Mkurugenzi
wa Uzalishaji na Matengenezo TEMESA Mhandisi Silvester Simfukwe
(katikati walio chuchumaa) akiwaonesha Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya
Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) sehemu ya kivuko cha Magogoni
inayoendelea kufanyiwa ukarabati.
Kivuko cha Magogoni kikiwa katika ukarabati katika Bandari ya Dar es Salaam.
Na Theresia Mwami- TEMESA
Wajumbe
wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) imetembelea na
kujionea maendeleo ya ukarabati wa kivuko cha Mv Magogoni chini ya
kampuni ya Songoro Marine katika Bandari ya Dar es Salaam.
Akizungumza
katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Bodi hiyo Balozi Herbert Mrango
ameeleza kuridhishwa na kasi ya ukarabati wa kivuko hicho na kuushauri
uongozi wa TEMESA kuharakisha malipo yanafanyika kwa wakati ili
kukamilisha kazi hiyo ndani ya muda uliopangwa.
“Nakuagiza
Kaimu Mtendaji uhakikishe malipo kwa kampuni hii yanafanywa kwa wakati
na ukarabati huu kukamilika mapema ili kuwapa fursa wananchi kutumia
kivuko hiki”alisema Balozi Mrango.
Aliongeza
kuwa ni muhimu wananchi kurejeshewa huduma ya kivuko hicho ili kuondoa
kero inayowakabili kwa sasa kwa kuwa na kivuko kimoja chenye uwezo wa
kubeba magari ambapo kukamilika kwa ukarabati wa huu utakuwa umerahisiha
shughuli ya usafirishaji.
Kwa
upande wake Kaimu Mtendaji wa TEMESA Mhandisi Manase Ole kujan amesema
atahakikisha malipo yanafanyika kwa wakati ili kuwezesha mkandarasi huyo
kumaliza kazi hiyo kwa muda uliopangwa na kurejesha huduma ya kivuko
hicho kwa wananchi.
Aidha
aliongeza kuwa kazi ya ukarabati wa kivuko hicho imegawanywa katika
sehemu mbili ambazo ni, ukarabati wa “Body” pamoja na mifumo ya umeme
unaofanywa na Mkandarasi kutoka kampuni ya Songoro Marine huku TEMESA
ikihusika na ukarabati wa mitambo ya kuongozea kivuko.
Kivuko
cha Mv Magogoni kinachotoa huduma katika maeneo ya kigamboni na
Magogoni Jijini Dar es Salaam kilisimamisha rasmi kutoa huduma hiyo
mapema Mei mwaka huu kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati mkubwa chini ya
Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na kampuni ya Songoro Marine
kukiongezea ufanisi katika kutoa huduma ya usafiri kwa wananchi.
0 comments:
Post a Comment