Wakiwepo watoto wachanaga wawili katika ajali ya basi dogo aina ya Hiace na Roli la mizigo katika maeneno ya mji mdogo mbalizi Nje kidogo ya jiji la Mbeya
Roli la mizigo na Toyota Hiace magari yaliyosababisha ajali
Roli la mizigo lilivyo baada ya baada ya ajali na lina milikiwa na Aledy chakachaka wa mbeya
NAIMA ITUGA MKAZI WA SIMIKE NA ANAFANYA SHUGHULI ZAKE SONGWE VIWANDANI AKIKIMBIZWA KUPATA MATIBABU ZAIDI
BAADHI YA MAJERUHI WAPATIWA RUFAA KUPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA
TAHADHALI
KAMA HAUTAWEZA KUVUMILIA KUANGALIA PICHA ZA MIILI YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA USISHUKE CHINI.
TUNAOMBA RADHI WAPENZI WETU WA BLOG HII KWA PICHA ZITAKAZOTUMIKA HAPA KATIKA HABARI HII KWAKUA ZIMEHALIBIKA VIBAYA KAMA HUWEZI KUZITAZAMA USIENDELEE KUSHUKA CHINI
BAADHI YA WATU WALIOKUFA WAKIWEPO WATOTO WAWILI WADOGO
MIILI YA WATU WALIOPOTEZA MAISHA KATIKA AJILI HIYO IKIWA KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI KATIKA HOSPITSLI TEULE YA MBALIZI
HABARI KAMILI YA TUKIO
Aidha, baadhi ya madereva wa daladala waliofika hospitalini waliweza kumtambua dereva wa Dalada hilo, ambaye ni miongoni mwa watu 10 waliofariki dunia katika ajali hiyo na kumtaja kwa jina la Petro Mng’ong’o.

WATU 10
wamefariki dunia papo hapo na wengine saba kujeruhiwa vibaya, baada ya basi
dogo aina ya Toyota hiace walilokuwa wakisafiria kuparamia Lori, maeneo ya mji
mdogo wa mbalizi barabara kuu ya Tanzania na Zambia
Tukio hilo
lilitokea majira ya saa 11.30 ambapo Toyota Hiace lenye namba za usajili T237
BFB , ililokuwa ikitokea Mwanjelwa kwenda
katika mji mdogo wa Mbalizi kulipalamia roli la mizigo lenye namba za
usajili T158 CSY aina ya tata
Taarifa
kutoka kwa mashuhuda wa ajili hiyo, zinadai kuwa huenda daladala hiyo ilikuwa
imepata hitilafu katika mfumo wa breki wakati likishuka katika mteremko mkali
wa mlima Iwambi, ambapo lilienda kuliparamia roli lililokua likitokea upandea
wapili na kuingia barabar kuu.
“Wote,
Dereva wa Daladala na roli wanaweza wakawa na makosa, kwani haiwezekani
ukaingia barabarani bila kuangalia, huku naye wa daladala alipaswa kupunguza
mwendo….sasa hapa wote wanapaswa
kulaumiwa” alisema shuhuda ambaye hakuwa tayari jina lake litajwe
Muuguzi Mkuu
wa Hospitali teule ya Ifisi, Sikitu Mbilinyi, alithibitisha kutokea kwa vifo
hivyo. kifafanua zaidi, Mbilinyi alisema walianza kupokea miili ya marehemu hao
na majeruhi majira ya saa 6:30, ambapo baadhi ya majeruhi walipewa rufaa na
kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.
Hata hivyo alisema,
ingawa hawakuweza kupata majina ya marehemu, walipokea maiti 10 kati yao, wanaume
walikuwa wanne na wanawake wanne, huku maiti za watoto wadogo walioonekana kuwa
chini ya miaka mitano zikiwa mbili.
Aliongeza
kuwa, kwa upande wa majeruhi walikuwa saba, ambapo kati yao wanawake walikuwa
wanne na wanaume watatu.
“Kati ya
majeruhi hao saba , watatu hali zao zilikuwa mbaya sana na tukaamua kutoa rufaa
na walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa ajili ya matiabu zaidi”
alifafanua Mbilinyi.
Aidha, baadhi ya madereva wa daladala waliofika hospitalini waliweza kumtambua dereva wa Dalada hilo, ambaye ni miongoni mwa watu 10 waliofariki dunia katika ajali hiyo na kumtaja kwa jina la Petro Mng’ong’o.
Naye
kondakta wa daladala hiyo, ambaye amejeruhiwa vibaya amejulikana kwa jina la
Justin Chaula (28), Mkazi wa Mabatini, Jijini Mbeya.
Mmoja wa
majeruhi hao, ambaye hata hivyo hakuwa tayari
kuzungumza chochote, alijitambulisha kwa jina la Naima Ituga, Mkazi wa Simike, Jijini hapa na
alikuwa akielekea kazini kwake maeneo ya Viwandani Songwe.
Mwisho.