Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 4:00 asubuhi wakati basi hilo dogo lenye namba za usajili T 245 AMH likitokea jijini Mbeya kwenda Chimala wilayani Mbarali lilipogongana na lori lenye namba za usajili T276 ATQ lililokuwa likitokea jijini Dar es Salaam kwenda Tunduma.
Watu walioshuhudia ajali hiyo walisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni lori ambalo lilikuwa likiyumba barabarani.
Muuguzi wa zamu katika kitengo cha huduma ya haraka cha Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Jane Kipenye, alisema kuwa amepokea majeruhi 11, lakini mmoja alipoteza maisha wakati akiendelea kupatiwa matibabu.
Kipenye aliwataja majeruhi hao kuwa ni Elia Mlowa (18), Fizara Kassim (28), Hajira Abdallah (8), Elika January (26), Charles Gumani (53), Doto Jagala (44), Beta Sanga (52), Maria Anania (32), Isaka Leonard (17) na Erasto Mlwale (34).
Alisema kuwa majeruhi mmoja ambaye alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu jina lake halikufahamika mara moja kwa sababu alikuwa hawezi kuzungumza.
Kwa upande wake, muhudumu wa chumba cha maiti cha Hospitali ya Rufaa Mbeya, Augen Vuruga, alisema kuwa amepokea miili sita ya watu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo na kuwa kati ya maiti hizo tayari tano zimetambuliwa na moja haijatambuliwa.
Kwa mujibu wa Vuruga, waliofariki dunia na miili yao kutambuliwa ni Steven Kimario, Shalfa Abdallah, Simon Mwakalukwa, Maria Mwanginde na Andrea Simbeye.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuahidi kuitolea maelezo zaidi baada ya kupata taarifa zaidi kutoka kwa askari waliokwenda katika eneo la tukio.
BASI AINA YA TOYOTA HIACY YANYE NAMBA ZA USAJIRI T245 AMH ILIYOGANWGA NA ROLI LA MIZIGO |
NDUDU MSOMAJI NA MPENZI WA BLOG YETU TUNAKUOMBA RADHI KWA PICHA ZA MAITI UTAKAZOZIONA KATIKA HABARI HII KWAKUA ZINA HARI MBAYA NA KAMA HAUTAWEZA KUVUMILIA TUNAOMBA USIENDE KUZITAZAMA
BAADI YA MIILI YA WATU WALOPOTEZA MAISHA KATIKA AJARI HIYO
BAADHI YA MAJERUHI WAKIKIMBI MSAADA WA HARAKA KWA AJIRI YA KUPATIWA MATIBU AMBAO MAJINA YAO HAYAKUPATIKANA MAPEMA
0 comments:
Post a Comment