Muandaaji
wa tamasha la michezo kwa vijana wa mkoa wa Arusha Neema Mollel ambaye
pia ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Sakina pamoja na mlezi wa Timu za
mpira kata ya Sakina Jijini Arusha akiongea katika fainali za Tamasha la
vijana lililofanyika katika viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid
jijini hapa.
Martini Shimweta( Mdau) ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Olmatejoo A.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha Mjini Wilfred Soilel.
Diwani wa kata ya Ungalimited akiwa anawaasa vijana kuachana na madawa ya kulevya katika fainali hizo
Kiongozi wa Intersport Club akipokea kombe baada ya ushindi.
Na Woinde Shizza,Arusha
Timu
ya Intersport club yaibuka kidedea katika Tamasha la vijana mara baada ya kuifunga Club ya mairiva bao 3 kwa 1 katika fainali
iliyofanyika katika uwanja wa Shekhe Amir Abeid uliopo
Jijini Arusha.
Tamsha
hilo ambalo lilianza mapema mwanzoni mwa mwezi huu limeweza kufikia
tamati huku vijana wakiwatoa wito kwa wadau mbalimbali wa michezo
kujitokeza kuanzisha mashindano kama haya kwani yanawasiadia kwa kiasi
kikubwa
Akizungumza
wakati wa fainali za mashindano hayo muuandaaji wa mashindano hayo
ambaye ni mwenyekiti wa CCM kata ya Sakina Neema Mollel alisema kuwa
lengo la kuanzisha tamasha hili la vijana ni kuwaleta pamoja vijana na
kuwapa elimu ya jinsi ya kupiga vita utumiaji wa madawa ya kulevya kwa
vijana
Alisema
kuwa vijana wengi wamekuwa wanajishirikisha na utumiaaji wa madawa ya
kulevya ivyo aliona ni bora akatumia muda huu kuwaleta pamoja ili kuwapa
elimu pamoja na kuwashirikisha katika tamasha hili la michezo ambalo
limeweza kuwafundisha vijana wengi huku wengine wakiwa wameamua
kuaachana kabisa na kutumia madawa haya ya kulevya badala yake wameamua
kushiriki katika mazoezi pamoja na michezo
"nia alisi ya kuandaa mashindano haya ni kuwaleta kwa pamoja vijana pamoja na kupiga vita
madawa ya kulevya kwa vijana,kuwaleta vijana pamoja,kuwaondoa vijana
wasiendelee kukaa mitaani bila kazi kwani michezo ni ajira"Alisema Neema Mollel
Aidha aliwataka wazazi na jamii kwa ujumla kuwajengea vijana misingi
Imara ilikuwajengea mtizamo mzuri wa maisha ya mbeleni badala ya
kuwatupia lawama ambazo baadae zinajenga uadui kati yao na wazazi na
jamii.
Akikabidhi
kombe kwa washindi ambao ni Interspot club ,mwenyekiti wa CCM wilaya ya
Arusha Wilfred Soilel amesema kuwa Michezo hujenga hujenga
urafiki kati ya vijana ,wanafahamiana pia afya ya mwili inaimarika, pia
itamfanya kijana ufahamu wake kuchangamka.
Sambamba
ugawaji wa zawadi katika fainali hizo mshindi wa kwanza Intersport club
kutoka kata ya Ungalimited, amekabidhiwa Kombe pamoja na Tsh 100,000
,Mshindi wa pili Mairiva club Tsh 75,000 na mshindi wa tatu ni Black
Eagle Tsh 50,000.
0 comments:
Post a Comment