Mkuu
wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela (kushoto) akipokea sehemu ya madawati
70 kutoka kwa Meneja Masoko wa Benki ya B arclays Tanzania (BBT)
Nasikiwa Berya yaliyotolewa ba benki hiyo kusaidia Shule ya Sekondari
Handeni kupitia timu yake ya soka iliyopewa jina la ‘Blue Eagle’ ikiwa
ni sehemu ya juhudi za benki hiyo katika kusaidia jamii. Hafla ya
makabidhiano ilifanyika wilayani Handeni mkoani Tanga hivi karibuni.
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela (kushoto), akikabidhi madawati hay kwa
baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Handeni wilayani humo hivi
karibuni.
Meneja
Masoko wa Benki ya B arclays Tanzania (BBT) Nasikiwa Berya (watatu
kushoto), akikabidhi sehemu ya msaada wa madawati 70 kwa Mwanafunzi wa
Shule ya Sekondari handeni, Amani Mmbaga, yaliyotolewa na benki kupitia
timu yake ya soka iliyopewa jina la ‘Blue Eagle’ ikiwa ni sehemu ya
juhudi za benki hiyo katika kusaidia jamii. Hafla ya makabidhiano
ilifanyika wilayani Handeni mkoani Tanga .
Mmoja wa maofisa wa Benki ya Barclays Tanzania, Raymond Bunyinyiga (kushoto), akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Benki ya Barclays wakibeba madawati tayari
kuyakabidhi kwa mkuu wa mkoa wa Tanga kusaidia shule za sekondari
wilayani Handeni.
Mchezaji
wa timu ya soka ya Benki ya Barclays iitwayo ‘Blue Eagle’ Edwin Makata,
akichuana na Issa Silaji (kulia) wa timu ya soka ya Shule ya Sekondari
Handeni, katika mchezo wa kirafiki mara baada ya kukabidhi msaada wa
madawati 70 yaliyotolewa na timu hiyo.
0 comments:
Post a Comment