Pages

Ads 468x60px

Thursday, February 27, 2014

BARAZA LA MITIHANI LATOA UFAFANUZI MATOKEO KIDATO CHA NNE


BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

                                                       

 UFAFANUZI WA MASWALI MBALIMBALI YA WADAU WA ELIMU KUHUSU MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2013
 
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania Dkt Charles Msonde
 Imetolewa Na:

KAIMU KATIBU MTENDAJI


25 Februari, 2014


UFAFANUZI WA MASWALI MBALIMBALI YA WADAU WA ELIMU KUHUSU MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2013

Baraza la Mitihani la Tanzania lilitangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2013 tarehe 21/02/2014. Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Baraza limekuwa likipokea maswali mbalimbali yanayoashiria kuwa baadhi ya wadau wa elimu hawakuelewa vizuri kuhusu Viwango vya Ufaulu (grade ranges), alama ya chini ya ufaulu (pass mark) na Ufaulu wa jumla wa mtahiniwa (overall performance). Baraza la Mitihani linapenda kutoa ufafanuzi katika mambo hayo kama ifuatavyo:

1.        Viwango vya ufaulu (grade ranges) ni makundi ya alama yanayopangwa ili kuwaweka pamoja watahiniwa wenye uwezo unaofanana katika somo husika na kuwatofautisha na watahiniwa waliopo katika kundi jingine. Makundi haya hupangwa ili kuwawezesha wadau kutambua namna watahiniwa walivyotawanyika katika viwango mbalimbali vya umahiri wa somo husika. Baraza la Mitihani la Tanzania, limekuwa likitumia makundi Matano (5) kwa kipindi kirefu hadi mwaka 2012. Aidha, Kuanzia Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2013, Baraza limeanza kutumia utaratibu wa Makundi Saba (7) ambayo ni A, B+, B, C, D, E na F. Utaratibu huu umelenga kupunguza mlundikano mkubwa wa alama katika kundi moja. Mgawanyo wa makundi hayo ni kama inavyoonekana kwenye Jedwali la 1.


Jedwali Na 1: Viwango vya ufaulu vilivyotumika katika Matokeo ya CSEE 2013.


Kundi
Gredi
Alama
Idadi ya Pointi
1
A
75 - 100
1
2
B+
60 - 74
2
3
B
50 - 59
3
4
C
40 - 49
4
5
D
30 - 39
5
6
E
20 - 29
6
7
F
0 -  19
7


Aidha, Idadi ya makundi ya ufaulu hutofautiana kati ya nchi na nchi kulingana na mahitaji ya nchi husika.  Kwa mfano; Kenya wana makundi Kumi na mbili (12), Malawi Tisa (9), Uganda Tisa (9), Nchi za Afrika magharibi (Nigeria, Ghana, Siera Leone na Liberia) makundi Tisa.


2.        Kwa kuzingatia viwango vya ufaulu vilivyoainishwa katika makundi saba yaliyopo kwenye Jedwali na 1, kiwango cha chini cha ufaulu ni gredi D na kiwango cha juu cha ufaulu ni Gredi A. Mtahiniwa atakuwa amefaulu somo husika iwapo atapata gredi D na kuendelea. Aidha, mtahiniwa aliyepata gredi E na F atakuwa hajafaulu somo husika.


3.        Madaraja ya ufaulu yamepangwa kwa mujibu wa kifungu cha 20 (1)-(6) cha Kanuni za Mitihani kinachoelekeza kuwa Ufaulu katika daraja la Kwanza hadi la Tatu upangwe kwa kuzingatia jumla ya alama (Points) na Ufaulu katika Daraja la Nne unapangwa kwa kuzingatia ufaulu wa chini aliopata mtahiniwa ambao ni gredi D katika masomo yasiyopungua mawili au ufaulu kwa kiwango kisichokuwa chini ya Gredi C katika somo moja. Hivyo, madaraja yaliyotumika ni kama yanavyoonekana kwenye Jedwali la 2.


Jedwali 2: Madaraja yaliyotumika katika CSEE 2013


Daraja
Pointi
I
7 – 17
II
18 – 24
III
25 – 31
IV
1.      Ufaulu katika somo moja kwa kiwango kisichokuwa chini ya Gredi C au
2.      Ufaulu katika masomo yasiyopungua mawili katika Gredi D
0
Alama chini ya D mbili


4.        Kwa mujibu wa Kanuni za Mitihani, ufaulu wa somo katika Gredi A hadi C utakuwa ni ufaulu wa “Credit” na Gredi D itahesabika kuwa ni “pass”. Aidha Gredi E na F zitakuwa alama za kufeli.


5.        Baraza la mitihani la Tanzania linapenda kutoa taarifa kwamba ufafanuzi wa sifa za kujiunga na mafunzo katika ngazi mbalimbali kwa kutumia mfumo huu mpya wa madaraja utatolewa na mamlaka husika ambapo Kamishna wa Elimu atalitolea ufafanuzi zaidi.





Imetolewa Na:



KAIMU KATIBU MTENDAJI

Wednesday, February 26, 2014

HATARI SANA ANGALIA MAPICHA:HAKUNA ASKOFU BILIONEA TANZANIA KAMA HUYU ....ULINZI WAKE NI ZAIDI WA RAIS KIKWETE


ASKOFU na Nabii George David ‘Geordavie’ wa Kanisa la Geordavie Ministry ‘Ngurumo ya Upako’ lililoko jijini Arusha na Kawe, Dar hivi karibuni alifanya mkutano mkubwa na kutikisa nchi  kwa kuwa na magari ya kifahari na ndege aina ya helikopta ‘chopa’ iliyokuwa ikirandaranda juu ya anga kulinda usalama wake, Uwazi lina ushuhuda wa kutosha.
Katika mkutano huo uliofanyika Karatu mkoani Manyara, mwandishi wetu alishuhudia msafara wa Geordavie ambaye hutoa huduma ya uponyaji kwa njia za miujiza, ukiwavutia watu wengi kwa kuwa ulikuwa na ulinzi mkali ambao haujawahi kutokea.
Mbali ya kuwa na chopa iliyokuwa ikiimarisha ulinzi ambayo ameinunua hivi karibuni, askofu huyo alikuwa na msururu wa magari yenye thamani kubwa yanayomfanya kutajwa kuwa tajiri kuliko maaskofu wengine wanatoa huduma katika makanisa ya kiroho Tanzania.
Akiwa Karatu, mbali na ulinzi binafsi, Geordavie alikuwa akilindwa na askari wa jeshi la polisi, askari kanzu, Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wale wa usalama barabarani.
Mbali na askari hao wa serikali ambao wamekuwa wakimlinda kila anapofanya mikutano yake, pia Geordavie analindwa na askari wake binafsi hali iliyowafanya baadhi ya watu kuamini kuwa ulinzi wake ni kama ule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’.
“Sijawahi kumuona JK akilindwa na chopa lakini mtumishi wa Mungu Geordavie analindwa na ndege katika msafara wake! Hii ni mara yangu ya kwanza kuona,” alisema muumini mmoja ambaye hakupenda kutajwa gazetini.
Hata hivyo, baadhi ya watu walikuwa wakihoji utajiri wa askofu huyo kutokana na fedha nyingi anazozitumia anapofanya mikutano katika sehemu mbalimbali jijini Arusha.
“Tunajua kuwa ni tajiri, lakini anapata wapi fedha za kutumia hivi?” alihoji muumini aliyejitambulisha kwa jina moja la Julius ambaye naye alihudhuria mkutano wa askofu huyo anayetumia kaulimbiu ya Ngurumo ya Upako katika kutoa huduma yake.
Pia, waumini wengine walilalamikia ugumu wanaoupata wanapotaka  kumuona mtumishi huyo wa Mungu kutokana na ulinzi mkali anaopewa.
“Kila mtu alitamani kumuona mtumishi wa Mungu lakini haikuwezekana kutokana na ulinzi wake kuwa mkali, utajiri wake hakuna mfano, hata kule nyumbani kwake Arusha, anaishi kama Mfalme Daud,” alisema Fred Mushi.
Gazeti hili lilimsaka Askofu na Nabii Geordavie kwa lengo la kutaka kujua sababu ya kuwa na ulinzi mkali na kutumia magari ya kifahari ikiwemo chopa katika mikutano anayoifanya lakini simu yake iliita bila kupokelewa.

WAREMBO KWENYE SHOW YA OMMY DIMPLES JIJINI LONDON





































Thursday, February 20, 2014

AJALI LORI LA MAFUTA LATEKETEA KWA MOJA WATUNNE WAPOTEZA MAISHA


                                  Wanainchi wakiangalia Lori baada ya kuungua
                    Mabaki ya Lori hilo bada ya kuteketea kabisa na moto jioni hii
                            Baadhi ya wasafiri wakitazama lori lililongua jioni hii

                Bonde la mlima sekenke linavyoonekana na baadhi ya miti imeungua
                                            Hii ni njia ya mlima sekenke
            Haya ni mabaki ya mwili wa mmoja ya watu walikuwam kwenye Lori hiloo
Moto ukimalizikia kwa mbaliii kama inavyoonekana

Lori la mafuta limeanguka katika eneo la milima ya sekenke mkoani singida na kuua watu wanne hapohapo.Chanzo cha ajali hiyo ni breki kufeli kukamata wakati lori hilo lilipokuwa linashuka mlima huo.Shuhuda wa ajali hiyo bwana Julius chacha alipoongea na mtandao wetu amesema kwamba Lori hilo lilipoacha njia lilipinduka na kuingia bondeni na kushika moto.
Akiendelea kuongea shuhuda huyo alisema walishindwa kutoa msaada wowote kwa kwa moto uliposhika ulikuwa mkubwa na hawakuwa na vifaa vya kuokolea.
Watu wanne wamekufa papo hapo kutokana na ajali hiyo Polisi walikuwa bado hawajafika eneoo la tukio mpaka tunaondoka eneo la tukio.na Dj Sek

MSAADA TOKA UINGEREZA KWA MAMA WA MAPACHA WANNE WA MBEY


Misaada ya hali na mali imeanza kumiminika kwa ajili ya Aida Nakawala (25) mkaazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne mapacha kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya. 
 Msamaria mwema wa Uingereza, Bi Gladness Sariah, ametuma maboksi mawili yenye nguo na vitu kadhaa vya watoto, ambavyo vimewasili salama katika ofisi za Michuzi Media Group (MMG) inayoendesha Globu ya Jamii jijini Dar es salaam baada ya kusafirishwa bure na Wazee wa Kazi, Serengeti Freight Forwarders ya huko Uingereza. 
 Hivi sasa MMG ikishirikiana na waratibu wa misaada kwa mama huyo, Mbeya Yetu Blog, wanaandaa utaratibu wa kumfikishia Mama Aida mizigo yake haraka iwezekanavyo. 
 Kwa niaba ya mzazi wa mapacha hao, Michuzi Blog na Mbeya Blog zinatoa shukrani za dhati kwa msamaria mwema Gladness Sariah kwa wema na upendo aliouelekeza kwa mzazi huyo. 

Huo ni mfano wa kuigwa, na tunatarajia misaada zaidi itatolewa na wasamaria wema ambao tunajua mko wengi kila kona ya dunia. 
 Kama umeguswa na hili na unataka kutoa msaada tafadhali wasiliana na issamichuzi@gmail.com ama j.mwaisango@tonemg.com nasi tutafikisha ubani wako. 
 Muhidin Issa Michuzi
Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.
Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi.