Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dk.Lenard Akwilapo
akikabidhiwa picha na Mwakilishi Makazi wa Shirika la KAS, Daniel
El-Noshokaty ya waasisi wa ushirikiano kati ya Tanzania na Shirika
lisilo la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) la nchini Ujerumani, Hayati
Mwalimu Julius Nyerere (kushoto pichani) na Konrad Adenauer (kulia),
wakati wa Kongamano la la kitaifa na kimataifa lililokuwa na mada yake
kuu uadilifu wa viongozi na utawala bora katika usimamizi wa maliasili
kwa ajili ya maendeleo endelevu ya Tanzania lililofanyija katika Chuo
cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Dar es Salaam juzi.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania Bara, Philip Mangula akichangia jambo kwenye kongamano hilo.
Taswira katika ukumbi wakati wa kongamano hilo.
Mhadhiri
wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Apium Chengula (kulia),
akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akitoa
majumuisho yaliyofikiwa katika kongamano hilo.Kushoto ni Mratibu wa
Mipango wa Shirika la KAS, Richard Shaba.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dk.Lenard Akwilapo
(katikati mbele waliokaa), akiwa na viongozi mbalimbali na wanafunzi wa
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere wakati wa kongamano hilo. Kutoka
kulia waliokaa ni Mratibu wa Mipango wa Shirika la KAS, Richard Shaba, Makamu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania Bara, Philip Mangula, Mkuu
wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Dk. Shadrack Mwakalila,
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la KAS, Daniel El-Noshokaty, Naibu Mkuu wa Chuo Utawala Fedha na Mipango, Dk. Margaret Shawa na Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma, Dk. Thomas Ndaluka.
Na Dotto Mwaibale
VYOMBO
vyenye mamlaka vimetakiwa visiwatishe waandishi wa habari pale wanapo
andika habari sahihi za kuikosoa serikali nchini badala yake viwalinde.
Hayo
yalielezwa Dar es Salaam jana na Mhadhiri wa Chuo cha Kumbukumbu ya
Mwalimu Nyerere, Apium Chengula wakati wa majumuisho yaliyofikiwa
katika kongamano la kitaifa na kimataifa lililokuwa na mada yake kuu
uadilifu wa viongozi na utawala bora katika usimamizi wa maliasili kwa
ajili ya maendeleo endelevu ya Tanzania.
"Tulipitisha
maazimio kadhaa kama wenye mamlaka kuvilinda vyombo vya habari vinapo
andika habari sahihi za kuiokosoa serikali, kuhimiza viongozi
kuzingatia maadili na kupata mafunzo ya uongozi, kuhimiza viongozi
kulinda maliasili ambazo ni endelevu na kusisitiza kuwa na itikadi
inayoeleweka katika kuongoza nchi" alisema Chengula.
Kongamano
hilo liliandaliwa na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo
Kigamboni kwa ufadhili wa Shirika lisilo la kiserikali la Konrad
Adenauer Stiftung (KAS) la nchini Ujerumani.
Chengula
alisema kongamano hilo lilifanikiwa kutokana na kuwa na mada moto moto
zilizohusu rasilimali za taifa na suala zima la utawala bora na kuwa
lilisimamiwa na Kibweta cha Mwalimu Nyerere.
Alisema
Kibweta cha Mwalimu Nyerere ni idara iliyoanzishwa chuoni hapo kwa
ajili ya kusimamia masuala yote ya mafunzo ya viongozi na maadili ya
viongozi iliyoanzishwa mapema mwaka jana na kuzinduliwa na Rais mstaafu
Dk. Jakaya Kikwete.
"Katika
kongamano hilo kuliwa na mada mbalimbali zilihusu maliasili za Tanzania
na jinsi zinavyo wasaidia wananchi ambayo ilitolewa na Profesa Aidan
Msafiri kutoka Chuo cha Kanisa Katoliki Mwenge, mada nyingine ikiwa ni
utawala bora kuhusu mali asili changamoto na fursa zake iliyoendeshwa na
Dk.Camirius Kasala kutoka Chuo cha Takwimu cha Afrika Mashariki na kuwa
mada ya tatu ilihusu maendeleo endelevu katika Tanzania mchango wa
utawala bora unaozingatia maadili ya uongozi bora" alisema.
Alisema
Hayati Mwalimu Julius Nyerere kabla ya Uhuru 1961 alikwenda nchini
Ujerumani ambapo alionana na Muasisi wa Shirika la KAS, Konrad
Adenauer na kuona ni jinsi gani wataweza kusaidia kutoka mafunzo ya
uadilifu kwa viongozi na tangu hapo walianzisha ushirikiano huo ambao
unaendelezwa na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Shirika hilo
ambalo limefanikisha kudhamini kongamano hilo.
0 comments:
Post a Comment