Wale wote walioasi hawatafika mbinguni kwa baba
Viongozi wa mbeya moraviani Town Choir wakimtembelea Askofu Conradi Nguvumali Nyumbani kwake Sumbawanga
Mbeya moraviani Town Choir wakiimba na Mkuu wa mkoa wa Sumbawanga Stella Manyanya wakimpokea Waziri Mkuu Pinda
Viongozi Mbalimbali akishikana mikono na Viongozi Baada ya kuwasili Ikulu ya Mijini Sumbawanga
Wachungaji wakiwa katika hali ya kumsikiliza waziri mkuu katika ukumbi wa mikutano katika ikulu ya Sumbawanga
Mbeya moraviani Town Choir wakonesha umahili wao katika uimbaji uliofanyika katika kanisa la moraviani Sumbawanga
Maandamano ya waumini na wachungaji kuelekea uwanja wa kumbukumbu ya Nelesoni Mandela kwa ajili ya ibaada ya kumsimika Askofu nguvumali
Askofu Nguvu Mali akiwasili na kusalimiana na maaskofu na viongozi katika viwanja vya Neleson Mandela
Mgeni Rasmi Waziri Mkuu Pinda akiwasili Kiwanjani hapo akipokelewa na maaskofu Mbalimbali
Mbeya Moravian Town choir Wakitumbuiza mara baada ya kuwasili Mgeni Rasmi waziri mkuu Pinda kiwanjani hapo
Kwaya mbalimbai zimeshiriki kuimba katika ibaada ya kumsimika Askofu Nguvu mali
Katibu wa jimbo la Sumbawanga akitambulisha wageni mbalimbali waliofika kushudia ibaada ya mbaraka wa Askofu
Baba na mama wa Askofu nguvumali
Watu mbalimbali waliofika kushuhudia Mbaraka wa Askofu Nguvumali wakiwa katika uwanja wa mandela
Mjumbe wa bodi ya kanisa aCharle Mwakipesile akiteta jambo na Askofu Kiongozi
Maasikofu wakisoma masomo katika ibaada ya mbaraka wa Askofu Nguvumali
Askofu Aizack Nikodemu wa jimbo la Magharibi Tabora akihubiri katika ibaada hiyo
Matukio mbalimbali ya shughuri nzima ya mbaraka wa Askofu Nguvu mali
Wachungajiwaki andaa kiti cha kiuaskofu
Askofu Nguvumali paoja na mke wake baada ya kubarikiwa
Mc Charles Mwakipesile akiongoza utaratibu wa mkutano huo na alikua kivutio sana katika ibaada hiyo
HABARI KAMILI
Charles Mwaipopo
Askofu wa Kanisa la Moraviani Tanzania Jimbo la
Magharibi Tabora AIZACK NIKODEMU ameya
sema hayo katika Ibaada ya kumsimika
Askofu wa Kanisa la Moraviani Jimbo la Rukwa CONRAD NGUVUMALI iliyofanyika
katika uwanja wa NELSON MANDELA Sumbawanga na kuhudhuliwa na viongozi
mbalimbali wa kitaifa na madhehebu mengine ya kikristo nchini.
“Biblia imesema wazi kwamba kizazi hiki chote
kimewekwa akiba kwa moto wa milele kwani Yesu anasema nikifananishe na nini
kizazi hiki, watu wake hawambiliki hawasikii wameingiza siasa kanisani watu wame jaa unafiki wanacheka nawe kumbe
hawakutakii mema katika maisha yako” Amesema Nikodem.
Ameongeza kua dunia ina wacheka wale wote
waliopitwana wakati, kwakua wakati ni wakati tu wengi wao hutenda dhambi
zilizopitwa na wakati huko ni kupitwa na wakati kwakua mungu alikifutilia mbali
kwa maji kizi kilichopita na kumuokoa Nuhu kwa sababu ya dhambi.
“Hakuna dhambi iliyo mpya katika dunia hii wewe
uliyepitwa na wakiti unatenda dhambi zilizopitwa na wakati Mungu alikifutilia
mbali kizazi cha Nuhu kwasababu ya dhambi akaaanza kizazi kipya nacho kikaasi
akakakichoma moto enzi za Sodoma na Gomola, Nawaambia wale wote walioasi
hawataingia mbinguni” Ameongeza Nikodemu.
Akiongea kwa Msisitizo mkubwa juu ya ubaya wa dhambi
amesema Dhambi inalitesa kanisa, Taifa la Tanzania limegawanyika katika makundi
kwa sababu ya ambi na koo zimetengana, na maisha yamekua magumu, Mungu
anakusumbiria urudi kwake akupumzishe na kukuongoza katika maisha ya kumpendeza
yeye.
Kwa upande wao waumini waliohudhuria ibaada hiyo
wamempongeza mkuu wa mko wa Rukwa Stella Manyanya kwa kitendo chake cha ujasili
katika kutafuta suru kati mwasiasa mkongwe Dr Chrisent Mzinda kaya na Mbunge wa
Sumbawanga Mjini (ccm) Aeshi Hilaly Ambao wamekua wakitofautiana tangu uchaguzi
upite.
Pamoja na juhudi hizo haziku zaa matunda baada ya
Mzindakaya kukataa kusemehe mpaka pale watakapofuata taratibu na mashalti
aliyowapa wakati waziri mkuu alipojaribu kuwapatanisha kwamba zitumike taratibu
za vikao vya chama na si katika mikutano ya dini kwani haihusiani na siasa
Nae Aeshi Hilaly alikili kuwepo kwa tofauti kati
yake na na mkongwe huyo katika siasa na kusababisha kuwepo kwa makundi katika
chama chao na kumuomba msamaha mzee huyo akisema hakuna marefu yasiyo na ncha
naomba nisamehewe ili tuweze kuijenga Rukwa yetu.
Waziri mkuu Peter Pinda Amewataka wa viongozi kuto
kimbilia wala kufurahia kazi za kuwaongoza watu kwakua ni mzigo mkubwa ambao
hautakiwi kuona raha endapo unachaguliwa kuwa kiongozi wa kuongoza watu kwakua
ni vigumu sana kuwaongazo watu
Akinuukuu baadhi ya vifungu kutoka katika Biblia kwamba
aitakae kazi ya uasikofu ataka kazi njema lakini asiwe ni mtu mwenye kulaumiwa
na wengine uongozi si jambo jepesi hivyo ni vema kuhubili amani ili kanisa liwe
na amani na nchi pia iwe na amani
Pinda ameongeza kuwa
Nchi hii wala Serikali yake havina dini na itaeendelea hivyo japo wananchi wake
wana dini wanazotaka kuzitumikia hivyo basi amewataka viongozi wa dini kutoingiza
siasa katika dini zao ila wasiwakataze waumini wao kuwa na vyama wanavyopenda
kushabikia