WAMEDAI AME
WADHARAU NA KUWADHALILISHA SANA, BITI ZA
NYIMBO ZAKE AMETENGENEZA KATIKA STUDIO ZA MBEYA ADAI NI DAR-ES-SALAM
EMMANUELI MGOGO KATIKA ALBAM YA MSIKILIZE MUNGU
NAMBA YA MAWASILIANO NA IMAIL YAKE VINAVYO ONESHA SI ALBAM SI YA SAYUNI BAND BALI NA YAKE BINFSI
TASWILA NDANI YA DVD YAKE INAVYO ONESHA VEDEO NA OUDIO IMEREKODIWA WAPI
KWA UNDANI WA HABARI HII SOMA HAPA CHINI
IMMANUELI MGOGO AWACHEFUA MAPRODUCER WA MKOA WA MBEYA,
WAMEDAI AME
WADHARAU NA KUWADHALILISHA SANA, BITI ZA
NYIMBO ZAKE AMETENGENEZA KATIKA STUDIO ZA MBEYA ADAI NI DAR-ES-SALAM
Baadhi ya wamiliki wa studio na waandaaji wa nyimbo za injili mkoani hapa
wamemlalamikia mwambaji anae chipukia wa njimbo za injili EMMANUELI MGOGO kwa
kitendo alicho kifanya cha kuandika jina
la Studio ECK PRODUCTION ya jijini
Dar-es-salaam kwamba ndiyo iliyorekodi
nyimbo zilizomo katika albam yake ya MSIKILIZE MUNGU wakati sikweli nyimba hizo zimerekodiwakatika Studio za hapa jijini Mbeya.
Hayo yamebainishwa na Produser wa Studio ya Braju Baraka
Mwasambamba iliopo Airpot jijini hapa alipokua akiongea na mwandishi wa habari
hizi, amekiita kitendo alichokifanya mwimbaji huyo si cha uungwana na hakina
ustaarabu na hekima ndani yake kwani ni
kuudharau mkoa wa mbeya.
“Mwandishi kwanza ninasikitika sana kwa jinsi alivyo
tudhalilisha Immanueli Mgogo sisi
waandaaji wa nyimbi mkoani hapa, mimi nimetengeneza Bit ya wimbo wa Msikilize
Mungu, alikuja hapa na kwaya moja kwa lengo la kuwasaidia kurekodi nilipotengeneza hiyo Biti kwa lengo la
kuitengenezea hiyo kwaya yeye akasema naomba usiwape hawa ninaitaka niitungie
maneno nikamkubalia” alibainisha Mwasambamba
Ameongeza kua baadae alikuja na kuaanza kuingiza
maneno tukiwa wote hapa Studioni kwangu, tulipo maliza aliniomba aichukue data apelike
Dar es salaam ampelekee mpiga kinanda amjazie maeneo yaliyo acha wazi mimi
nilikubali nikampa hizo data nashangaa sana kuona ndani ya hiyo DVD yake ameandika OUDIO imetengenezwa na ECK PRODUCTION huu ni udhalilishaji.
Baraka amehoji kwamba kama kweli nyimbo hizo
zomerekodiwa Dar es salaama anaweza kudhibitisha?, je wale waimbaji wanao
mwitikia alikwenda nao huko ECK? Alihoji huku akiwa na jazba kwa jinsi
alivyolipokea swala hilo, tunajua waimbaji wengi wa huku Mbeya wakiisha pata
majini kidogo tu hupenda kuhamia huko
lakini si kututukana matusi watu wa mkoa huu kama huyu.
Kwa upande wake Producer Peter Mbuba wa H Studio iyopo maeneo ya Isanga
jijini hapa yeye kasema anamuachia Mungu kwa kitendo alichokifanyiwa na
mwimbaji huyo kwani amesikitishwa sana baada ya kuona wimbo alioutunga Producer
huyo na kuutengenezea Bit yake anakuta
anatukuzwa mtu mwingine.
“Mimi ndiye niliyetengeneza biti na maneno ya wimbo
wa Niko ulieko nimeiga kutoka kwa mwimbaji wa Afrika kusini Rebeka Marope
nashangaa leo hii naona katika cd yake kwamba imetengenezwa Dar es salaam na
Studio ya ECK hii si sawa hata kama ameona Mbeya hakuna watengezaji bola
angetengeneza huko”
Bwana, Mbuba ameongeza kwamba hata kama Mgogo
atapinga haya yeye anao ushahidi wa nyimbo hizo ikiwa ni pamoja na biti za
kinanda chake hakiingiliani na vinanda vingine anaweza kutoa ili kilinganishwe
na huyo anaemwita ECK, wa Da es salaam kwamba ndiye alie recod nyimbo hizo, kwakufanya
hivyo ni sawa na kuukataa mkoa wake ulio mtoa.
Nao baadhi ya waimbaji aliokua akiimba nao katika albam ya kwanza iliyokua ikiitwa Iko wapi njia ya Sayuni Band kwa kutotaka kutajwa majina wamesema wao katika albam ya Msikilize mungu hawajahusishwa na kwamba hawajui imerecodiwa lini wapi na kwa gharama gani na hata mapato yake hatuyajui.
“Ukweli ni kwamba Mgogo katika Sayun bandi ni
mwalimu tu na atabaki kua mwalimu sisi albam ya Msikilize mungu
Hatujashilikiswa kwa hiyo si ya Sayuni Bandi hiyo ni yake kama mgogo na ndio
mana ukiangali Imeandikwa Immanueli
mgaga hilo neon Sayun Bandi ameliweka tu wala si Sayuni Badi” Hyo yamesemwa na
baadhi ya waimbaji wa Sayuni Bandi.
Awali mwambaji Immanueli mgogo amekua akijipatia
umaarufu katika uimbaji wa nyimbo za injili ambapo mwanzoni mwa safari yake ya
uimbaji ilianzaia katika Albam ya kwanza iliyoitwa Iko wapi njia iliyo kua
chini ya Sayuni Band, albam hii ilitokea kutamba sana katika vymbo vya habari
na hata katika matamasha mbalimbali, na kitu ambacho kimemfanya atambulike ndani na nje ya mkoa wa Mbeya
Kama ilivyo kawaida ya baadhi ya watu wanapo pata
nafasi ya kupata umaarufu kidogo husahau aliko toka na kujiona mafanikio hayo
yamekuja kwa nguvu na juhudi za akili zake na kusahau msemo wa wahenge uliokua
ukisema ukimuona kobe juu ya mti ujue kapandishwa.