Na Lilian Lundo-MAELEZO
Serikali ya awamu ta Tano
imedhamiria kuifanya sekta ya Viwanda nchini kuchangia pato la taifa kwa
asilimia 40 ifikapo mwaka 2020 kutoka asilimia 7.3 ya sasa
Hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya
utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo
Jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli amesema kuwa jambo
hilo linawezekana hasa kwa kuzingatia nchi yetu ina rasilimali
zinazohitajika katika kujenga uchumi wa viwanda.
“Nafahamu kwamba tunakila aina ya
rasilimali inayowezesha uwepo wa viwanda hapa nchini ikiwemo umeme wa
kutosha pamoja na malighafi zake na kwa maana hiyo serikali ya awamu ya
tano imepanga kuifanya sekta ya viwanda kuchangia pato la taifa kwa
asilimia 40 ifikapo mwaka 2020 kutoka 7.3 ya sasa”. Alisema Rais
Magufuli.
Aidha Dkt. Magufuli aliwatoa
wasiwasi wadau hao kuhusu uwepo wa soko la uhakika kwa bidhaa
zitakazozalishwa kwani Tanzania imezungukwa na nchi zenye uhitaji wa
bidhaa mbalimbali na pia ni Mwanachama wa jumuiya mbalimbali ndani na
nje ya Afrika.
Naye Waziri wa Viwanda, Biashara
na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage aliwataka wamiliki wa Viwanda Nchini
kuunganisha nguvu katika uanzishaji na uendelezaji wa viwanda nchini ili
kuongeza upatikanaji wa bidhaa nchini hali itakayopelekea kukuza uchumi
wa nchi na kuongeza ajira kwa watanzania.
0 comments:
Post a Comment