Pages

Ads 468x60px

Monday, July 13, 2015

MWANDISHI WA HABARI KALULUNGA AJITOSA MBIO ZA UBUNGE MBEYA VIJIJINI

Mwandishi wa Habari, Gordon Kalulunga akizungumza katika viwanja vya mahubiri alipokuwa akitangaza nia ya kugombea Ubunge jimbo la Mbeya vijijini.
Kalulunga akitaja vipaumbele vyake
Katibu wa Umoja wa Vijana Wilaya ya  Mbeya vijijini, Siulanga  akiwaasa Vijana kumuunga mkono kijana mwenzao.
Kalulunga akisalimiana na mmoja wa wazee waliojitokeza kumsikiliza alipokua akitangaza nia
Baadhi ya wanachama wapya wakikabidhiwa Kadi
Vijana wakiserebuka
Burudani zikiendelea
Wananchi wakimsikiliza Kalulunga

MWANDISHI wa habari wa gazeti la Mtanzania kutoka Mbeya, Gordon Kalulunga amejitosa kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Ubunge katika Jimbo la Mbeya vijijini kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi(CCM).
Kalulunga alitangaza kuingia kwenye mchakato wa kugombea kuteuliwa na Chama ili aweze kupeperusha bendara katika uchaguzi mkuu ujao katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jana kwenye viwanja vya mahubiri Mbalizi mkoani Mbeya.
Mtia nia huyo alisema endapo Chama chake kitampitisha na hatimaye kushinda Ubunge katika Jimbo hilo atahakikisha wananchi wote wanajiunga na mfuko wa bima ya afya kwa ajili ya matibabu kwa kila kaya kuchangia ili kupunguza adha na gharama kubwa za matibabu.
Aliongeza kuwa akifaniiwa kuukwaa Ubunge pia atasimamia kuhakikisha Jimbo hilo linapata Chuo cha aina yoyote kikiwemo Chuo cha ufundi kwa ajili ya vijana kupata elimu jambo lilatalopunguza wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana.
Kalulunga alisema kipaumbele kingine atakachoshughulikia ni pamoja na kupigania ujenzi wa ofisi za makao makuu ya Wilaya hiyo katika eneo husika ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi tofauti na ilivyosasa ambapo Ofisi za Wilaya ya Mbeya zipo katikati ya Jiji la Mbeya.
Awali Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Mbeya vijijini, Japheti Siulanga aliwataka vijana wote kuungana ili kumuunga mkono kijana mwenzao aliyejitokeza na kuonesha nia ya kutaka kuongoza akiwa Mbunge wa jimbo hilo.
Aidha katika mkutano huo vijana zaidi ya 26 walijiunga na Chama cha mapinduzi na kukabidhiwa kadi za umoja wa Vijana.

Habari na Mbeya yetu:

MAJAMBAZI YATIKISA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM LEO MCHANA YATIWA MBARONI


 Picha ya 1-2 ni mmoja wa watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi akiwa mikononi mwa polisi baada ya kutiwa mbaroni Mnara wa Saa maeneo ya Stesheni Dar es Salaam leo mchana kwa madai ya kupora kiasi kikubwa cha fedha. Watu hao wanadaiwa kuwa walikuwa wanne.


 Kijana mwingine anayedaiwa kuwa ni jambazi akiwa amekamatwa.
 Watuhumiwa hao wanne wa  ujambazi  wakiwa ndani ya Noah kabla ya kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi. Kulia ni askari Polisi.
 Askari kanzu (katikati), ndiye anadaiwa kuwadhibiti majambazi hayo kabla ya kujificha chini ya uvungu wa taxi zinazoegeshwa jirani na Mnara wa Saa katika makutano ya barabara ya Uhuru, Samora na Nkruma.
 Gari lenye namba T 976 BKK walilokuwa wakitumia majambazi hayo liondolewa eneo la tukio kupelekwa kituo kikuu cha polisi.
 Wananchi wakiwa eneo la tukio.
 Askari Polisi wakilipekua gari walilokuwa wakitumia watu hao wanaodaiwa kuwa ni majambazi.
 Upekuzi ukiendelea.
Maofisa wa polisi wakiteta jambo eneo la tukio baada ya kuwakamata majambazi hayo. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com)