Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia
Wakandarasi, Wahandisi na wadau mbalimbali wa sekta ya Ujenzi kabla ya kufungua
rasmi Mkutano wa Siku mbili wa
Mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini CRB uliofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Akitoa mfano, Mhe. Magufuli alisema katika ujenzi wa
mahakama za mwanzo hapa nchini, jengo moja lilikadiriwa kukamilika kwa milioni
200 lakini wakandarasi wa Tanzania walioomba zabuni hiyo walitoa kiwango cha
kati ya shilimgi milioni 670 na bilioni
1.4. Amesema kwa jinsi hii hata mtu awe na huruma ya namna gani hawezi kuwapa
kazi.
Amesema serikali yake itawajali kwanza wakandarasi wa hapa
nchini lakini akawataka wajipange na pengine waungane ili kufanya kazi kwa
pamoja.
Aidha, Mhe. Rais amesema ujenzi wa bomba la mafuta kutoka
Hoima, Uganda hadi Tanzania unakaribia kuanza lakini akauliza wakandarasi wa
hapa nchini wamejipangaje katika kushiriki ujenzi huo.
Kuhusu ulipaji wa madeni ya wakandarasi, Mhe Rais amesema,
serikali yake imekuwa ikilipa madeni hayo na itaendelea kufanya hivyo hadi deni
litakapoisha. Amesema kwa kuanza serikali imelipa bilioni 650 na baadaye
ikatumia bilioni 462 kutoka Mfuko wa Barabara kuwalipa wakandarasi.
Amesema wakandarasi ni watu wa muhimu sana katika maendeleo
ya Taifa na ni injini ya maendeleo kwani wako kila sekta ya maendelo. Amesema
kwa mfano wako katika ujenzi wa
mioundombinu, kwenye zana za kilimo,kwenye uvuvi, na pia usafirishaji wakandarasi
hawakosekani.
|
0 comments:
Post a Comment