Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga.
Kushoto ni Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi,
Ikponwosa Ero na kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini (UN), Alvaro Rodriguez.
Nae
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanguga
alisema katika kongamano hilo wametoka na maazimio ambayo wanaiomba
serikali iweze kuyafanya ili kuwezesha watu wenye ualbino kuwa na
usalama wa uhakika.
"Tumejadili
mambo mengi lakini tunaiomba serikali ihusike moja kwa moja kupinga
unyanyasaji, ukatili na ubaguzi nia tunaiona kwahiyo tunaomba waendelee
kuwa hivyo na pia waongeze bajeti na zaidi katika matibabu kwa watu
wenye ualbino," alisema Nyanduga.
Kwa
upande wa Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia Mratibu Mkazi wa
mashirika hayo, Alvaro Rodriguez alisema ni wataendelea kuwasaidia watu
wenye ualbino ili kuwezesha kupunguza changamoto ambazo zinawakabili.
|
0 comments:
Post a Comment