Pages

Ads 468x60px

Monday, April 28, 2014

WAUMINI WA DINI YA KRISTO WAMETAKIWA KULINDA SANA AMANI


MWINJILISTI ESAU MWAMTOBE





KWAYA KUU YA KANISA LA MORAVIANI USHIRIKA WA IWAMBI AMBAO WALIKUA KIVUTIO SANA KWA UIMBAJI WAO KATIKA IBAADA HIYO

KWAYA KUU YA USHIRIKA WA MBEYA MJINI WAKITMBUIZA KATIKA IBAADA
                       KWAYA YA SHULE YA JUMAPILI USHIRIKA WA MBEYA MJINI

                                KWAYA YA UINJILISTI USHIRIKA WA MBEYA MJINI





KWAYA YA VIJANA USHRIKA WA MBEYA MJINI WAKIONGOZA NYIMBO ZA KUABUDU ZIKIONGOZWA NA MWENYEKITI WA MICHEZO PENIELI MWAISANGO










ASILI YA JINSI YA KUONGOZA NYIMBO KWA KUPIGA MAPIGO KUTOKA KWAYA KUU IWAMBI

                                                                    HABARI KAMILI



WAUMINI WA DINI YA KRISTO WAMETAKIWA KULINDA SANA AMANI
KWAKUA NDIYO THAMANI YA MAISHA YA MWANADAMU HAPA DUNIANI

Hayo yamesemwa na mwinjilisti ESAU MWAMTOBE wa kanisa la Moraviani Tanzania Jimbo la kusini magharibi ushirika wa Mbeya mjini alipokua akihubiri katika ibaadailiyofanyika kanisani hapo  jumapili ya kwanza baada ya Pasaka, akisoma samo kutoka yohana 20:19-31 ambalo yesu alipo fufuka aliwaombea wanafunzi wake Amani.

Ili kuipata Amani ni lazima watu wamtegemee mungu na kumtumikia kwa uaminifu, akinukuu maandiko kutoka katika Biblia MWAMTOBE amesema  utafuteni kwanza ufalme wa mungu na mengine yote mtazidishiwa, watu wamekua wakitafuta Amani na furaha katika kujilimbikizia mali kitu ambacho ni ubatili mtupu

Wakristo wamekua wakikwepa majukumu yao katika kumtumikia mungu ili kueneza ijili yake ulimwenguni kote na kusababisha baadhi ya watu wengine kushindwa kumjua mungu na kukosa Amani  katika maisha yao na hivyo wengi watakosa kuiona mbingu kwa kukosa la kutomtumikia.

MWAMTOBE ameongeza kua hakuna jambo la muhimu katika maisha ya mwanadam zaidi ya Amani na ndicho kitu chenye thamani kubwa, Ameongeza kua wapo watu wana mali na kila kitu kilichopo duniani lakini hawana furaha moyoni mwao kutokana na kutokuwa na Amani.

Friday, April 25, 2014

Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) kimemtuhumu meya wa jiji la mbeya kuendesha njama za kumfunga jela mwenyikiti wao mtaa wa itiji



Ezekieli king alieye hukumiwa kutumikia kifungo cha miaka saba kwa kosa la kupiga na kujeruhi.

Mwenyekiti Wa Chadema kata ya Itiji Daniel Mwakasita akiongea na mwandishi wa habari hii
Mwenyekiti wa mtaa wa itiji Ezekiel King akiwa kizimbani baada ya kuhukumiwa
                       Meya wa jiji la Mbeya Atanas kapunga ( Picha na Libraly yetu)

                                                                    Habari Kamili

Hayo yamesamwa na DANIELI MWAKASITA mwanyekiti wa kata ya Itiji kupitia chama hicho katika ofisi za wilaya ya mbeya mjini walipokua wakushughulikia rufaa ya kupinga hukumu hiyo
MWAKASITA  amemtupia lawama meya wa jiji la mbeya ATANASI KAPUNGA kuhusika na hukumu hiyo kua haikuwa na haki na kunasiasa ndani yake kutokana na kutokuwepo kwa mahusia mazuri kati yake na mwenyekiti huyo kutoka na kukihama chama chake mapinduzi (ccm) kwenda chadema

Ameongeza kua meya huyo alijitapa katika moja ya mikutano yake ya hadhara kwamba atahakikisha mwenyekti huyo ametumia gharama yoyoe kumfunga na sasa adhima yake imetimia na wao kama wanachama wa chadema hawako tayali kukubaliana na hukumu hiyo hivyo wana kata rufaa na kuweka wakili wa kumtetea kiongozi wao.

Nae DOMI MWASALEMBA mmoja wa wafuasi wa chama hicho amehoji hukumu hiyo kuwa haikua na haki kutokana na kesi kutofuta ushahidi wa kidaktali kwamba anaedai kupigwa anatatizo la ugojwa wa akili na kwamba alileta fujo kilabuni akapingwa na watu wengine lakini amemtaja king kwakua ndiye aliye mpeleka Polis kisha Hospital

Awali mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Itiji Jijini Mbeya mkoani Hapa anayewakilisha (CHADEMA) Ezekiel King(52) na mwenzake Antony Simon(53) wamehukumiwa kwenda jela miaka 7 kutokana na makosa ya shambulio na kumdhuru mwili Nicholaus Mwakasinga(56) mkazi wa Itiji mjini humo.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi wa mahakama ya Mkoa wa Mbeya Maria Batulaine, mbele ya mwendesha mashtaka wa serikali Juliana William alisema kuwa washitakiwa kwa pamoja walimshambulia Mwakasinga kwa kumpiga na kumjeruhi kichwani na mkononi wakati wakiwa katika kilabu cha pombe za kienyeji kilichopo mtaa wa Itiji.

Alisema anawatia hatiani washitakiwa hao kutoka na kuwepo kwa mashaka juu ya ushahidi wa watu watatu  upande utetezi kugongana na hivyo kuridhika na ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka  na hivyo kuwatia hatiani na kwamba hata hivyo wanayo fursa ya kukata rufaa iwapo hawajaridhika na hukumu iliyotolewa.


 

MWENYEKITI WA CHADEMA AFUNGWA MIAKA 7 KWA KUJERUHI KILABUNI


Mwenyekiti wa CHADEMA Ezekiel King akiteta jambo na jamaa zake mara baada ya kuhukumiwa kwenda jela miaka 7 kwa kosa la kumjeruhi mtu kilabuni
Askari polisi wakimsindikiza Mwenyekiti wa CHADEMA baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 7 jela
Mmoja wa jamaa waliohudhuria mahakamani akimwaga machozi baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA mtaa wa Itiji kuhukumiwa kifungo  cha miaka 7 kwa kujeruhi.
MWENYEKITI wa serikali ya Mtaa wa Itiji Jijini Mbeya mkoani Hapa anayewakilisha (CHADEMA) Ezekiel King(52) na mwenzake Antony Simon(53) wamehukumiwa kwenda jela miaka 7 kutokana na makosa ya shambulio na kumdhuru mwili Nicholaus Mwakasinga(56) mkazi wa Itiji mjini humo.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu mkazi wa mahakama ya Mkoa wa Mbeya Maria Batulaine, mbele ya mwendesha mashtaka wa serikali Juliana William alisema kuwa washitakiwa kwa pamoja walimshambulia Mwakasinga kwa kumpiga na kumjeruhi kichwani na mkononi wakati wakiwa katika kilabu cha pombe za kienyeji kilichopo mtaa wa Itiji.
Alisema anawatia hatiani washitakiwa hao kutoka na kuwepo kwa mashaka juu ya ushahidi wa watu watatu  upande utetezi kugongana na hivyo kuridhika na ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka  na hivyo kuwatia hatiani na kwamba hata hivyo wanayo fursa ya kukata rufaa iwapo hawajaridhika na hukumu iliyotolewa.
Akitoa mifano ya kesi  mbalimbali zinazoshabihiana na kesi hiyo Hakimu Batulaine alisema kuwa makosa hayo ni kinyume cha kifungu sheria  cha kanuni ya adhabu namba 225 sura ya 6 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Hakimu Batulaine alisema kuwa katika maelezo ya shahidi namba moja Mwakasinga  ambaye ndiye mlalamikaji  ni kwamba alijeruhiwa na kuumizwa na washitakiwa alipoingia katika kilabu cha pombe za kienyeji na  kwamba alifanyiwa hivyo baada ya kuingia ndani ya kilabu hicho na kusukumwana kuanguka nje.
Alisema katika maelezo hayo shahidi namba moja hadi namba tatu wa upande wa mashtaka walitoa ushahidi unaofanana lakini maelezo ya mashahidi wa upande wa utetezi yanajichanganya na hivyo kutoa mashaka juu ya utetezi wao.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mlalamikaji Mwakasinga alipigwa na kujeruhiwa na washitakiwa na baadaye washitakiwa hao walimchukua na kumpeleka kituo cha Polisi wakidai kuwa mlalamikaji Mwakasinga alikuwa akifanya vurugu kilabuni.
Hata hivyo mlalamikaji ambaye alilazwa katika hospitali ya rufaa wodi namba nne ambayo hulazwa watu wenye ugonjwa wa akili ili kumpima kama alifanya vurugu kutokana na ugonjwa wa akili alipotoka alifungua mashtaka ya kupigwa na washitakiwa hao ambao walikamatwa na kufunguliwa kesi ya kudhuru mwili.
Katika utetezi wake kabla ya kutolewa hukumu Mshitakiwa King aliomba mahakama impunguzie adhabu kutokana na kuwa na watoto sita na kuwa hakujua kama kitendo cha yeye kama kiongozi wa mtaa kuamka  kwenda kwenye tukio kingemtia hatiani.
 
 Posted  by Rashid Mkwinda