Na matukiodaimaBlog
WAZIRI wa Kilimo ,Mifugo na
uvuvi Bw Mwigulu Nchemba amewaomba radhi watanzania kwa usumbufu mkubwa walioupata baada ya kuadimika kwa
sukari kwa siku miezi michache
iliyopita na kuwa serikali inaendelea kutafuta
ufumbuzi wa
kudumu kwa kuagiza sukari tani 70,000 kutoka nje ya Tanzania.
Mwigulu ambae ni mbunge
wa jimbo la Iramba aliyasema haya jana
wakati wa ziara yake ya
kuwashukuru wananchi wake
kwa kumchagua kuendelea
kuwa mbunge wa jimbo
hilo kwenye uchaguzi mkuu
uliofanyika mwaka jana pasipo kufanya kampeni .
Akijibu kero za
wananchi wa kijiji hicho cha Kilampanda alisema
kuwa kero hiyo ya
sukari si kwa kijiji
hicho pekee kwani kuna baadhi ya maeneo
wananchi walikuwa wakikosa kabisa sukari hata ile inayouzwa kwa
bei kubwa japo kwa sasa hali ya upatikanaji wa sukari imeanza
kurejea katika hali ya kawaida
baada ya serikali kuagiza sukari kutoka
nje .
Alisema kuwa kuwa
tani zaidi ya 20,000 zimeingia
nchini wiki moja iliyopita na hivi sasa
tani 15,000 zipo njiani kuingia nchini
hivyo bei ya sukari itashuka zaidi ya bei ya sasa baada ya sukari kuingia kwa
wingi.
“ Mimi niwahakikishie
muda si mrefu hali ya Sukari itarejea katika bei ya kawaida japo wapo
baadhi ya watu wananunua
akiba ya sukari kwa wingi kwa bei
ya sasa ila nawaondoa hofu kuwa sukari itapatikana kwa wingi mbeleni kwani uzalishaji utaanza hivi
punde”
Alisema kuwa imekuwa
ni kawaida bei kupanda juu
zaidi pindi bidhaa zinapoadimika japo ushukaji
wake huwa wa kusuasua na katika kukabiliana na uhaba
wa sukari na mfumko wa bei
serikali imelazimika kuagiza
sukari kwa wingi na
itaendelea kufanya hivyo
ili kuwa na sukari ya ziada
ili kutopata adha
tena ya sukari.
Hata hivyo alisema
kwa kuwa sukari
hiyo tano 20,000 zimekwisha ingia na tani 15,000 zipo njiani kuingia
suara ya
usambazaji linaendelea kufanyika
ili kuwafikia wananchi kote nchini ,sukari itakayouzwa
kwa bei
ilekezi ya serikali.
Awali wananchi wa
kijiji hicho cha Kilampanda walimlalamikia waziri
huyo kupanda kwa bei ya sukari hadi
kufikia kiasi cha Tsh 3000 kwa
kilo na kabla ya serikali
kutoa bei elekezi
sukari kila mfanyabiashara alikuwa akiuza kwa bei yake wengine
wakiuza hadi Tsh 4000 kwa kilo
jambo ambalo lilikuwa
likiwatesa wananchi wenye
kipato cha chini.
0 comments:
Post a Comment