Mwenyekiti
wa soko la Soweto jijini Mbeya ONOLA MBOGERA miaka (36) amefikishwa mahakamani
kwa tuhuma za kushawishi wafanya biashara wa soko hilo kugoma kulipa ushuru.
Akiongea
mmoja wa wafanya biashara hao Emani kaloti amesema wamefikia uwamuzi huo
kutokana na halmashauri ya jiji kushindwa kuwatimizia maombi yao, ikiwepo
kufanya usafi katika soko hilo
pamoja na ubovu wa miundombinu japo wao huto
ushuru huo kila siku.
Kwaupande
wake mkurugenzi wa halmashauri hiyo MUSA ZUNGIZA amekili kuwepo kwa tukio hilo
lakini amesema wamekaa na viongozi wao na kufikia muafaka kisha kufuta kesi
mahakamani.
Mwenyekiti wa soko la soweto ONELA MBOGERA akisubili dhamana katika mahakama ya mwanzo Mbeya mjini
Baadhi ya wafanya biashara wakiwa eneo la mahakama akisubilia hatima ya mwenyekiti wao
Mwenyekiti wa masoko mkoani Mbeya Charles syonga akiongea na wafanya biashara juu ya makubaliano waliyofikia na Halmashauri ya jiji
Wafanya biashara wakisikiliza kwa makini makubaliano ya viongozi wao