Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky akitoa vyeti kwa wawakilishi
wa Kampuni mbalimbali zilizosaidia katika kampeni ya siku 10 ya kufanya
usafi katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA),Zoezi la
utoaji Vyeti limefanyika katika lango la Marangu wakati wa hafla fupi ya
kuwapokea washiriki wa zoezi hilo la usafi.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky akizungumza na washiriki wa
kampeni ya siku 10 ya kufanya usafi katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima
Kilimanjaro (KINAPA) muda mfupi mara baada ya kurejea.
Baadhi
ya Washiriki wa Kampeni ya siku 10 ya kufanya usafi katika Hifadhi ya
Taifa ya Mlima Kilimanjaro wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro Said Mecky Sadicky alipokuwa mgeni rasmi katika Hafla ya
kutunuku vyeti kwa washiriki pamoja na wamiliki wa kampuni.
Mkuu wa Wilaya ya Moshi,Novatus Makunga akizungumza katika Hafla hiyo.
Baadhi ya Washiriki wa zoezi hilo.
Mkuu
wa Wilaya ya Siha ,Dkt Charles Mlingwa akizungumza katika hafla hiyo
baada ya kukaribishwa huku akiwasilisha ombi la zoezi kama hilo la usafi
lielekezwe katika lango la kupandia mlima la Londros lilopo wilayani
Siha.
Baadhi ya Washiriki wa zoezi hilo ambao wanajulikana kama Wagumu.
Kaimu
Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Mtango
Mtahiko akizungumza juu ya mafanikio ya kampeni ya siku 10 ya usafi
katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro.
Katibu
Tawala mpya wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Mhandisi Aisha Amour akifuatilia
shughuli hiyo ya kutunuku vyeti ilivyokuwa ikiendelea .
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA),Betrita Loibook akizungumza katika hafla hiyo.
Mhifadhi
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA)Betrita Loibook
akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Siha,Dkt Charles Mlingwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro akiliongoza kundi la watu waliopanda Mlima
Kilimanjaro kwa ajili ya kufanya usafi muda mfupi baada ya kurejea
kutoka katika kilele cha mlima huo.
Baadhi ya washiriki wa zoezi hilo.
Washiriki
wa zoezi la usafi katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro wakiwa katika
picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick huku
wakionesha vyeti walivyotunukiwa baada ya kufanikisha zoezi hilo.
Washiriki wakifurahia vyeti.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadicky akizungumza jambo na
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Betrita
Loibook.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
0 comments:
Post a Comment