Mkurugenzi
wa Utafiti na Mipango Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu
Bi. Naima Mrisho akitoa neno la ufunguzi katika mkutano wa kujadili na
kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na
Kukabiliana na Maafa katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya
ya Kilosa mkoani Morogoro Mei 30, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mwenyekiti
wa Chama cha Msalaba Mwekundu Bw. Christopher Chusi akichangia hoja
wakati wa mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango
wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa uliofanyika Mei 30,
2016 Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi
ya wajumbe wa mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya
Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa wakifuatilia
mada ya Menejimenti ya Maafa kutoka kwa Mratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri
Mkuu Bw. John Kiriwai (hayupo pichani) katika Ukumbi wa Mikutano wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Morogoro tarehe 30 Mei, 2016. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkurugenzi
wa Utafiti na Mipango Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu
Bi. Naima Mrisho akiwaongoza Wajumbe wa Kamati ya maafa katika zoezi la
ukakamavu katika kujiandaa na kukabili maafa wakati wa mkutano wa
kujadili na kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa
Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa Wilayani Kilosa tarehe 30 Mei, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mratibu
wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Fadhili Mtengela akiwasilisha mada ya
kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na
Kukabiliana na Maafa katika mkutano wa kujadili mpango huo uliofanyika
Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro tarehe 30 Mei,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkuu
wa Wilaya ya Kilosa Mhe. John Henjewele (katikati) akiwa katika picha
ya pamoja na wajumbe wa mkutano wa kujadili na kuboresha rasimu ya
Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa
mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo Wilayani kilosa Morogoro tarehe 30
Mei, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Na. Mwandishi Wetu
Ofisi ya Waziri Mkuu imejadili na
kuboresha rasimu ya Kiswahili ya Mpango wa Halmashauri wa Kujiandaa na
Kukabiliana na Maafa wilayani Kilosa Mei 30, 2016.
Rasimu hiyo imejikita katika
kutoa miongozo ya uratibu katika kukabili dharura za aina zote za
majanga yanapotokea katika ngazi zote za Kitaifa.
Akizungumza na wajumbe wa Kamati
ya Maafa Wilayani Kilosa Mkurugenzi wa Tafiti na Mipango Idara ya
Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bi. Naima Mrisho alieleza kuwa
muongozo huo ni sehemu ya kuisaidia jamii katika kupata mbinu bora
za kujiandaa, kukabili, na kurejesha hali pindi maafa yanapotokea ili
kuzisaidia jamii zetu.
“Ni muhimu kuwa na mpango huo kwa kuzisaidia Halmashauri zetu katika kupambana na maafa yanayotukabili,”alisema Bi. Naima
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Kilosa Mhe. John Henjewele alibainisha umuhimu wa Mpango huo ikiwa ni
sehemu ya kuanzia na inayotoa muongozo mzuri unaosaidia katika
Halmashauri yake katika kukabiliana na Maafa.
“Tangu mpango kuanza kutumika
Desemba 2013 Wilaya ya Kilosa imeweza kuwa na mbinu za kuyakabili maafa
yanapotokea hususani yale ya mafuriko” Alisema Mkuu wa Wilaya.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Kilosa Bw. Idd Mshili aliipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa
kuona umuhimu wa kuitembelea Halmashauri yao kwa kuupitia Mpango na
kuuboresha ili kusaidia kurahisisha uelewa kwa kua lugha ya Kiswahili
inaeleweka kwa urahisi hususani ngazi ya chini na kwa wanavijiji
wanaokumbana na maafa pindi yanapotokea.
“Nichukue fursa hii kuwapongeza
Idara ya Uratibu wa Maafa kwa kuona umuhimu wa kuubadili mpango kutoka
lugha ya Kingereza kuwa katika lugha ya Kiswahili ili kufikia makundi
yote ya jamii kwa urahisi.”
AWALI: Mpango wa Halmashauri wa
Kujiandaa na Kukabiliana na Maafa ulianza kutumika mwaka 2013 ikiwa na
lengo la kuziwezesha Halmashauri kujiandaa na kuyakabili maafa
yanapotokea, Ofisi ya Waziri Mkuu imefanikiwa kufanya Tathimini kwa
Halmashauri za baadhi ya Mikoa kwa kuangalia ubora wa mpango tangu uanze
kutumika katika Mikoa ya Mtwara, Kilimanjaro, Morogoro, Dodoma, Singida
na Shinyanga kuanzia Mei 23 hadi 30, 2016.
0 comments:
Post a Comment