Tanzania ni miongoni mwa mataifa machache duniani yaliyojaliwa kuwa na rasilimali na madini mengi.
Na baada ya
kugunduliwa kwa gesi asili huko Mtwara na dhahabu sasa watafiti kutoka
Uingereza wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya
Helium nchini Tanzania.
Watafiti
kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na
wataalumu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi
bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika.
Ugunduzi huo umefanyika katika eneo la bonde la ufa la Tanzania.
Katika
taarifa kwa wanahabri huko Japan, watafiti hao wanasema kuwa uhaba wa
gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa madaktari
ambao wanatumia gesi hiyo adimu kuendesha mashine za utabibu
zijulikanazo kama MRI scanners, mbali na kutumika katika mitambo ya
kinyuklia miongoni mwa sekta zingine nyingi za kawi na teknolojia.
Kabla ugunduzi huo watafiti walikuwa wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo baridi ifikapo mwaka wa 2035.
Mnamo mwaka wa 2010 Mwanafizikia mshindi wa tuzo la Nobel Robert Richardson alikuwa ametabiri kumalizika kabisa kwa gesi hiyo.
Ukosefu huo
ulikuwa umesababisha wataalamu kuhimiza kutungwa kwa sheria
itakayopunguza matumizi yake katika bidhaa zisizo za dharura kama vile
kwenye vibofu kutokana na hali ya kuwa gesi hiyo ya Helium ni nyepesi
kuliko ile ya Oxygen.
''Gesi
tuliyoipata huko Tanzania inaweza kujaza silinda za gesi milioni moja
nukta mbili za mashine za MRI'' alisema Chris Ballentine kutoka chuo
kikuu cha Oxford.
0 comments:
Post a Comment