Pages

Ads 468x60px

Tuesday, June 28, 2016

Rais wa Zanzibar Dkt SHEIN awaapisha Naibu Katibu Wakuu Mjini Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein   akimuapisha Dk.Islam Seif Salum kuwa Naibu Katibu Mkuu ,Mifugo na Uvuvi katika Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi, katika  hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akimkabidhi hati ya kiapo  Dk.Islam Seif Salum  baada ya kumuapisha  kuwa Naibu Katibu Mkuu ,Mifugo na Uvuvi katika Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi, katika  hafla iliyofanyika leo  ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein  akimuapisha Nd,Hassan Abdulla Mitawi  kuwa  Naibu Katibu Mkuu Habari katika Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe,Zubeir Ali Maulid,(kulia) akifuatiwa na Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi mhe,Hamad Rashid Mohamed,Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo mhe,Rashid Ali Juma,pamoja na Viongozi wengine akiwepo Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe, Ayuob Mohamed Mahmoud wakiwa katika hafla ya kuwapishwa Watendaji katika Wizara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar leo Ikulu Mjini Unguja. 
[Picha na Ikulu]

0 comments:

Post a Comment