Kutokana na kudaiwa deni la zaidi ya mil 100 kanisa la Sinza
Christian Center latupiwa nje vyombo
vyake na dalali aliyepewa tenda hiyo bwana Joshua aliyeteuliwa na Mahakama na
mmiliki jengo hilo Bwana Prosper Rwendera .
Akizungumza
na Dar es salaam
yetu Blog mke wa mmiliki wa jingo Hilo Bi. Patricia Prosper Alisema;
“huyu aliyepanga hapa hakufuata utaratibu wowote na ndiyo maana tukapewa
jengo letu."
Alipotafutwa
msemaji wa Kanisa ambaye ni Askofu anayedaiwa kuvamia jengo hilo,
hakupatikana kuzungumzia
sakata hilo na hata waumini wa kanisa hilo walipotafutwa walikataa kwa
madai hawana mamlaka ya kuzungumzia lolote kuhusiana na sakata hilo.
Hili ni eneo la Kanisa Hilo.
Viti vyote vikiwa vimetolewa nje.
Vyombo vya Muziki vikiwa nje.
Magari yakiwa yanatolewa nje.
Vitu vikiwa nje ya Jengo hilo ambapo mpaka sasa kuna sinto fahamu vinapelekwa wapi.
Vikombe nje...
Wametoa vitu vyote....
Baadhi ya Magari yaliyotolewa katika Jengo hilo ambapo hapo awali ilikuwa ni Kanisa.
Kushoto
kwa mbali ni Mke wa Miiliki wa Jengo hilo Bi. Patricia Prosper
akiendelea na majukumu huku pembeni vijana wakipata maelekezo ya
kuendelea kutoa vitu.
Picha zote na Fredy Njeje/ Blogs za Mikoa
0 comments:
Post a Comment