatua kali kutokana na uchochezi.

Wananchi hao pia walilipongeza jeshi la polisi kutokana na kutumia busara badala ya nguvu kuhakikisha maandamano hayo yanakuwa ya amani.

Sunday, August 18, 2013

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA FIESTA KIGOMA ILIVYOFANA..!!


Sehemu ya umati wa watu waliofurika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika usiku huu wakiburudika na Wasanii wa Serengeti Fiesta 2013
Burudani ya kutosha kabisa
Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Neylee akiimba kwa hisia kwenye jukwaa la tamasha la Serengeti Fiesta 2013,usiku huu kwenu uwanja wa Lake Tanganyika.
Hapatoshi ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika usiku huu.
Mwanamuziki mahiri wa muziki wa Dansi,Christian Bella akikamua jukwaani usiku huu ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika,mkaoni Kigoma ambapo watu wamefurika ile mbaya.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Cassim Mganga akiimba jukwaani mbele ya maelfu ya wakazi wa Kigoma ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika.
Sehemu ya umati wa watu waliofurika ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika usiku huu
Msaniii anekuja kwa kasi kwenye miondoko ya Hip Hop,Stamina akikamua jukwaani usiku huu mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Kigoma waliojitokeza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta
Ni Shangwe tu ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma usiku huu,wakati tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea
Yaani hapatoshi kabisa,wakazi wa Kigoma wamecharuka na burudani murua kabisa ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rachael kutoka THT,akionesha umahiri wake wa kutumbuiza jukwaani usiku kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Washabiki wa tamasha la Fiesta wakifuatilia kwa makini yanayojiri usiku huu ndani y uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
Wadau nao wamejitokeza kwa wingi
Peter Msechu na densa wake wakikamua vilivyo usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.
Pichani ni msanii wa bongofleva ajulikanae kwa jina la Shilole na madansa wake wakiwachengua vilivyo wakazi wa Kigoma,waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta,ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika