Eneo la Kariakoo, Jijini Dar es Salaam |
MAANDALIZI ya Ripoti ya pili ya Maendeleo ya Binadamu (THDR) inayotarajiwa kuzinduliwa Juni 2017 yamefikia katika ngazi ya mwisho ya ukusanyaji wa maoni ya kitaalamu katika mada mbalimbali zinazojadiliwa katika ripoti hiyo.
Katika
warsha hiyo ya rasimu ya pili na ya mwisho kabla ya uhariri,
inajadiliwa na wanazuoni kupitia mada 11 ambazo zitakuwapo katika
taarifa hiyo ya Maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2017.
Warsha
hiyo ya siku mbili itatoa msingi wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu
nchini kwa kuangalia Sera ya hifadhi ya jamii katika muktadha wa
mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania.
Miongoni
mwa mada zilizojadiliwa jana baada ya ufunguzi wa kongamano hilo
uliofanywa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na
Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida ni usambazaji wa maji kwa kuangalia
sera, fedha na upatikanaji wake; elimu; sera ya jamii na mabadiliko ya
kiuchumi; na hifadhi ya jamii.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi
Kida akifungua warsha ya siku mbili iliyowakutanisha wanazuoni kuandaa
Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya mwaka 2017 jijini Dar es
Salaam.
.............................
.............................
Akifungua
kongamano hilo Dkt. Kida aliwataka wadau wote kutambua kwamba kazi
wanayoifanya ni ya muhimu sana kwa taifa kwani imekuwa chanzo cha
upangaji wa mipango ya maendeleo na namna inavyostahili kuwa.
Alisema
mpango wa pili wa maendeleo nchini kuelekea uchumi wa kati umechukua
fikra na falsafa nyingi kutoka katika taarifa ya Maendeleo ya Binadamu
iliyofanyiwa mwaka 2014 na kuzinduliwa mwaka 2015.
Mpango
wa maendeleo wa pili wa miaka mitano uliozinduliwa wiki iliyopita
umetumia vionjo vingi kutoka katika ripoti iliyopita na hivyo ni vyema
wadau wakachangia mada hizo na kuzipa uhai mkubwa zaidi kwa manufaa ya
Ripoti ijayo alisema Dkt. Kida.
Aidha
aliwataka wahusika wote kuwa karibu na ESRF wakati wa uandishi wa
mwisho ya ripoti hiyo baada ya kumalizika kwa kongamano hilo.
Mtafiti
mwandamizi mshiriki na Mshauri wa kiufundi wa mradi wa THDR, Marc Wuyts
akizungumzia mada ya uhusiano wa sera ya jamii na mabadiliko ya
kiuchumi katika warsha hiyo ya siku mbili inayoendelea jijini Dar
esSalaam.
Akizungumza
uhusiano wa sera ya jamii na mabadiliko ya kiuchumi (Situating Social
Policy in social economic transformation: A conceptual Framework)
Mtafiti mwandamizi mshiriki na Mshauri wa kiufundi wa mradi wa THDR,
Marc Wuyts alisema iko haja ya kutambua kwamba mabadiliko ya kiuchumi
yatafanikiwa kwa kuongeza ufanisi na tija ya kiuchumi kabla ya kugawa
manufaa yake kuimarisha huduma za kijamii.
Alisema
kukosekana kwa maunganisho na kuanza kutekeleza sera za jamii na
kusahau misingi ya kuinua uchumi, ndio uliokwamisha siasa za Ujamaa na
kujitegemea za Rais Julius Nyerere.
Alisema
ipo haja kubwa ya kutambua muunganiko na kipi kinafaa kuanza kwanza ili
kufanikisha maendeleo na ustawi wa binadamu na kutahadharisha kwamba
tafiti yoyote ambayo haitazingatia ukuaji wa uchumi kwanza hayatapeleka
taifa hili katika uchumi wa kati.
Alisema
utekelezaji wa mpango wa Mkukuta utafanikiwa ikiwa kutaangaliwa namna
ya kuunganisha mpango huo na sera ya maendeleo ya kupeleka taifa katika
uchumi wa kati.
Kumekuwa
na dhana kwamba utekelezaji wa sera zinazonyanyua hifadhi ya jamii
kunaimarisha uchumi lakini huwezi kutumia ambacho hujakizalisha.
Profesa
Flora Kessy kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe kampasi ya Dar es salaam
akizungumzia upatikanaji wa maji, usambazaji, gharama na sera zake
wakati wa kujali vipengele muhimu katika taarifa ya Maendeleo ya
Binadamu ya mwaka 2017 katika warsha ya siku mbili inayoendelea jijini
Dar es Salaam.
Mtaalamu
huyo alisema kwa kufanya kitendo hicho unakuwa unakwamisha maendeleo ya
kiuchumi kwa kuwa umetumia ambacho hujakizalisha.
Imani kuwa elementi zilizomo katika hifadhi ya jamii zinachochea ukuaji wa uchumi, ndio kisa kilichuokwamisha siasa ya ujamaa.
Mtaalamu
huyo anaamini katika mada yake kwamba ujamaa ulijali zaidi kuwaweka
watu katika hali bora na kusahau kushughulika na masuala ya kiuchumi na
hivyo kuikwamisha siasa hiyo.
Alisema ustawi wa jamii kama usipoangaliwa hukwamisha ukuaji wa kiuchumi.
Mtaalamu
mwingine Profesa Flora Kessy kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe kampasi ya
Dar es salaam alizungumzia upatikanaji wa maji, usambazaji, gharama na
sera zake (Water Provision in Tanzania- Access Financing and Policy
Trends).
Profesa
wa Elimu na Menejimenti yake, kutoka Shule Kuu ya Elimu, Chuo Kikuu cha
Dar es salaam (UDSM), Herme Mosha akichambua kipengele cha elimu katika
kuendeleza maarifa nchini wakati wa warsha hiyo ya siku mbili
iliyowakutanisha wanazuoni kuandaa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu
Tanzania ya mwaka 2017 jijini Dar es Salaam.
Katika
mada yake alisema kwamba bado kuna tatizo kubwa la utumiaji wa maji
katika usafi na pia matumizi ya vyoo. Alisema japokuwa kumekuwepo na
maendeleo katika matumizi ya vyoo, asilimia 11.5 hawana vyoo kabisa.
Aidha
alitaja mikoa ya Mara, Arusha na Manyara kuongoza kwa kutokuwa na vyoo
huku akisema wastani asilimia 7.5 hawana vyoo na Mara ikiongoza katika
kundi hilo.
Mikoa
yote hiyo ni ya wafugaji labda tabia zao za kuhamahama na mifugo yao
zinachangia. Pia profesa huyo alisema kwamba matumizi ya maji unaweza
kuona kama yapo ya kutosha kwa kuangalia suala la uoshaji mikono.
Alisema
watu hawaoshi mikono kwa maji na sabuni na mkoa wa Dare s salaam
unaongoza sana katika hilokwa wastani wa asilimia 21 huku maeneo mengine
yakiwa katika wastani wa 7 hadi 9. Alisema upatikanaji wa maji ni
muhimu katika kuonesha maendeleo ya binadamu.
Pichani
juu na chini ni sehemu ya washiriki wakiwasilisha maoni yao katika
warsha ya rasimu ya pili na ya mwisho kabla ya uhariri, inayojadiliwa na
wanazuoni hao kupitia mada 11 ambazo zitakuwapo katika taarifa ya
Maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2017.
Naye
Profesa wa Elimu na Menejimenti yake, kutoka Shule Kuu ya Elimu, Chuo
Kikuu cha Dar es salaam Herme Mosha, akichambua elimu katika kuendeleza
maarifa alizungumzia tatizo la hesabu nchini na kutaka juhudi za
makusudi kuchukuliwa kukabiliana nalo kwani maendeleo ya rasilimali watu
katika stadi ni muhimu sana kufikia uchumi wa kati.
Alipongeza
serikali kwa kuweka uwiano mzuri wa jinsia katika shule na pia ongezeko
la fedha kwa ajili ya maabara na uboreshaji wa elimu nchini.
Aidha
amesema kwamba maamuzi ya makusudi ya serikali kurejesha vyuo vya
kufunza stadi badala ya kuwa vyuo vikuu utasaidia kuwepo kwa wataalamu
wanaostahili katika kufanikisha mapinduzi ya viwanda.
Mwenyekiti
wa warsha hiyo ya siku mbili Prof. Amon Mbelle akitoa mwongozo wakati
wa kupitia na kufanyia maboresho rasimu ya pili na ya mwisho kabla ya
uhariri wa Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya mwaka 2017 jijini
Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa
Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida.
Pichani
juu na chini ni sehemu ya wanazuoni wanaoshiriki kwenye warsha ya siku
mbili ya kupitia na kufanya maboresho katika Ripoti ya Maendeleo ya
Binadamu Tanzania ya mwaka 2017 inayoendelea jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi
Kida (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanazuoni
wanaoshiriki kwenye warsha ya siku mbili ya kupitia na kufanya maboresho
kwenye Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu Tanzania ya mwaka 2017 jijini
Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment