Pages

Ads 468x60px

Wednesday, December 31, 2014

JUST IN: MTUHUMIWA ALIYEJARIBU KUTOROKA MAHAKAMA YA KISUTU APIGWA RISASI


Muonekano wa mahabusu aliyekuwa anatuhumiwa kubeba madawa ya kulevya, Abdul Koroma raia wa Sierra Leone baada ya kupigwa risasi.
Koroma akiwa  kwenye machela tayari kwa kupelekwa kuifadhiwa hospitalini.
MAHABUSU aliyekuwa anatuhumiwa kubeba madawa ya kulevya, Abdul Koroma raia wa Sierra Leone ameuawa kwa kupigwa risasi na Askari Magereza wakati akijaribu kutoroka katika eneo la Mahakama ya Kisutu jijini Dar leo!

Mtuhumiwa wa madawa ya kulevya raia wa Sierra Leone akiwa amepigwa risasi baada ya kutaka kuwatoroka askari magereza katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.









Mtuhumiwa wa madawa ya kulevya raia wa Sierra Leone akiwa amepigwa risasi baada ya kutaka kuwatoroka askari magereza katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
Mtuhumiwa wa madawa ya kulevya raia wa Sierra Leone akiwa amepigwa risasi baada ya kutaka kuwatoroka askari magereza katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win

Monday, December 29, 2014

FERI YA ABIRIA 460 YASHIKA MOTO



Amri imetolewa ya kuwataka abiria kuondolewa kwa ferry iliyo na karibu abiria 460 ambayo ilishika moto ilipokuwa safarini kutoka nchini Ugiriki kwenda Italia.
Abiria waliokuwa kwenye ferry hiyo walipiga simu kwa vituo vya runinga nchini Ugiriki wakisema kuwa mawimbi makali na upepo unatatiza shughuli za uokoaji.
Maafisa wa ulinzi wa pwani nchini Ugiriki wamesema kuwa ferry hiyo ya Norman Atlantic ilikuwa umbali wa kilomita 30 kutoka kisiwa cha Othonoi wakati walipotuma ujumbe .
Vyombo vya habari nchini Italia vinasema kuwa moto ulianzia kwenye eneo la kuegesha magari

Ndege ya AirAsia yapotea na abiria 160

Shirika la ndege la AirAsia linasema kuwa limeanzisha shughuli ya kuitafuta ndege yake iliyopoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za ndege dakika 45 baada ya kuondoka kwenye mji wa Surabaya nchini Indonesia.
Zadi ya watu 160 walikuwa ndani ya ndege hiyo ya Airbus 320 iliyokuwa safarini kwenda nchini Singapore.
Wengi wa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo wanatoka nchini Indonesia.
Msemaji wa wizara ya usafiri nchini Indonesia amesema mawasiliano yalipotea kati ya visiwa vya Kalimantan na Java.
Wataalamu wa safari za ndege wanasema kuwa huenda ndege hiyo iliishiwa na mafuta

TASWIRA MBALI MBALI KATIKA MTANANGE KATI YA YANGA NA AZAM FC UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR LEO


 Kikosi cha timu ya Azam FC kilichoanza mechi ya leo.
 Kikosi cha timu ya Yanga.
 Wachezaji wa timu ya Azam FC wakishangilia goli yao la kwanza dhidi ya Yanga.
 Mshambuliaji wa Yanga,Hamis Tambwe akiipatia timu yake bao la kusawazisha katika mtanange wa muendelezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam leo.Picha zote na Othman Michuzi.
 Mfungaji wa goli la kwanza kwa timu ya Yanga,Hamis Tambwe na Mfungaji wa Bao la pili,Simon Msuva wakishangia ushindi wao dhidi ya timu ya Azam katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam hivi sasa.
 Shangwe kwa Yanga.
 Beki wa timu ya Azam, Pascal Wawa akimdhibiti Mshambuliaji wa Yanga,Hamis Tambwe katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.
 Benchi la ufundi la Yanga.
 Makocha wakifatilia timu zao.
 Mchezaji wa Yanga,Kpah Sherman akitoa pasi mbele ya mabeki wa Azam.
 Beki wa kushoto wa Azam FC,Shomary Kapombe akiangalia namna ya kumdhibiti Simon Msuva wa Yanga.
 Kapombe na Msuva......
 Danny Mrwanda akipokea pasi mbele ya Beki wa Azam,Aggrey Morris.
 Kiumbo mshambuliaji wa Yanga,Haroun Nyionzima akiruka daluga mardadi mbele ya mabeki wa Azam.
 Nyomi la Yanga.
 Mashabiki wa Azam wakishangilia Goli lao la kusawazisha.
 Mrwanda akimtoka Beki wa Azam.

Tuesday, December 23, 2014

Escrow yamfukuzisha kazi Profesa Tibaijuka, Muhongo awekwa kiporo

JK AMNG'OA UWAZIRI PROFESA ANNA TIBAIJUKA SAKATA LA AKAUNTI YA ESCROW Mh.Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na taifa kupitia Wazee wa Dar es Salaam leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadik na kulia ni katibu wa Baraza la wazee wa Dar es Salaam Abdul Mtulia.Rais alizungumzia sauala ya vurugu katika uchaguzi wa Srikali za Mitaa na kuagiza vyombo vya kuwachukulia hatua za kisheria. Vilevile alifafanua kuhusu sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow na kuchukua uamuzi wa kumng'oa aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na kumuweka kiporo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. Baadhi ya mawaziri wakisikiliza kwa makini hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, ambapo alifafanua kuhusu sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow na kutangaza kumg'oa uwaziri aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na kumuweka kiporo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. Baadhi ya wazee na wananchi wakimsikiliza kwa makini Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokuwa akilihutubia taifa kupitia wazee wa Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo Wazee wa Wilaya ya Temeke wakiwa katika mkutano huo Sehemu ya umati wa wananchi wakiwa kwenye mkutano huo Baadhi ya viongozi wa dini wakiwa katika mkutano huo.

Copy and WIN : http://bit.ly/copy_win
Rais wa Jamhuri wa Tanzania Jakaya Kikwete ametangaza kutengua uteuzi wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka baada ya vyombo vya Serikali kubaini na kijiridhisha kuwa amekiuka maadili ya utumishi wa Umma kwa kuingiziwa fedha kiasi cha Sh1.65bilioni kwenye akaunti yake binafsi.
Rais kikwete ametangaza kufukuzwa kazi kwa Waziri huyo leo alipokuwa anazungumza na wazee wa mkoa wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini hapa, na baada ya kutangaza kufukuzwa kwake maelfu ya wazee waliohudhuria kwenye mkutano huo walipiga kelele za kumpongeza Rais Kikwete kwa uamuzi wake.(MM)
Rais kikwete amesema miongoni mwa mapendekezo ya Bunge kuhusiana na sakata la uchotwaji wa fedha kwenye akaunti ya Escrow Tegeta yaliyofikishwa kwenye Serikali ni pamoja na kuwajibishwa kwa Bodi ya Shirika la umeme (Tanesco), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka, pamoja na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
Rais Kikwete amesema baada ya uchunguzi wa vyombo husika viliweza kubaini kuwa kiasi cha Sh1.65bilioni kiliingizwa kwenye akaunti binafsi ya Profesa Tibaijuka, jambo ambalo ni kinyume na maadili ya utumishi wa Umma.
"Tumezungumza na Profesa Tibaijuka na tumemuomba atupishe ili tuweze kuteua waziri mwingine kwani viashiri vyote vinaonyesha kuwa alikiuka kanuni na sheria ya maadili ya Umma," anasema Rais Kikwete.
Aidha Rais Kikwete amesema katika suala la Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo analiweka kiporo maana bado hajapata ufafanuzi kuhusu mambo kadha wa kadha, hivyo pindi atakapopata ufafanuzi na kujiridhisha ataujulisha umma .
Amesema kuhusu suala la bodi ya Tanesco hana shida nalo kwa sababu tayari bodi hiyo imeshamaliza muda wake hivyo ni kama imekwishajifuta yenyewe, na kuongeza kuwa tayari Ikulu imeshapewa taarifa za kumtaka achague bodi nyingine, hivyo ndani ya siku chache bodi mpya ya Tanesco itatangazwa.
Amesema suala la Katibu Mkuu wa Nishati na Madini na viongozi wengine wa utumishi wa Umma ambao wametajwa katika sakata hilo tume ya maadili, Taasisi ya Kuzuia na Kupapambana Rushwa (Takukuru) pamoja na jeshi la polisi wanaendelea kufanya uchunguzi wao, na ikithibitika kuwa walikiuka maadili yao ya kazi sheria stahiki zitachukuliwa.

Wednesday, December 10, 2014

SHEREHE MIAKA 53 YA UHURU ZILIVYOFANA DAR ES SALAAM




Rais Kikwete akiwa kwenye sherehe hizo.

Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara CCM, Philip Mangula.(P.T)

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akisalimiana na Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick, akisalimiana na waziri mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.

Baadhi ya viongozi wa nchi wakiwa jukwaa kuu.


Askari wa majeshi ya ulinzi na usalama wakitoa heshima kwa Rais Kikwete.

Haya ni maonyesho ya halaiki.

Baadhi ya wananchi waliofika kwenye sherehe hizo.
RAIS Kikwete leo ameongoza sherehe za kuadhimisha miaka 53 tangu Tanzania Bara ipate uhuru wake Desemba 9 1961. Hafla hiyo ilifanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali nchini na wawakilishi wa nchi za nje walioshuhudia burudani ya kwaya, gwaride, halaiki, ngoma za asili, sarakasi na michezo mingineyo kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.
(Habari/Picha: Gabriel Ng’osha/GPL)