Meneja utetezi kutoka Shirika la Kimataifa la OXFAM Tanzania Bi. Eluka Kibona akifungua mafunzo juu ya uelewa wa Bajeti ya Kilimo na Mabadiliko ya Tabianchi yanavyoathiri sekta ya kilimo Tanzania hasa wakulima wadogo wadogo.
Mkurugenzi wa Forum CC Bi. Rebecca Muna akielezea umuhimu wa mafunzo hayo yatakavyoweza kuwasaidia wakulima wadodogo katika kukabiliana na tatizo la Mabadiliko ya tabianchi.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo hayo wakiwa katika kikundi kujadiliana maswala mbalimbali juu ya namna ya kuandaa bajeti
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo hayo wakiwa wanawasikiliza wenzao wakati walipokuwa wanawasilisha mada walizopewa
Muwezeshaji kutoka Forum CC Feizal Ally Akiongoza majadiliano juu ya uandaaji wa bajeti ya kilomo na mabadiliko ya tabianchi ambayo yanawathiri kwa kiasi kikubwa wakulima wadogo wadogo.
Baadhi ya wadau waliohudhuria mafunzo hayo wakiwa wanatazama mfano wa jarida linalo onesha jinsi bajeti inavyo andaliwa
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo ambao ni wakulima wadogo wadogo wakichangia mada juu ya changamoto wanazozipata katika kuandaa Bajeti na kutoshirikishwa
Baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo wakichangia juu ya mabadiliko ya Tabianchi yanavyosababisha athali katika kilimo.
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo
Picha na Fredy Njeje
Dar es salaam, Wanawake wakulima wadogowadogo
wakiongozwa na waliokuwa washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaloratibiwa
na shirika la Oxfam, wamekutana pamoja na wadau kutoka taasisi mbalimbali na
baadhi ya wanafunzi kutoka elimu ya juu, Tanzania kujadili Bajeti ya Kilimo kwa mwaka 2016/17 na changamoto za mabadiliko ya Tabia Nchi.
Akifungua Mkutano huo wa siku tatu, Meneja utetezi wa Oxfam Tanzania, Bi. Eluka
Kibona alisema kuwa lengo la kuwakutanisha wakulima hao na wadau ni kufanya
majadiliano juu ya Bajeti ya kilimo na Mabadiliko ya Tabia Nchi kwa kuwa hali
ilivyo sasa ni kwamba wakulima wengi hasa wadogowadogo hawapati nafasi ya
kushirikishwa katika masuala ya bajeti hiyo, hivyo mkutano huo utasaidia kuibua
changamoto mbalimbali ambazo zitatakiwa kutatuliwa bila kusahau suala la
mabadiliko ya Tabia Nchi ambayo yataathiri kwa kiwango kikubwa katika kilimo.
Akizungumza
katika mkutano huo Mkurugenzi wa Programu Forum CC, Bi. Rebecca Muna alisema
mabadiliko ya Tabia Nchi yamekuwa yanaendelea kuathiri zaidi wakulima wadogo
wadogo hasa waliopo vijijini, hivyo kupitia mkutano huo wakulima wanapata elimu
ili kukabiliana na mabadiliko hayo.
Akieleza kwa undani juu ya Mabadiliko ya tabia nchi
mwezeshaji kutoka Forum CC, Faizal Ally alisema kwamba changamoto kubwa zaidi
ya mabadiliko ya Tabia nchi ni pamoja na maji chumvi kuingia nchi kavu na
kuathiri ukuaji wa mazao, kuongezeka kwa joto, misimu ya mvua zisizotabirika, kupungua
kwa kina cha maji katika mito na maziwa, kuongezeka kwa majanga ya hali ya hewa
ikiwa ni pamoja na mafuriko, ukame na vimbunga na kuongezeka kwa magonjwa ya
mazao.
Alisema kuwa
mambo yote hayo yamekuwa yakichochea wakulima na wafugaji kukosa maeneo
ya malisho kwa ajili ya mifugo na kuongeza kuwa ili wakulima waweze kukabiliana
na changamoto hiyo ya mabadiliko ya Tabia nchi wanatakiwa kujifunza mbinu
mbalimbali ikiwemo kuvuna maji ya mvua, kutumia umwagiliaji wa matone, matumizi
ya mbegu bora zinazostahimili magonjwa na Ukame, kilimo mchanganyiko/mseto,
matumizi ya mbolea asili na kuongeza thamani ya mazao.
Nao wakulima hao kwa nyakati tofautitofauti walizungumzia
suala zima la bajeti ambapo walisema kuwa changamoto nyingi wanazozipata kwa
kutoshirikishwa kwenye bajeti kuu juu ya kilimo zinasababisha wasifikiwe na
elimu na huduma mbalimbali zitakazowasaidia kwenye shughuli zao za kilimo hivyo
basi kupitia mkutano huo wameomba kusikilizwa maoni yao hasa wakati wa uandaaji
wa bajeti kwa ujumla kwa kuwa wao ndiyo walengwa namba moja kwenye sekta ya
kilimo nchini.
0 comments:
Post a Comment