Serikali kuunda
chombo cha kudhibiti upandaji wa kodi za nyumba za kupanga
Na Daudi
Manongi-MAELEZO
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya
Makazi Dkt Yamungu kayandabila amesema kuwa serikali iko mbioni kuunda chombo
cha kudhibiti upandaji wa kodi za nyumba za kupanga.
Dkt Kayandabila ameyasema hayo leo hii jijini Dare
s Salaam alipokuwa akizungumza katika kipindi cha asubuhi cha Power Breakfast
kinachorushwa na Clouds Fm.
“Sisi kama serikali tumesikia kilio cha wapangaji
na tuko mbioni kumaliza tatizo hili kwa kuunda chombo kitakachodhibiti upandaji
wa kodi hizi za nyumba kiholela,tumeshapokea kesi nyingi sana kutoka kwa
wananchi na hivyo tumejipanga kulitatua kabisa tatizo hili”Alisema Dkt Yamungu.
Aidha katibu mkuu huyo amewaasa wapangaji wa
nyumba za kupanga kuhakikisha wanakuwa na mikataba ya kisheria yenye
makubaliano ya pande zote mbili kupunguza migongano isiyokuwa ya kilazima na
kushauri kama watashindwa kumudu gharama za mwanasheria wanaweza kuwatumia
wenyeviti wa serikali za mitaa kama mashaidi katika kusaini mikataba yao.
Awali ya yote Dkt Yamungu alizungumzia kukamilika
kwa Sera ya nyumba ambayo iko mbioni kukamilika ikizungumzia masuala haya yote
na kwa kiasi kikubwa sera hii itapunguza migogoro mingi ya masuala ya nyumba
kwa ujumla.
Mwaka huu mwezi wa nne Waziri wa Ardhi,Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi aliweka wazi Bungeni nia ya serikali
kutungwa kwa sheria itakayounda chombo cha kudhibiti upandaji wa kodi za nyumba
za kupanga.
0 comments:
Post a Comment