Pages

Ads 468x60px

Monday, April 25, 2016

RC MBEYA AMOS MAKALLA ALA CHAKULA NA WAFUNGWA GEREZANI










RC MBEYA ALA CHAKULA NA WAFUNGWA GEREZANI
MKUU wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla aibukia kwenye Gereza la Mahabusu la Ruanda lililopo Jijini Mbeya na kula chakula pamoja na wafungwa gerezani.
Pamoja na kula chakula na wafungwa Makalla pia alikagua malazi ya wafungwa pamoja na zahanati ambapo pia amewaahidi wafungwa na mahabusu kufuatilia tatizo la ucheleweshaji wa kesi kutokana na kisingizio kwa kuchelewa kwa majalada ya upelelezi.
Mbali na kutembelea wafungwa na mahabusu gerezani,Makalla ametekeleza ahadi yake ya kuitembelea timu ya Prison kama alivyofanya kwa timu ya Mbeya City na kukabidhiwa jezi ya timu hiyo na kutoa wito kwa timu zote za Prison na Mbeya City kuendelea kufanya vyema katika ligi Kuu ili ziendelee kutoa burudani kwa wakazi wa mkoa wa Mbeya msimu ujao.
 
Story na Mkwinda Blog

0 comments:

Post a Comment