skip to main |
skip to sidebar
WAJUE BAADHI YA WANAWAKE AMBAO WAKO KATIKA MAMLAKA YA DUNIA KATIKA NCHI ZAO, NI VIONGOZI WANAOTIFUA KIVUMBI DUNIANI.
Joyce
Banda alichaguliwa kama Rais wa kwanza mwanamke Kusini mwa Afrika April
2012. Akawa rais wa Malawi alipomrithi mtangulizi wake aliyefariki
kutokana na mshtuko wa moyo.
Michelle Bachelet amechaguliwa kama Rais wa Chile kwa muhula wa pili na kumshinda mpinzani wake Evelyn Matthei kwa kura nyingi.
Rais
wa Liberia,Ellen Johnson Sirleaf, 72, alitajwa kama mmoja wa washindi
wa tuzo ya amani ya Nobel mwaka 2011. Alichaguliwa kama Rais wa kwanza
mwanamke barani Afrika mwaka 2005 miaka miwili baada ya kumalizika kwa
vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 14 Liberia.
Sheikh
Hasina alichaguliwa kwma waziri mkuu wa kwanza wa Bangladesh kwa muhula
wa pili mwezi Januari mwaka 2009. Lakini mwaka 2008 chama chake cha
Awami, kilipata ushindi mkubwa dhidi ya mpinzani wake Begum Khaleda Zia.
Korea
Kusini imemchagua rais wake wa kwanza mwanamke Park Geun-hye, kwenye
uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali Disemba mwaka 2012. Babake Park
Chung-hee alitawala nchi hiyo kwa miaka 18.
Waziri
mkuu wa Thailand, ingluck Shinawatra dadake mdogo waziri mkuu
aliyeondolewa mamlakani Thaksin Shinawatra, aliongoza chama chake cha
upinzani kuweza kushinda uchaguzi uliofanyika Julai 2011.
Helle
Thorning-Schmid alichaguliwa kama waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa
Denmark, baada ya chama chake kupata ushindi kwenye uchaguzi uliofanyika
Septemba mwaka 2011. Thorming alikosolewa hivi karibuni kwa kujipiga
picha na waziri mkuu wa Uingereza Cameron na Rais Barack Obama kwenye
ibada maalum ya hayati Mandela.
Dalia Grybauskaite alichaguliwa kama rais wa kwanza wa Lithuania katika uchaguzi mkuu wa Mei 2009. Alishinda kwa kura 69%.
Chansela
wa Ujerumani, Angela Merkel anajulikana kama kiongozi asiyekuwa na mbwe
mbwe nyingi na kusababisha watu kumuita..Mutti..mama wa taifa. Markel
anajiandaa kwa muhula wa tatu baada ya kushinda uchaguzi wa Septemba 22.
Rais
wa Argentina, Cristina Fernandez alishinda uchaguzi uliofanyika mwezi
Oktoba mwaka 2007 ushindi ambao wengi walisema ulitokana na umaarufu wa
mumewe aliyekuwa Rais Nestor Kirchner.
Rais
wa Brazil Dilma Rousseff alichaguliwa kama rais wa kwanza mwanamke
nchini Brazil alipochukua hatamu za uongozi kutoka kwa Luiz Inacio Lula
da Silva mwaka 2011. Alikuwa mkuu wa majeshi kabla ya kuteuliwa na
kumrithi Rais De Silva.
Kiongozi
wa upinzani nchini Jamaica, Portia Simpson-Miller alishinda uchaguzi
uliofanyika Disemba mwaka 2011 kwa idadi kubwa ya kura. Alikuwa waziri
mkuu wa Jamaica kabla ya kushindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2007.
Kamla
Persad-Bissessar alichaguliwa kama waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa
Trinidad and Tobago, wakati chama chake kilishinda uchaguzi kwa idadi
kubwa ya kura mwezi Mei mwaka 2010. CHANZO BBC.
0 comments:
Post a Comment