Pages

Ads 468x60px

Monday, April 25, 2016

MAJAMBAZI MBEYA WATAKA KUMUAGA KAMANDA MSANGI

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi akionesha Bunduki SMG kwa waandishi wa Habari
           Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi akionge jambo kwa wana habari







            Wanahabari wakipata taarifa kwa kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi
                                          Mwandishi wa Habari Felix Mwakyembe akiuliza swali
Baada ya Taarifa Kamanda Msangi kulia amekabidhi ofisi kwa Rpc Mpya Justus Kamugisha
Rpc Mpya wa Mkoa wa Mbeya Justus Kamugisha akiongea jambo kwa wana habari baada ya kukabidhiwa ofisi
              Mrakibu mwandamizi wa Polis mpya Benjamini Kuzaga aksema neno kwa wanahabari

HABARI
MNAMO TAREHE 18.04.2016 MAJIRA YA SAA 03:00 USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA MALAMBO, KATA YA RUIWA, TARAFA YA ILONGO, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. WATU WANAOSADIKIWA KUWA MAJAMBAZI AMBAO IDADI YAO HAIKUWEZA KUFAHAMIKA MARA MOJA WALIFIKA NYUMBANI KWA GERVAS LAZARO [56] MFANYABIASHARA NA MKE WAKE AITWAE WITNESS MWAKALENGA [50] WOTE WAKAZI WA MALAMBO KWA LENGO LA KUFANYA UHALIFU WA KUJARIBU KUNYANG’ANYA KWA KUTUMIA SILAHA.

HATA HIVYO KUTOKANA NA KUWEPO KWA TAARIFA ZA SIRI KUHUSIANA NA NJAMA NA MPANGO HUO, ASKARI POLISI WALIKUWA TAYARI ENEO HILO LA TUKIO ILI KUWEZA KUKABILIANA NA MAJAMBAZI HAO.

KATIKA KUKABILIANA NA MAJAMBAZI HAO, BAADHI YA ASKARI WALIIMARISHA ULINZI ENEO HILO NA KUFANIKIWA KUPATA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.913 CGF AINA YA T-BETTER RANGI NYEKUNDU AMBAYO ILIKUWA IKITUMIWA NA MAJAMBAZI HAO. BAADA YA UCHUNGUZI PIKIPIKI HIYO ILIBAINIKA KUWA NA INJINI NAMBA ZJ16ZFNJC2512944 NA CHASSES  LZEPCKLASCL812905 AMBAYO ILITELEKEZWA NA MAJAMBAZI HAO BAADA YA KUONA POLISI WAMEDHIBITI ENEO HILO.

HATA HIVYO POLISI KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI WA ENEO HILO WALIENDELEA KUWAFUATILIA MAJAMBAZI HAO NA KUFANIKIWA KUPATA SILAHA MOJA AINA YA SMG NAMBA UA 2911997 PAMOJA NA RISASI 27 KWENYE MAGAZINE. AIDHA KATIKA ENEO HILO LA TUKIO AMBALO ILIKUTWA SILAHA HIYO PIA ILIKUTWA KOFIA MOJA YA KUFICHA SURA [MZURA] ILIYOTELEKEZWA NA MAJAMBAZI HAO KABLA YA KUKIMBILIA PORINI.

KWA SASA MSAKO /DORIA INAENDELEA MAENEO YA PORI LA NARCO LILILOPO KATI YA WILAYA YA MBARALI NA CHUNYA, AMBAPO KIKOSI KAZI CHA ASKARI WA WILAYA HIZO WAMEUNGANA ILI KUWASAKA MAJAMBAZI HAO KWA AJILI YA KUWAKAMATA. AIDHA TARATIBU ZIMEFANYWA ZA KUSHIRIKISHA VIONGOZI WA VIJIJI VILIVYOPO MAENEO JIRANI NA MSITU HUO ILI KUSAIDIANA KUWAPATA MAJAMBAZI HAO. 

MWISHO

0 comments:

Post a Comment