Mbunge
wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akichangia Bajeti ya Serikai
katika Mpango pili wa wa miaka mitano ijayo wakati wa vikao vya bunge
la bajeti linaloendelea mjini Dodoma hivi karibuni.
Mbunge
wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akiendelea na uchangiaji wa hoja
katika Mpango huo wa pili wa Maendeleo wa miaka mitano ijayo.
Mbunge wa jimbo la Mkuranga Mh. Abdallah Ulega akizindua kisima cha maji Mkamba katika jimbo lake la Mkuranga mkoani Pwani.
......
SERIKALI ya
awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt.John Magufuli imedhamiria kuwa
Serikali ya mageuzi ya Viwanda ukilinganisha na zilizotangulia.
Rais
Dkt.Magufuli hata katika kampeni zake za uchaguzi 2015 wakati akipita
kuomba kura alisisitiza dhamira ya Serikali ya kujenga uchumi wa
Viwanda.
Wakati
Serikali ikisisitiza kujenga uchumi wa Viwanda huku ikipata sapoti
kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi wabunge nao katika kuunga mkono
hilo kila mmoja amekuwa na kiu ya Jimbo lake kuwa la mfano katika eneo
hilo.
Abdallah
Ulega ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga lililopo Wilaya ya Mkuranga mkoani
Pwani kwa upande wake tangu achaguliwe na wananchi wake ameonesha
dhamira na kiu ya kutaka kuwakomboa wananchi wake Kwa kutaka jimbo hilo
kuwa na viwanda.
Anasema kuwa
lazima wao kama wawakilishi wa wananchi Kwa maana ya wabunge
wanaotokana na Chama cha Mapinduzi CCM wapokee Kwa mikono miwili mageuzi
haya kwani wameahidi hivyo lazima watende.
Ulega
anasema kuwa Jimbo la Mkuranga ni kubwa na linarutuba ya kutosha hivyo
anakaribisha wawekezaji kuingia na kukubali Kuwekeza viwanda
vidogovidogo na vikubwa katika kilimo hasa cha mazao mbalimbali Kwa
ajili ya maendeleo ya watu wake.
Anasema kuwa
kuna jitihada kama Mbunge amekuwa akizifanya za kuhakikisha kwamba
jimbo lake ni miongoni mwa majimbo ambayo yanafaidika na mikakati ya
Serikali ya kutaka mageuzi ya viwanda.
0 comments:
Post a Comment