Na Neema Mwangomo
Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepokea msaada wa vifaa mbalimbali vya
watoto vyenye thamani ya Shilingi Milioni 23 kutoka Mgodi wa Dhahabu wa
Geita (GGM).
Msaada huo umetolewa kupitia chama cha Madaktari wa watoto Tanzania.
Vifaa
vilivyotolewa ni BP Machine 10, Infusion Pump 2, Thermometers 110,
Standing Weighing Scales 6, Lying Down Weighing Scales 6, Nebulies 3
pamoja na Pulse Oxymeter 10.
Akikabidhi
msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa GGM, Terry Mulpeter, Daktari
Mkuu wa mgodi wa GGM, Kiva Mvungi amesema lengo ni kuwa sehemu ya
jamii, lakini pia kutambua juhudi zinazofanywa na madaktari wa watoto
katika kuboresha huduma za afya.
“GGM
kama mdau katika sekta ya afya imeamua kutoa msaada huu ili watoto na
kina mama watakaofika Muhimbili waweze kupata huduma hizi muhimu kwani
tunatambua changamoto mnazopata katika kuwahudumia watoto, lakini pia
tunatambua mchango wenu,” amesema Daktari Mvungi.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Huduma za Tiba MNH ambaye ni Mkuu wa Idara ya Watoto, Daktari Mary Charles amesema msaada huo umekuja wakati muafaka kwani vifaa hivi ni muhimu na vinahitajika kwa ajili ya kuwahudumia watoto .
“Tunawashukuru
GGM kwa msaada wenu ni vifaa muhimu sana kwani unapotaka kumpatia
dawa mtoto hauangalii umri bali unaangalia uzito wake hivyo unampima
uzito kwanza alafu unampatia dawa kulingana na uzito wake” Amesema
Dk. Charles.
Kwa mujibu wa Dk Charles jengo la watoto hulaza watoto 300 ambapo pia kila kliniki ina uwezo wa kuchukua watoto 60.
0 comments:
Post a Comment