Na Daudi Manongi
Hifadhi ya Taifa
ya wanyamapori ya Selous iliyopo kusini
mwa Tanzania imepoteza asilimia 90 ya Tembo
waliopo katika hifadhi hiyo kutokana na ujangili uliokithiri.
Ripoti ya mfuko wa hifadhi
ya wanyapori na mazingira duniani (WWF) imesema kufikia mwaka 2022 kama
hakutakuwa na hatua zozote kali zitakazochukuliwa kuwalinda tembo kutokana na
ujangili basi watatoweka kabisa.
Ripoti hiyo
imeendelea kusema kuwa kwa miaka ya nyuma mbuga ya Selous ilikuwa mojawapo ya
mbuga kubwa kabisa katika bara la afrika yenye tembo wengi ambapo kulikuwa na
tembo zaidi ya 110000 lakini kutokana na ujangili uliokithiri katika miaka 40
iliyopita tembo hao wamepungua na kubakia 15000 tu uku mahitaji makubwa ya
pembe za ndovu katika nchi ya china yakitajwa na ripoti hiyo kuwa kichocheo
kikubwa cha ujangili na mauaji ya idadi kubwa ya tembo hao.
Aidha ripoti hiyo
inaonyesha hathari kubwa kiuchumi
itakayotokea kutokana na kwamba Tanzania
kupitia Mbuga ya Selous inaingiza dola milioni 6 kwa mwaka ikilinganishwa na Sekta
ya Viwanda inayochangia dola bilioni 5 katika pato la Taifa.
Pamoja na Hayo
Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara
ya Maliasili na Utalii imeweka mikakati madhubuti ikiwemo kuunda kitengo chake
cha intelijensia na kuunda kanda nane za doria za ushirikiano katika mifumo ya
ikolojia ya mbuga ya Selous ambayo imeanza kuwa na mafanikio ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wadau wa
uhifadhi kuwezesha upatikanaji wa vitendea kazi na zana kwa ajili ya doria.
Mwaka 2014 Shirika la
Kimataifa la Sayansi,Elimu na Utamaduni la umoja wa mataifa(UNESCO) liliiweka
Mbuga ya Selous katika Urithi wa asili ulio hatarini Duniani.
0 comments:
Post a Comment