Katika kuelekea kilele cha Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametembelea banda la Umoja wa Mataifa (UN) lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.
Makonda
alifika katika banda hilo na kupata nafasi ya kupata maelezo kutoka kwa
wafanyakazi wa UN kuhusu kazi ambazo zinafanywa na shirika hilo hapa
nchini.
Mtaalamu wa
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu (kulia) akitoa
maelezo ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
(katikati) alipotembea banda la shirika hilo lililopo katika ukumbi wa
Karume kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika
katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.
Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu kuhusu Malengo
17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ambayo yanatakiwa kumfikia kila
mwananchi alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa lillilopo katika
ukumbi wa Karume kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa
yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa
jijini Dar.
Mtaalamu wa
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu akimwonyesha
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Malengo 17 ya Maendeleo
Endelevu (SDG's) yaliyobandikwa katika banda la UN na jinsi
walivyojipanga katika kuelimisha wananchi kuhusiana na malengo hayo
kwenye Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika
viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar.
Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisaini kitabu cha wageni katika banda
la Shirika la Umoja wa Mataifa lililopo katika ukumbi wa Karume kwenye
Maonyesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja
vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar. Kulia ni Maafisa
Habari wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu na Usia Nkhoma Ledama. RC Makonda
amekuwa mgeni kwanza mashuhuri kutembelea banda hilo na kutoa baraka
zake kwenye maonyesho hayo.
Mtaalamu wa
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu katika picha ya
pamoja huku wakiwa na bango maalum linalowakilisha rangi za malengo 17
ya SDGs na mmoja wa vijana aliyetembelea banda la Umoja wa Mataifa
lililopo kwenye ukumbi wa Karume kwenye maonyesho ya 40 ya Biashara ya
Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya
Kilwa jijini Dar.
Afisa Habari
wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama
akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kuhamasisha wananchi
kutembelea banda hilo na kujifunza Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu SDGs
na kujua shughuli mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo hapa nchini.
0 comments:
Post a Comment