Pages

Ads 468x60px

Tuesday, September 22, 2015

MABASI 138 YA BRT YATUA DAR




Sehemu ya mabasi 138 ya Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) yaliyowasili katika Bandari ya Dar es Salaam, kwa ajili ya kuanza kutoa huduma ya usafiri katika kipindi cha mpito kwenye miundombino ya mfumo wa mabasi yaendayo haraka (BRT)kuanzaia mwezi ujao.

Mkuu wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki akijaribu basi la Mradi wa Mbasi Yaendayo Haraka (DART), alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam kujionea kuwasili kwa Mabasi 138 ya Mradi huo ambayo mwezi ujao yataanza kutoa huduma ya usafiri jijini Dar es Salaam katika Kipindi cha mpito.(P.T)

Mkuu wa Mkowa Dar es Salaam, Bw. Saidi Meck Sadiki akishuka katika basi la Mradi wa Mbasi Yaendayo Haraka (DART), alipofanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam kujionea kuwasili kwa Mabasi 138 ya Mradi huo ambayo mwezi ujao yataanza kutoa huduma ya usafiri jijini Dar es Salaam katika kipindi cha mpito.Mabasi 138 ya Mwendo Kasi (BRT), yamewasili katika Bandari ya Dar es Salaam kutoka nchini China. Kuwasili kwa mabasi hayo kutasaidia kupunguza tatizo la usafiri katika Jiji la Dar es Salaam. 

Katika Bandari ya Dar es Salaam kutoka China tayari kwa huduma ya usafiri. Mkuu wa Mkoa  wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, aliwaambia waandishi wa habari jana baada ya kufanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam kujionea kuwasili kwa mabasi hayo.

“Tumefikia hatua nzuri na naipongeza Kampuni ya Uda Rapid Transit (Uda-RT) kwa kuleta mabasi hayo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma hii ya usafiri katika kipindi cha mpito. Hii itasaidia kuondoa adha ya usafiri kwa wakazi wa jiji hili,” alisema.

Alisema serikali ilifanya kazi kubwa kuunganisha Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam na wamiliki wa daladala na baadaye kuanzisha kampuni ya Uda-RT.
Hata hivyo, alisema taarifa za nauli za mabasi hayo ya Sh.  900 zilizotolewa katika mtandano, zilikuwa ni uzushi na upotoshaji.

Alisema suala la nauli linahusisha ushiriki wa taasisi mbalimbali chini ya Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) na hivyo uzushi huo umewaletea usumbufu mkubwa wakazi wa Dar es Salaam hivyo wanatakiwa kuwapuuzia.

Msemaji wa Kampuni ya Uda-RT, Subri Maburuki, alisema mabasi yote yameingia yakiwamo ya mita 12 yapo 101 na mita 18 yapo 39 na huduma ya usafiri kipindi cha mpito kitaanza baada ya kukamilisha taratibu za bandari.
“Tuliahidi kuwa mwezi huu mabasi yatakuwa yamewasili na ni kweli yamekuja, kwa pamoja na yale ya kufundishi yatakuwa mabasi 140,” alifafanua Maburuki. 

Kaimu Meneja Bandari ya Dar es Salaam, Hebel Mhanga, alisema meli iliyobeba mabasi hayo ilipitia Kenya na kimsingi kutokea nchini China, ilikuwa imebeba magari 1,700 yakiwamo mabasi ya Uda-RT.
CHANZO: NIPASHE

IBADA YA KUWEKWA WAKFU ASKOF PANJA WA KANISA LA MORAVIAN

Maaskofu mbalimbali wa wakiwa mwombea kwa kumpa baraka Askofu wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini mchungaji Kenan Panja kwenye ibada maalumu ya kuwekwa wakfu askofu huyo iliyofanyika jumapili mjini Tukuyu wilayani Rungwe.
 Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilali akisalimiana na maaskofu mara baada ya kuwasili uwanjani kwaajili ya ibada


Wachungaji mbalimbali wa kanisa la Moraviana Tanzania wakiwa katika ibada





 Mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Mchungaji Samwel Kabigi akisoma risala ya kanisa mbele ya mgeni rasmi makamu wa Rais Dk.Bilali.
 Kwaya ya  Shalom ikitumbuiza katika ibada hiyo maalumu mbelea ya makamu wa Rais Dk.Bilali.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akitoa salamu za mkoa kabla ya kumkaribisha makamu wa Rais Dk.Bilali
 Makamu wa rais Dk.Mohamed Gharib Bilali akimpongeza askofu Panja kwa kufikia daraja hilo la kiroho.Numa ya askofu na mkewe mama Panja.
 Makamu wa Rais Dk.Bilali akihutubia waumini na wadau mbalimbali waliohudhuria ibada hiyo ya kuwekwa wakfu kwa askofu Panja.
  Askofu Panja akitoa neno la Shukrani mara baada ya kuwekwa wakfu.
Habari na Lyamba lya mfipa Blog