Pages

Ads 468x60px

Monday, September 22, 2014

MBEYA CITY YAANZA NA SALE NYUMBANI DHIDI YA JKT RUVU



Imani za kishilikina za husika, mlinda mlango wa Jkt Ruvu ashindwa kumaliza mchezo huo atolewa uwanjani baada ya kupingwa upofu.
 Kipa wa Jkt Ruvu Jacson chove akiruka na beki wake kisha kuanguka chini kisha kushindwa kuona na kisha kutolewa nje ya uwanja


                   Madaktari wa timu hiyo wakijalibu kumpatia matibubu laiki ilishindikana kuona
 Baadhi ya wachezaji wenzake wakijaribu kumsihii ajikaze ili amalizie dakika zilizosalia lakini alikataa
                                 Sioniiiiiii siweziiiii baadhi ya maneno aliyotaka chove
                               Hapakua na jinsi chove alitoka nje ya uwanja huku akilia


                                   Matukio ya kuumia yalivyo kua katika mchezo huo












                            Matukio mbalimbali ya mchezo kati ya mbeya city na Jkt Ruvu








                                       Mwashabiki wa waliohudhulia katika mchezohuo

                     Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya Ahmed Msangi akiwasili uwanjani hapo

Baadhi ya mashabiki wakieleza hisia zao za kutokubalina na matokeo wengine wakitokwa na machozi kwa timu yao kutoka sale


                                                          HABARI SOMA HAPA


MBEYA CITY YAANZA NA SALE NYUMBANI DHIDI YA JKT RUVU

Imani za kishilikina za husika, mlinda mlango wa Jkt Ruvu atolewa uwanjani baada ya kushindwa kuona.

Timu ya mpira wa miguu mkoani Mbeya, Mbeya city imeanza michuano ya Vodacom kwa kusuasua baada ya kutoka sale ya bila kufungana na timu ya Jkt ruvu ya jijini dare s salaam ikiwa kiwanja cha nyumbani

Michuano hiyo iliyozinduliwa jumamosi hii ya 20 september katika viwanja mbalimbali nchini, Mbeya city ilianza kwa kuwa karibisha Jkt ruvu katika kiwanja cha kumbukumbu ya sokoine jijini Mbeya.

Katika mechi hiyo Mbeya city haikuonesha mchezo uliozoeleka kwa mashabiki wake ambao hua unakua kivutio kwa kile kinacho itwa amsha amsha na kupelekea matokeo ya sele kati yake na timu pinzani huku wakiwa wenyeji wa mchezo huo.

Baadhi ya mashabiki wa timu hiyo akiwepo Andulile mwakaje kutoka Tunduma ameutaka uongozi wa mbeya city kujipanga vizuri katika  michezo inayofuata kwani kiwango kilicho oneshwa na timu hiyo si cha kulidhisha sana ili kuleta upinzani uliokuwepo msimu uliopita

“Sisi na mashabiki wa Mbeya city ukweli hatujalidhishwa na jinsi amba vyo timu yetu imeonesha mchezo wa leo kwani sio kiwango chake ilicho kionesha msimu uliopita tunaomba uongozi uliangalie upya na kujipanga katika michezo inayo fuata” amesema mwakaje

Pamoja na hayo ndani ya mechi hiyo kikwazo kikubwa cha Mbeya city kilikua kwa mlinda mlango wa Jkt ruvu  Jacson chove ambae alikua kivutio sana kwa watazamaji wa mchezo huo kwakupangua mashuti kadhaa yaliyoelekezwa katika timu yake.

Baadhi ya mashuhuda walishangazwa na kitendo cha mlinda mlango huyo kushindwa kumaliza mchezo huo baada ya kutolewa nje ya uwanja kwa sababu ya kushindwa kuona

Shuhuda huyo  ambae hakutaka kutajwa jina lake amesema ameona mtu akitupa kitu mfano wa hilizi muda mchache kabla ya tukio hilo. Lililopelekea watu kuamini kuwa na imani za kishilikina.

Katika mechi hiyo mlinda mlango wa jkt ruvu Chove alishinda kumalia mchezo huo kabla ya dakika 15 kuisha kwa mechi hiyo alipoa angukachini  baada ya kugongana na beki wake na kisha  kushindwa kuona, Na mwisho wamchezo huo timu zote mbili zilishindwa kutambiana Kwa kutoka sale ya bila kufungana.   



Wednesday, September 17, 2014

Seed co kulejesha fadhila kwa jamii ya watanzania

 Yatoa zawadi ya madawati 100 yenye thamani ya milioni 15 zikiwepo simu za mkononi katika shindano la mashamba darasa katika shule za msingi nyanda za juu kusini

Kaimu mkurugenzi wa kampuni ya Seed co nyanda za juu kusini Michael Rikanga akiongea na waandishi wa habari na kuonesha mbegu wanazotegemea kuingiza katika kilimo msimu huu
                                   



            Waandishi wa habari mkoa wa mbeya wakimsikiliza kwa makini Rikanga
                              Hii ndiyo form maalimu ya kujisajili katika shindano hilo

 Shule ya msingi Nsoho iliyopo nje ya jiji la mbeya ambapo mwandishi wa habari hizi alifika kupata maoni ya waalimu na wanafuzi wanapokeaje shindano hili



Baadhi ya mashamba ya shule hiyo yaliyokodishwa kwa wanakijiji yakiandaliwa tayali kwa kilimo kwa msimu huu wa kilimo
 Msitu uliopandwa kuizunguka shule hiyo kama mradi ambao inasemekana umesababisha kukausha mto uliokua kipita na kutililisha maji karibu na shule hiyo
           Baadhi ya makazi ya wanakijiji wa Nsoho wanaoizunguka shule hiyo
 
Mwandishi wa habari hii akipita katika bonde lilikauka maji na akishuhudia kutoweka kwa mto uliokua ukitililisha maji kwa msimu wote ukiwa umekauka

                                                    HABARI KAMILI

Kampuni ya pembejeo Tanzania Seed co LTD imezindua rasmi shindano la shama darasa katika shule za msingi, ambapo shule itakayokua imelima shamaba zuri kwa kuzingatia misingi yote ya kilimo bora cha kisasa itajishindia zawadi kubwa ya madawati miamoja yenye thamani ya milioni kimi na tano.

Akiongea katika mkutano na waandishi wahabari uliofanyika katika ukumbiwa mtenda jijini Mbeya MICHAEL RIKANGA kaimu mkurugenzi wa kampuni hiyo amesema lengo la shindano hilo ni kutaka kuisaidia jamii na kuiunga mkono serikal kauli mbiu yake kua uti wa mgongo wa Tanzania ni kilimo.

“Tumeona ni vema tuhamasishe kilimo bora huku chini kabisa katika shule za msingi kwakua kumekua na elimu mbalimblia zinazo pita kwa jamii ambayo haziwagusi wananchi wa chini hivyo kama kampuni imeamua kuanzisha shindano hili kwa shule za msingi ili wanapomaliza kidato cha nne wawe na uelewa wa kilimo kwakua wengi hurudi kuwa saidia wazazi kazi za kilimo” amesema Rikanga

Ameongeza kua pamoja na vijana waliopo vijijini kuendelea na shughuli za kilimo basi ni viema wakajifunza kilimo bora  na cha kisasa ambacho watakua wamejinifunza katika mashamaba darasa yaliyopo mashuleni, Hivyo kukuza kilimo cha Tanzania kwa kutumia pembejeo zilizo bora na kuongeza kipata kwa jamii

Katika mkutano huo Rikanga ametambulisha mbegu mpya aina ya chapa tembo yenye ubora mkubwana ambayo katika hekali moja ukilima kwa kufuata kilimo cha kisasa mkulima anauwezo wa kuvuna zaidi ya magunia albaini na amewataka wananchi kuzitumia mbegu hizo ambazo zimefanyiwa utafiti na maraka husika.

Kwa upande wa mwalimu wa shule ya msingi  Nsoho Rugano kajisi iliyopo nje ya jiji la Mbeya amesema shindano hilo ni zuri na wanalipokea kwa moyo mkubwa japo habari hizi hawajazipata na wala hawajui kama kunashindano la aina hiyo lakini wakipata nafasi ya kushiliki watajitahi kufanya vizuri kwani zawadi ya madawadi 100 yataisaidia shule yao.

“Ukweli ni kwamba sisi kama shule ya msingi Nsoho hatujasikia kama kuna shindano la aina hiyo endapo tukipata nafasi ya kushiriki tutajitahi kufanya vizuri na kujishindia hayo madawati 100 kwa kua mashamba tunayo lakini hatuyalimi zaidi tunawakodishaia wanakijiji tukiingia katika shindano hilo tutayalima sisi wenyewe” amesema Kajisi

Ameongeza kua shule haina miradi ya kuingizia kipato kikubwa endapo watapata elimu ya kilimo cha kisasa itawasaidia kuanzisha mradi wa kilimo na kuisaidia shule kuongeza kipato, kwani mpaka sasa wanategemea miti iliyo pandwa kizunguka shule hiyo kama mradi wa kuwapatia kipato.

Pamoja na kuwa na mradi hua bado ameulaumu kwakua miti iliyo panda imekua ikinyonya maji kwa wingi ambapo inaweza kusababisha ukame kwani mpaka sasa chini ya shule hiyo kuna mto wa maji ulikua ukitililisha maji kwa mda wote kwa sasa umekauka kutokana na msitu uliopandwa karibu yake.

Kwa upande wa wanafunzi wa shule hiyo walipta nafasi ya kuhojiwa na mwandishi wa habari hizi wamefurahishwa sana na shindano hilo na kuahidi kushiriki kwa nguvu zote ili kujinyakulia zawadi hiyo kwani wamekua na uhaba mkubwa wa madwati katika shule yao hivyo hiyo wanaiona ni fulsa ya kujikwamua na tatizo la muda mlefu.

Shindano hilo litaanza haraka iwezekanavyo katika msimu huu wa kilimo wa mwaka 2041-2015 na kwa habari zaidi za shindano hili zinapatika katika gazeti la nipashe.