Baadhi
ya wakazi wa mkoa wa mtwara waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa mpango
wa kugawa bure vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito
na watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki
chandarua.
Baadhi
ya watoto wa mkoani mtwara wakishindana kucheza muziki ikiwa ni sehemu
ya burudani zilizosindikiza hafla ya uzinduzi wa mpango wa kugawa bure
vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye
umri wa chini ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua.
Wasanii
Joe makini na Niki wa pili kutoka kundi la weusi wakitumbuiza hadhara
iliyojitokeza katika uzinduzi wa mpango wa kugawa bure vyandarua vyenye
viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya
miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Msanii
wa nyimbo za taarab isha mashauzi akiimba moja ya kibao chake wakati
akitoa burudani kwa wakazi wa mkoa wa mtwara waliohudhuria hafla
uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa
wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa
ujulikanao kama kliniki chandarua
Msanii
wa nyimbo za taarab isha mashauzi akitoa burudani kwa wakazi wa mkoa wa
mtwara waliohudhuria uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye
viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya
miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Mkuu
wa mkoa wa mtwara halima dendego akimbeba mmoja ya watoto
waliokabidhiwa chandarua chenye viuwatilifu ikiwa ni sehemu ya hafla ya
uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa
wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa
ujulikanao kama kliniki chandarua
Mkuu
wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akirusha maputo angani kuashiria
uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa
wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa
ujulikanao kama kliniki chandarua
Mkuu
wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akimkabidhi chandarua chenye
viuwatilifu mmoja ya mama wajamzito ikiwa ni sehemu ya hafla ya uzinduzi
wa mpango mpya wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu kwa wakina mama
wajawazito na watoto wenye umri chini ya miezi tisa ujulikanao kama
kliniki chandarua
Mkuu
wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego akimkabidhi chandarua chenye
viuwatilifu mmoja ya mama wenye watoto wa chini ya umri wa miezi sita
ikiwa ni sehemu ya hafla ya uzinduzi wa mpango mpya wa kugawa vyandarua
vyenye viuwatilifu kwa wakina mama wajawazito na watoto wenye umri chini
ya miezi tisa ujulikanao kama kliniki chandarua
Serikali
ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya
Malaria wameendelea na jitihada za kupambana na ugonjwa huo ili kufikia
lengo la serikali la kupunguza vifo hadi kufikia asilimia moja ifikapo
mwaka 2020.
Katika
kutekeleza azma hiyo, serikali ya Tanzania na wadau hao wamezindua
mpango wa kugawa vyandarua vyenye viuwatilifu vya muda mrefu kwa akina
wajawazito na watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa.
Akizindua
mradi huo kitaifa, mkuu wa mkoa wa Mtwara Bi Halima Dendego amewataka
wanawake kuhudhuria kliniki wakati wa ujauzito ili kupata ushauri na
kinga dhidi ya malaria ikiwa ni pamoja na kupata chandaru kitakacho
mkinga dhidi ya ugonjwa huo.Amesisitiza suala la kusafisha ameneo yote
ili kudhibiti mazalia ya mbu waenezao Malaria ikiwa ni njia moja wapo ya
kupambana na kuenea kwa ugonjwa huo unaosababisha vifo vya wakina mama
wajawazito na watoto wa chini ya miaka 5.
“kwa
mujibu wa Takwimu za ugonjwa huo kwa mkoa wa Mtwara, zimeshuka kutoka
asilimia 33 mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 17 kwa mwaka
2011/2012. Hata hivyo takwimu za kitaifa zinaonesha kushuka kwa ugonjwa
huo kutoka asilimia 33 mwaka 2007/2008 hadi kufikia asilimia 9 mwaka
2015”. Alisema Bi Dendego.“Lengo la kitaifa la mapambano dhidi ya
Malaria linaonesha kupunguza vifo hivyo hadi kufikia asilimia 5 mwaka
huu na asilimia 1 mwaka 2020 hivyo sisi mkoa wa Mtwara tuna jukumu la
kuhakikisha takwimu zetu zinaenda sambamba na takwimu za kitaifa”.
Amesisitiza Mkuu huyo wa mkoa.
Kwa
upande wake Naibu Mkurugenzi wa kutoka ofisi ya Afya ya shirika la
misaada la Marekani USAID Bibi Ana Bodipo -Memba amesema, ushirikiano wa
serikila ya Marekani na Tanzania katika mapambano dhidi ya Malaria
umeonesha mafanikio makubwa kwani wamefanikiwa kupunguza kwa silimia 50
vifo vitokanavyo na malaria kwa upande wa Tanzania Bara na chini ya
asilimia moja kwa upande wa Zanzibar.
“Marekani
inafahamu umuhimu wa mapambano dhidi ya Malaria, na hivyo mfuko wa Rais
wa Kupambana na Malaria kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania
imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo hivyo nah ii ni ishara
nzuri katika kufikia malengo ya kuutokomeza kabisa ugonjwa huu.” Alisema
Bi Bodipo.
Mwakilishi
wa wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Bi Helen
Semu amesema, serikali itaendelea na uhamasishaji wa jamii kuendelea
kutumia vyandarua vyenye viuwatilifu ili asilimia 85 iliyofikiwa kwa
sasa izidi kuongezeka na kufikia lengo la kumaliza kabisa tatizo hilo
nchini.“Sisi Serikalini tutahakikisha tunaongeza jitihada za kuhamasisha
jamii kuendelea kutumia vyandarua vyenye viuwatilifu ili kila mmoja
afahamu umuhimu wa kufanya hivyo na kudhibiti maambukizi na vifo
vitokanavyo na ugonjwa huu” alisema bi Helen
Mpango
wa utoaji vyandarua vyenye viuwatilifu kwa akina mama wajawazito na
watoto wenye umri wa chini ya miezi tisa ujulikanao kama CHANDARUA
KLINIKI unachukua nafasi ya mpango wa zamani wa HATIPUNGUZO na
unasimamiwa na Mradi wa VECTORWORK kwa kushirikiana na serikali ya
Tanzania na unfadhiliwa na mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na
Malaria chini ya usimamizi wa shirika la misaada la nchi hiyo – USAID.
0 comments:
Post a Comment