Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akihojiwa na
waandishi wa habari katika mkutano wa wadau wa Utafiti wa Viashiria na
Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 uliofanyika leo jijini Dar
es Salaam. Utafiti huo utafanyika nchi nzima kuanzia mwezi Agosti,
2016. Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa akihojiwa na
waandishi wa habari katika mkutano wa wadau wa Utafiti wa Viashiria na
Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 uliofanyika leo jijini Dar
es Salaam. Utafiti huo utafanyika nchi nzima kuanzia mwezi Agosti,
2016.
Na Veronica Kazimoto
30 Mei, 2016.
Wito umetolewa kwa wadau pamoja na wananchi ili kushiriki kikamilifu katika kuwezesha upatikanaji wa takwimu rasmi nchini.
Akizungumza
katika Mkutano wa Wadau wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI
Tanzania wa mwaka 2016/2017 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amesema wananchi
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wana mchango mkubwa katika
kufanikisha upatikanaji wa takwimu rasmi nchini.
“Leo
hii tumekutana na wadau mbalimbali wa Utafiti wa Viashiria na Matokeo
ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017 utakaofanyika mwezi Agosti mwaka
huu kwa ajili ya kujadili na kushauriana namna ya kufanya utafiti huu
kwa ufanisi ili kupata takwimu bora zitakazosaidia katika kutunga sera
na kupanga mipango ya maendeleo nchini”, amesema Dkt. Chuwa.
Dkt.
Chuwa amefafanua kuwa utafiti huu unategemea sana ushiriki wa wananchi
kwani wao ndio wadau na wahusika wakuu ambao wanapaswa kutoa ushirikiano
wa kutosha ili kurahisisha upatikanaji wa takwimu rasmi zitakazosaidia
Taifa katika kuboresha huduma za afya kwa manufaa ya watanzania wote.
Dkt.
Chuwa amesema Ofisi ya Taifa ya Takwimu ipo katika harakati za
kukamilisha maandalizi ya utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI
Tanzania 2016/2017 ambao utaanza kufanyika nchi nzima kuanzia mwezi Juni
mwaka huu.
Aidha Dkt. Chuwa amesema
utafiti huu ni wa kipekee ukilinganishwa na tafiti zilizotangulia
kutokana na kuongezeka kwa viashiria vitakavyo chunguzwa ikiwemo
kuangalia kiwango cha CD4, kiwango cha maambukizi mpya, upatiakanaji wa
huduma zinazohusiana na UKIMWI pamoja na kupima watoto wadogo wenye umri
chini ya mwaka mmoja.
Amesisitiza
kuwa kukamilika kwa utafiti huu kutasaidia Serikali katika kuboresha
huduma za afya nchini hasa katika kupambana na maambukizi mapya ya
UKIMWI na namna ya kuboresha upatikanaji wa vifaa tiba.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkazi wa ICAP nchini, Dkt. Fernando Morales
amesema utafiti huu ni wa muhimu katika kupima viashiria na matokeo ya
UKIMWI kwa nchi ambazo zimekuwa zikipata msaada wa kupambana na UKIMWI
kutoka Serikali ya Marekani.
“Lengo
la Utafiti huu ni kupata viashiria ambavyo vinasababisha maambukizi
mapya pamoja na kupima jinsi gani Taifa limeweza kupambana na ugonjwa wa
UKIMWI nchini”, amesema Dkt. Morales.
Utafiti
wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania wa mwaka 2016/2017
unafanyika katika nchi Ishirini (20) Afrika ambapo kwa sasa nchi nane
(8) zinaendelea na utafiti huu zikiwemo Zimbabwe, Zambia, Malawi, ,
Lesotho, Swaziland, Uganda, Namibia na Tanzania.
0 comments:
Post a Comment