

Sehemu ya umati wa watu waliofurika kwenye uwanja wa Lake Tanganyika usiku huu wakiburudika na Wasanii wa Serengeti Fiesta 2013

Burudani ya kutosha kabisa

Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Neylee akiimba kwa hisia kwenye jukwaa
la tamasha la Serengeti Fiesta 2013,usiku huu kwenu uwanja wa Lake
Tanganyika.

Hapatoshi ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika usiku huu.

Mwanamuziki mahiri wa muziki wa Dansi,Christian Bella akikamua jukwaani
usiku huu ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika,mkaoni Kigoma ambapo watu
wamefurika ile mbaya.


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Cassim Mganga akiimba jukwaani mbele ya
maelfu ya wakazi wa Kigoma ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika.

Sehemu ya umati wa watu waliofurika ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika usiku huu

Msaniii anekuja kwa kasi kwenye miondoko ya Hip Hop,Stamina akikamua
jukwaani usiku huu mbele ya maelfu ya wakazi wa mji wa Kigoma
waliojitokeza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta

Ni Shangwe tu ndani ya uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma usiku huu,wakati tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea

Yaani hapatoshi kabisa,wakazi wa Kigoma wamecharuka na burudani murua kabisa ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Rachael kutoka THT,akionesha umahiri
wake wa kutumbuiza jukwaani usiku kwenye tamasha la Serengeti Fiesta
2013.

Washabiki wa tamasha la Fiesta wakifuatilia kwa makini yanayojiri usiku huu ndani y uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Wadau nao wamejitokeza kwa wingi

Peter Msechu na densa wake wakikamua vilivyo usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.

0 comments:
Post a Comment