Mahali anapo lala kijana Emanuel Fedrick (20)Mkazi wa Mwambeja Kata ya Ilemi jijini kwa zaidi ya Miaka 11 sasa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kuficha aibu ya familia. |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Katika hali isiyokuwa ya kawaida
kijana mwenye tatizo la ulemavu wa
viungo na akili, amegundulika kufungiwa ndani kwa zaidi ya miaka 11 na
wazazi wake katika eneo la Mwambenja Kata ya Ilemi Jijini hapa.
Kijana huyo, mwenye umri wa miaka
20, ambaye amejulikana kwa jina la Fredrick Emmanuel ametajwa kuwa amekuwa
akiishi ndani bila ya kutolewa nje hali
iliyochangia kwa kiasi kikubwa kudhohofisha mwili wake .
Mmoja wa majirani ambaye hakutaka
jina lake litajwe amesema kuwa Kijana huyo licha ya kuzaliwa akiwa na ulemavu
wa viungo vya mikono na miguu,pia amezaliwa akiwa na utindio wa ubongo hali
inayomfanya kushindwa kuongea.
Amesema wazazi wa mtoto huyo
wamekuwa wakimfungia ndani ambapo hata wao hawakuluhusiwa kuingia ndani ya
nyumba hali iliyowafanya washituke na kutoa taarifa ili kumuokoa kijana huyo.
Akizungumzia tukio hilo , Mwenyekiti
wa mtaa wa Mwambenja, Rosemary Jama, amesema taarifa za Ferdrick kuishi ndani
ya nyumba hiyo walikuwa nazo lakini hawakuwahi kupata taarifa za kwamba
kijana huyo hatolewi nje.
“Sisi tunafahamu ndani ya nyumba ya
Emmanuel kuna mtoto ambaye ni mlemavu lakini hatukuweza kufahamu mazingira
anayoishi kijana huyu, nimeshuhudia kweli huu ni unyanyasaji wa kijinsia, licha
ya kutotolewa nje lakini kijana huyu anaonekana amekosa chakula,”alisema.
Akizungumza huku akionesha
kutojali , Baba wa kijana huyo Emmanuel
John , anasema mwanae Fedrick, alizaliwa mwaka 2007 ukiwa ni uzao wake wa
kwanza katika familia hiyo na akufuatiwa na wenzake watatu ambao wote mungu
amewajalia na kuzaliwa wakiwa wazima.
Kufuatia tukio hilo baadhi ya
majirani wameomba mamlaka husika kuingila kati ili kumsaidia kijana huyo kwani
maisha yake yapo hatarini kutokana na wazazi kutoonesha kujali.
0 comments:
Post a Comment