Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abass kandoro amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi
kujiandikisha kwenye dafutali la
kudumu la mpiga kura kwani Vitambulisho vya awali
havitumika kupiga kura kwenye
uchaguzi unatarajiwa kufanyika octoba
mwaka huu
|
Abass kandoro |
Kandoro amesema hayo katika maadhimisho ya sikuuu ya
wafanyakazi iliyofanyika katika uwanja wa kumbukumbu wa hayati sokoine jijini hapa
amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika
kujiandikisha katika dafaftali la kudumu la mpiga kura utakapo fika ili kupati
haki na sifa ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika October
mwaka huu.
“Ninatoa wito kwa wafanyakazi wote na wananchi waliofikisha
umri wa kupiga kura wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika daftali la kudumu
la mpiga kura ili upate haki ya kupiga
kura ya kumpata Diwani, Mbunge hatimae Raisi unaemtaka, na lazima ujiandikishe
kwani uchaguzi ujao utatumia vitambulisho vipya vile vya zamani havitatumika”
amesema Kandoro
Ameongeza kuwa wananchi wanatakiwa kutunza amani katika mchakato wote unaopelekea
uchaguzi ili upite salama na kuvuka tukiwa salama bila kuingia katika machafuko
na vita vitakavyo sababisha kushindwa kufanya shughuli za maendeleo ya wananchi
na taifa kwa ujumla.
Aidha kandoro amesema wananchi kwa kushirikiana na wafanyakazi kwa pamoja wapige vita udini ukabila kwani ni
moja ya sababu zinzopelekea machafuko mahali
popote duniani.
|
Tabia Mwanjotile |
Akisoma Risala kwa mgeni Rasmi Tabia Mwanjotile ameiomba Serikali kutazama upya ukusanyaji
kodi kwa wafanya kazi kwakuwa umekuwa ni mzigo mkubwa ikiwepo makato mbalimbil
ya mifuko ya kijamii na mikopo na hivyo
kuwafanya waishi mazingira magumu na
kushindwa kumudu gharama za kuendesha maisha .
Akizungumzia swala
upandaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo umeme,majina na ges mwanjotile amesema vimekuwa vikipanada kila mara bila kuangalia
kipato cha mfanyakazi wa kima cha chini na hivyo
kuendelea kumdidimiza mfanyakazi.
Zegge Pilipili mwaenyekiti TUCTA Mkoa wa Mbeya akimkaribisha mgeni Rasmi uhutubia Wafanyakazi
Viongozi mbalimbali wa TUCTA
Mwanafunzi wa Chuo kikuu Teku Aliejiite kwa jina la madodoso akiongea utenzi wenye ujumbe wa siku ya wafanyakazi.
Kundi la Lizombe likitoa burudan
Baadhi ya viongozi na wafanyakazi walifika katika madhisho
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiendelea na majukumu ya kihabari
Taasisi na makampuni mbalimbali yalpata fulsa ya kuonesha shughuli zao mbele ya mgeni Rasmi