Pages

Ads 468x60px

Wednesday, April 29, 2015

Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete azindua Meli Vita za Jeshi la Wanamaji

1
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa amri kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015
2
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua mara baada ya kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015
3 4
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na makamanda wa meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015
5
Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Chifu Edward Wanzagi wa kabila la Wazanaki (kati) pamoja na Mbunge wa Afrika Mashariki Mhe Makongoro Nyerere baada ya kuzindua rasmi meli vita mbili za doria bahari kuu TNS Msoga na TNS Mwitongo kwenye sherehe zilizofanyika Kamandi ya Jeshi la Maji Kigamboni jijini Dar es salaam leo April 28, 2015
PICHA NA IKULU

Watu wenye ulemavu wa kusikia Viziwi waipongeza Benki ya CRDB



Watu wenye ulemavu wa kusikia yaani Viziwi wameupongeza uongozi wa Benki ya CRDB mkoa wa Mbeya kwa  kuwapatia elimu ya ufunguaji  na utunzaji wa pesa katika akaunti za Benki.
 Shukrani hizo zimetolewa  na mwenyekiti wa Viziwi mkoan hapa TUSSA MWALWEGA alipokua akiongea katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki hiyo katika ukumbi wa  Youth Center.
Tussa Mwalwega

“Kumekuwepo na dhana potofu kwa jamii ya watanzania kwamba sisi watu wanye ulemavu wa kusikia tupo tofauti na wengine na kwamba yapo mambo ambayo haya tuhusu kitu ambacho si kweli sisi ni sawa na watu wengine na tunastahili kuchukuliwa kama hao kwani ulemavu hatukupenda kuwanao i ila tunaushukuru uongozi wa benki hii kwa namna ambavyo wamekubali  na kuona umuhumu wa kutoa elimu hii kwetu”  amesema Mwalwega.

Kwa upande wake STEPHAN MWAIPOPO ambaye alikuwa mkufunzi wa semina hiyo amewataka walemavu hao kujitokeza kwa wingi katika kufungua akaunti katika benki hiyo .

Mwaipopo amesema kuwa watawapunguzia gharama za kufungua   kutoka elfu ishilini hadi elfu kumi tu, kwa kuw a kunafaida nyingi  ikiwepo utunzaji wa pesa zao pamoja na mikopo midogo yenye riba nafuu itakayowawezesha kuendeleza  biashara zao ndogondogo zitakazo wafanya wajikwamue kiuchumi.

Naye meneja wa benki hiyo BENSON FRED amesema zoezi hilo lilikua gumu kutokana kushindwa kuelewana kutokana na kutokua na uelewa wa lugha ya alama ambayo wanatumia walemavu hao  lakini kwa sasa wamepata mtu mwenye ujuzi wa kutafsili lugha hiyo iameahidi kuendesha semina hiyo kwa wilaya zote za mkoa wa Mbeya ili kuwahamsisha kufungua akaunti katika benki yeke.

Meneja wa Benki ya CRDG Benson Fred  mwenye koti jeusi katika akiongea na watu wenye ulemavu wa kusikia VIZIWI kwa kutafsiliwa na mtaalamu wa Rugha ya alama FARAJA MBWILO katika semina hiyo



Mkufunzi wa Semina STEPHAN MWAIPOPO kutoka CRDB aliepo kushoto akifundishwa na kutafsiliwa na mkalimani Faraja MBWILO






      Wanasemina kutoka wilaya mbalimbali za mkoa wa Mbeya wakiwa katika mafunzo
         Lupi Mwaisaka Afisa Jinsia CHAVITA makao makuu akiongea jambo katika semina
                                                                        Fadhili kwale

                                                              Isdory Mwashimaha
                                Tussa Mwalwega mwenyekiti wa CHAVITA Mkoa wa mbeya
                                                                       Gwantwa Mugha
                                                               Severin Lwenagira
                                                              Tunganege Jackson
                                     Washiliki wa semina wakiuliza maswali baada ya mafunzo


Monday, April 27, 2015

Wakuu wa wilaya ya Rungwe na Kyele wa watimua LHRC



Maafisa wa kituo cha haki za binadamu(LHRC)  watimuliwa na wakuu wa wilaya ya Rungwe na Kyela baada ya kushindwa kujibu maswali yenye utata,hayo yamebainishwa na ZAINABU MBUSSI mkuu wa wilaya ya Rungwe alipokua akiongea na mwandishi wa habari hizi kujibu tuhuma zilizotolewa kwake kuwafukuza maafisa hao katika wilaya yake.
William Kahale

“ niliwasimamisha kuendelea na zoezi la kuendesha mdahalo na wananchi wa wilaya yangu kutokana na wao kushindwa kujibu baadhi ya maswali yangu kitu ambacho kilinitia shaka juu ya elimu wanayotaka kuipeleka kwa Wananchi wa Rungwe huenda haitakuwa sahihi.

Mwassa Jingi

Hali hiyo imejitokeza baada ya mmoja wa maafisa hao WILLIAM KAHALE katika mkutano na waandishi wa habari mkoa wa Mbeya uliofanyika katika ofisi za Mbeya Press Club zilizopo Soweto jijini hapa na kutoa shutuma kwa wakuu wa wilaya hao kuzuia kufanya midaharo ya katiba pendekezwa katika wilaya zao bila kupewa sababu za msingi.

“Nataka kuongea changamoto ambazo tumekutana nazo katika wilaya mbili katika utoaji wa elimu ya katiba mpya kwa niaba ya Tume ya uchaguzi kwa mujibu wa sheria kama tulivyopewa mamlaka kinyume na katiba ya jamhuri ya Tanzania ibara ya 18 na 21 ibara ndogo ya pili kwa kua tumepewa huo uhuru, Sheria ya kura ya maoni imeikaribisha Tume kutoa elimu ya uraia Tume imetupa majukumu asasi za kiraia kutoa  elimu kwa niaba yake, wametuzia kwa makusudi na kuvunja sheria
ya uchaguzi” amesema KIHALE
 
Awali Katika hali ya mchakato wa kuunda katiba mpya Sheria ya kura ya maoni  imeipa mamlaka Tume ya uchaguzi  kukaribisha Asasi za kiraia kutoa elimu ya uraia na kuziruhusu asasi za kiraia zaidi ya miatatu (300)  kutoa  elimu hiyo kikiwepo kituo cha sheria na haki za binadamu

                    Grace Mgonja Constitutional Trainer Sociologist (LHRC) akiongea na waandishi wa habari




                               Baadhi ya wananchi wa habari wakisikiliza kwa makini ndani ya mkutano huo.

                            Vailety Jailo kutoka Sweety Fm Radio akiongea jambo katika mkutano

Monday, April 20, 2015

TANGAZO KWA MABLOGER WA MBEYA


Haruna mwanauta awaza kutia nia ya kugombea ubunge na kumrithi Victor Mwambalaswa Chunya kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)



Imeelezwa kuwa  wilaya ya Chunya  ina rasilimali nyingi ambazo zinaweza kuwaondoa wananchi wake kwenye umaskini  pia kuifanya  wilaya hiyo kuwa tajiri  na kuwa nufaisha wananchi  wake.
 Hayo yamebainishwa na HARUNA MWANAUTA  ambaye ni mfanya biashara mkubwa katika sekta ya utarii na uwindaji wa wanyama poli katika kitalu cha Rungwa mwamagembe kilichopo  Lupa wilayani humo.

Mwanauta ameyasema  hayo wakati akizungumza na mwandishi wa habari  kuwa wilaya hiyo inayo dhahabu nyingi na wachimbaji wakubwa ambao wanaweza kuinufisha kwa kodi zao na pia kuwaunganisha wachimbaji wadogo ili waweze kukopesheka na  kununua vifaa vya kuchimbia  
HARUNA MWANAUTA
madini

Amesema swala la wilaya hiyo pamoja na wananchi wake kuitwa masikini yeye anapingana nalo,  nakumesema kuwa nikuwakosea wananchi wake  kwani  wanayo migodi ya Dahabu pamoja na kilimo cha Tumbaku ambacho kinaweza kuwa kwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini uliokithili .

 “Chunya inahitaji kiongozi mwenye ushirikiano na  wananchi katika kuwajengea uwezo wa kujikwamua katika umasikini uliopo , Kwani imegawanyika katika makundi mawili makuu kiuchumi ikiwepo Dhahabu na kilimo cha Tumbaku lazima apatikane kiongozi atakae wezesha sekta hizi mbili ziwanufaishe wananchi wa chunya” amesema Mwanauta.

 chunya ina ardhi yenye Rutuba inayo kubali kilimo cha aina yoyote, wananchi  waatumie  maafisa ugani kulima kilimo chenye tija na kutumia fursa ya uwanja wa Ndege wa songwe kuuza nje ya nchi mazao yao
  
Aidha  mwanauta amekua akiiangalia wilaya hiyo kwa mtazamo wakipekee na kuona fursa iliyo nayo ya dhahabu pamoja na kilimo kinaweza kuwanufaisha  kisha kuondokana dhana iliyo jengeka kwamba wilaya hiyo ni masikini pamoja na wakazi wake,  ameamua  kujitosa  kugombe nafasi ya ubunge muda utakapofika na kumrithi Victor Mwambalaswa aliyepo sasa

Nyalandu amaliza mgogoro Mbarali



WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amemaliza mgogoro wa ardhi uliodumu karibu miaka 10 wilayani Mbarali, mkoani Mbeya.
Mgogoro huo unahusisha wakazi wa vijiji 21 waliotakiwa kuondolewa kwa madai ya kuvamia eneo la Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Nyalandu, ambaye yuko ziarani mkoani Mbeya, jana alizungumza na wananchi na kuwahakikishia
Waziri Lazaro Nyarandu
kuwa Serikali haiwezi kuwaacha wakiangamia.
Akizungumza katika mkutano na  waandashi wa habari uliofanyika katika hotel ya Hill View jijini hapa alisema wananchi wanaoishi vijiji hivyo hawatahamishwa.

Alisema uamuzi huo ni utekelezaji wa maelekezo ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kuitaka Serikali kuhakikisha inamaliza mgogoro huo.
Alisema kwa muda mrefu mgogoro huo umekuwa ukitafutiwa ufumbuzi wa kudumu na umefika wakati ni lazima mambo yafikie mwisho ili wananchi waendelee na shughuli zao za maendeleo.

“Naomba niseme kuwa vijiji vinavyotakiwa kuhama vitaendelea kuwepo na ninaagiza kufanyika kwa ukaguzi wa mpaka katika GN 28 ili kuhakikisha haki inatendeka katika suala hili. Huu mgogoro ni lazima ufike mwisho na uamuzi huu una baraka zote za Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,” alisema Nyalandu.
 
Alisema maeneo yenye mgogoro mengi ndiyo kilimbilio na uchumi wa wananchi wa Mbarali kutokana na kuendesha shughuli za kilimo na makazi, hivyo Serikali haiwezi kuchukua uamuzi utakaokuwa na madhara kwa wananchi wake.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbarali, Mathayo Mwangomo, alisema mgogoro huo umeleta mpasuko mkubwa na kusababisha wananchi kukosa imani na baadhi ya viongozi.
 
Naye, Mbunge wa Mbarali, Modestus Kilufi, alisema mgogoro huo umedumu kwa miaka mingi na ilikuwa ni lazima mwafaka ufikiwe ili kuleta amani na utulivu ulioanza kutoweka.





     Waziri Lazao Nyarandu akiongea na baadhi ya Waandishi wa Habari Hill view Hateli jijini Mbeya