Watoto
kutoka taasisi ya "Pamoja Youth and Children Foundatio" ya jijini
Mwanza wakionyesha michezo ya sarakasi katika Maadhimisho ya miaka 40 ya
Mtoto wa Afrika, yaliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi
Mabatini kwa wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
.......................
Halmashauri ya Jiji la
Mwanza kwa kushirikiana na idara ya Ustawi wa Jamii, metakiwa kuwaondoa watoto
waliozagaa mitaani ambao wamekuwa wakiomba misaada kwa wasamaria wema barabarani.
Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku
ya Mtoto wa Afrika ambayo kwa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza yamefanyika shule ya msingi
Mabatini, Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga, amesema wengi wa watoto hao
wameacha shule kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kufiwa na wazazi ama
wazazi kutokuwa na uwezo wa kuwaendeleza kimasomo, hivyo Halamshauri hiyo ina
wajibu wa kuwasaidia.
Amesema hatua ya kuwaondoa watoto hao
inaweza kuonekana ni ngumu kutekelezeka, lakini inawezekana ikiwa kila mdau
ikiwemo jamii itatoa ushirikiano ambapo amewasihi madiwani katika baraza la halmashauri ya Jijini la Mwanza kupeleka hoja
kwenye baraza lao ili jambo hilo liwekwe kwenye vipaumbele vya Halmashauri hiyo.
"Mkurugenzi,
Meya na Madiwani wa halmashauri ya jiji la Mwanza, chukueni hatua
kuwaondoa watoto waliozagaa mitaani ikiwemo mtaa wa Nkuruma kwani hawako
pale kwa kupenda. Mkifanya hivyo itakuwa sifa kwenu na kwa baraza la
madiwani la mwaka 205/20". Amesema Konisaga.
Siku
ya mtoto wa Afrika huadhimishwa kila mwaka June,16 ikiwa ni kumbukumbu
ya mauaji ya mamia ya watoto waliouawa na polisi wa kikaburu mwaka 1976
katika Kitongoji cha Soweto nchini Afrika Kusini wakati walipokua
wakiandamana kupinga kubaguliwa kielimu kwa kufundishwa katika lugha
wasiyoifahamu ya Afrikana.
Katika
risala yao, watoto wameiomba serikali pamoja na jamii kuwalinda na
vitendo viovu ikiwemo ubakaji na ukatili unaowakumba ikiwemo kukosa
elimu.
Mkuu
wa wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Baraka Konisaga (wa kwanza
kushoto), ambae alikuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya miaka 40 ya
Mtoto wa Afrika, yaliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mabatini
kwa wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Mkuu
wa wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Baraka Konisaga, ambae alikuwa
mgeni rasmi katika Maadhimisho ya miaka 40 ya Mtoto wa Afrika,
yaliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mabatini kwa wilaya ya
Nyamagana mkoani Mwanza, akizungumza katika maadhimisho hayo.
Halleluyah
Benjamini ambae ni Katibu Baraza la Watoto mkoani Mwanza, akisima
risala ya watoto katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika
yaliyofanyika hii leo.
Halleluyah
Benjamini ambae ni Katibu Baraza la Watoto mkoani Mwanza (kushoto)
akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Paulina Robert.
Wanafunzi wakisoma ngojera katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
Mshereheshaji kutoka Baraza la Watoto mkoani Mwanza.
Wahudhuriaji
akiwemo mtoto kutoka Baraza la Watoto mkoani Mwanza, wakiendelea
kufuatilia maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika wilaya ya Nyamagana.
Viongozi
mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga (wa
tatu kushoto), wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
Kauli mbiu mkoani Mwanza.....
0 comments:
Post a Comment